Naibu katibu mkuu wa CCM taifa umetia aibu

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
2307bd3c6f9f84259dbe893a54eef856.jpg


Viongozi wa ccm Taifa wakiongozwa na Naibu Katibu mkuu wa ccm taifa (visiwani) Dr Abdallah Juma Mabodi akiambatana na waandishi wa Habari ameamua kwenda kumjengea Nyumba Kada wao Mtiifu na tena Balozi nyumba ya kuishi.

Yaani Dr mzima tena kiongozi wa kitaifa wa chama tawala kama bado wanapambana makada wao waishi kwenye nyumba za hivi Miaka 50 ya uhuru sisi wananchi tunategemea jipya Gani sasa.
 
Binadamu bana! Ingekuwa ni ghorofa inajengwa msingekosa la kusema.Sasa hiyo ni nyumba ya kawaida sana vijijini bado mnasema?Uwezo wa huyo mwenye nyumba ndio huo, afanyeje sasa?
 
Ccm ujinga, umasikini na maradhi ndio tawi walilolikalia, hivyo kwao ndio furaha yao kubwa kuona uduni wa maisha ya Watanzania ukitamalaki, hivyo ukiona hivyo ni usanii tu unafanyika kulaghai Watanzania lakini hawako na nia njema na nchi hii hata kidogo
 
Mwita ajaelimika. Kuelimika ni pamoja na kujitambua na kuitambua jamii yako. Katika jamii ya watanzania wapo watu wengi tu wanao ishi katika nyumba za udongo na nyasi. Wanapo pata matatizo wanatakiwa kusaidiwa kama anavyo fanya huyo naibu katibu mkuu. Na ndio maana ccm inapendwa na kuheshimika kwa sababu ya kugusa hisia za watu na hasa wanyonge. HONGERA SANA NAIBU KATIBU MKUU. wanao pinga jambo kama hilo ndo wanatia aibu, mi nawashauri waelimike.
 
Haya bhana! Tanzania ya viwanda,viongozi wa nchi wanamjengea nyumba kada mwenzao
Hawa ndio wanaotupeleka kufikia uchumi wa kati (kama Hong Kong) wakitumia ujuzi na weledi wao wote
 
2307bd3c6f9f84259dbe893a54eef856.jpg


Viongozi wa ccm Taifa wakiongozwa na Naibu centreatibu mkuu wa ccm taifa (visiwani) Dr Abdallah Juma Mabodi akiambatana na waandishi wa Habari ameamua kwenda kumjengea Nyumba Kada wao Mtiifu na tena Balozi nyumba ya kuishi.

Yaani Dr mzima tena kiongozi wa kitaifa wa chama tawala kama bado wanapambana makada wao waishi kwenye nyumba za hivi Miaka 50 ya uhuru sisi wananchi tunategemea jipya Gani sasa.
Hakuna haja ya kuficha hali halisi. Nyumba za aina hii zimejaa tele km chache tu toka city center kwenye miji kama Tanga na Zanzibar ndo usiseme. Lakini pia umasaini kuna nyumba ambazo ni ngumu kuamini kama binadamu anaweza kulalamo. Lililo la mhimu si kubezana, tuna wajibu kwa ujumla wetu sote kuirekebisha hali hii.
 
Nakubaliana na wafanyakazi wa Kilimanjaro waliosema kuwa huu ni muda wa "Hapa kero TU" maana hapo huyo balozi anaongezewa kero za maisha na ikifanywa na viongozi wa kitaifa.
 
halafu ni DR nimetoke kuwadharau sana ma DR na ma Pro wa Tanzania wnafanya mabo ya kijinga sana, nadhani walikuawanasoma ili wapate mishahara tu na sio ubunifu na kuwakomboa watanzania, sioni tofauti yao na kibabaji wa mtera
 
Back
Top Bottom