Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa ajiuzulu nyadhifa zake kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na mbunge wa Moshi Vijijini

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, ametangaza kujiuzulu nyazifa zake, kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na mbunge wa Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu. Anaandika Hamis Mguta…(endelea).

Akizungumza katika ofisi za MwanaHALISI, leo Jumapili, tarehe 15 Desemba 2019, Mtemelwa aambaye ni mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini alisema, ameamua kujiuzulu nyadhifa hizo za uongozi, ili kuwabika kwa kilichotokea.

“Mazungumzo yetu yalikuwa ya faragha sana. Nawajibika kwa kuvuja kwa mazungumzo hayo, wakati yalikuwa bado hayajaiva,” ameeleza Mtemelwa.

Amesema, audio inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inalengo la kumgombanisha yeye na chama chake, yeye na viongozi wenzake, pamoja na wanachama na wafuasi wa ACT- Wazalendo, “waliotapakaa nchi mzima.”

Mtemelwa anakiri kuwa alifanya mazungumzo na Komu, yenye lengo la kumshawishi mwanasiasa huyo, kujiunga na chama chake.

Hata hivyo, anasema kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye video hiyo, yamehaririwa kwa kiasi kikubwa na watu anaodai kwua wana lengo baya dhidi ya ACT- Wazalendo na viongozi wake.
Amesema, “kwenye audio inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inayonihusisha mimi, Zitto Zuberi Kabwe, Maalim Seif Shariff Hamad na watu wengine, imetengenezwa kwa nia ovu ya kutaka kukivuruga ACT-Wazalendo.”

Maalim Seif Hamad, Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo
Anasema, “ni ukweli usio na shaka kwamba maneno hayo yaliyoingizwa kwenye audio hiyo, yamewekwa kwa nia ovu ya kunigombanisha mimi na chama changu; na mimi na viongozi wangu; na kazi hii chafu, imefanywa na watu wenye nia mbaya na chama chetu.

“Mimi binafsi, sijawahi hata mara moja kumvunjia heshima Maalim Seif, kwa kuwa ni mtu ninayemheshimu sana. Amejitolea muda wake mwingi kujenga demokrasia katika nchi yetu, na kwa nafasi alizoshika na hadhi aliyonayo, ni vitu ambavyo havifanani na kwa mtu anayemjua kama mimi, nisigeweza kusema maneno ya aina hiyo.”

Akimzungumzia Maalim Seif, Mtemelwa anasema: “Kwangu mimi, Maalim Seif amekuwa mwalimu wangu wa siasa, baba, rafiki na mlezi na katika kipindi nilichokuwa naye karibu, nimegundua yanayosemwa juu yake, ni tofauti na yeye anavyoishi.

“Ninamheshimu sana Zitto kutokana na historia yetu ya mageuzi na tulikotokea. Nafahamu madhara ya migogoro kwenye vyama, hasa vyama hivi vyetu ambavyo havijawahi kushika madaraka ya nchi. Kwa hivyo, kwa vyovyote vile, nisigeweza kuzungumza maneno hayo kama yanavyonukuliwa.”

Alipoulizwa kutokana na kadhia hiyo ameamua kuchukua hatua gani, Mtemelewa anasema, “kwanza, namuomba radhi Maalim Seif na familia yake; namuomba radhi Zitto, naiomba radhi Kamati Kuu (CC) ya chama changu.

Source: Mwanahalisi online



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto na ACT haiwezi kuteteleka huyu jamaa kuhamia ccm

chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi mkuu 2020 kipo imara na kinajiandaa kuchukua nchi

kwa upande wa zanzibar ndio chama tishio kwa sasa

Huyo jamaa kuhama chama ni sawa na Sisimizi kumwangusha tembo, anapoteza muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona umeshindwa kunukuu kilicho zungumzwa katika hiyo audio ? Ulikua unataka kuwa Wa kwanza kupost ? Kiini hakipo hapo mnatupotezea muda

Wakati mwingine Kama huna data kamili usianzishe Uzi ntakupiga vibao mimi
 
Chadema ni mabingwa wa kudukua lakini hawaishi kuwatetea akina Nape, January ,Kinana na Ngeleja........hawa jamaa ni bure kabisa!
nilisema, nilikuwa nakuona kama mtu vile, wa maana, kumbe ni hao hao praise team. Nakumbuka enzi za ujima, mtawala wa wakati huo akijamba, wanaomzunguka wanaitikia kwa kusema mfalme amemwaga chakula... ndiko mnakoelekea kwa Jiwe! Kuna siku atajamba mtakimbia kuvuta ushuzi mpate baraka! It is not far from today!
 
nilisema, nilikuwa nakuona kama mtu vile, wa maana, kumbe ni hao hao praise team. Nakumbuka enzi za ujima, mtawala wa wakati huo akijamba, wanaomzunguka wanaitikia kwa kusema mfalme amemwaga chakula... ndiko mnakoelekea kwa Jiwe! Kuna siku atajamba mtakimbia kuvuta ushuzi mpate baraka! It is not far from today!
Hapo jiwe anaingiaje?!

Msafiri amejiuzulu.......tunasubiri kauli ya Komu!
 
ACT wazalendo ni chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi 2020.

Hata mawe yarushwe vipi nyumba imeshakuwa imara na imejengwa kwa mawe.
 
Back
Top Bottom