Naibu amiri wa jumuiya ya uamsho awasili Zanzibar akitokea Oman | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu amiri wa jumuiya ya uamsho awasili Zanzibar akitokea Oman

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kijana Msomali, Jun 1, 2012.

 1. K

  Kijana Msomali Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Naibu Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Azzan Khalid Hamdan amewasili leo katika uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Oman. Sheikh Azzan ni miongoni mwa viongozi wanaotafutwa na Jeshi la Polisi.

  Baada ya kufika uwanja wa ndege tu amekwenda nyumbani kwake na kufika nyumbani kwake huko mfenesini amekuta nyumba yake imeathirika kutokana na mabomu yaliopigwa wakati yeye akitafutwa na jeshi la polisi

  Sheikh Azzan amekwenda kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kuhusiana na kadhia aliyoikuta nyumbani kwake na pia kuulizia iwapo yeye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi.


  Baadhi ya maoni ya wakaazi wa Zanzibar kuhusu ujio wa naibu amiri wa JUMIKI na taarifa za kutafutwa kwake na Jeshi la Polisi.

  • [​IMG]Nurdin Moh'd Hao polisi bora wamuache patakuja kuwa hapatoshi bure.


  • Juma Awadhi hawana lolote hao vibaraka tu  • [​IMG]
   Salim Seif
   maandamo akapokewe?
  • [​IMG]
   Juma Awadhi
   hawana lolote hao vibaraka tu na insha-allah tutaomba dadaetu utujaze huko badae hali ilivokua lkn hao wanaokamata mashekh watapambana na ALLAH mwnyw!
  • [​IMG]
   Masoud Khamis
   Karibu nyumbn Sheikh wetu jidai unawatu wakufanaweye

   [​IMG]

   Mohamed Jabir
   Allah kwa hakika hatokuwa pamoja na wao na mwenyeezimung awalinde viongozi wetu wote wa harakati mpaka kieleweke. Lengo lao tayari tumekwisha lielewa na m/mungu atupe nguvu za pamoja inshaallah. Mungu atawahukumu hapa hapa duniani kabla ya yaumulkiyama. Mwenyezi mungu tupe umoja zaidi katika kudai HAKI YETU.  My take

  Katiba ya Jamhuri inatoa haki ya kila mwananchi kuzungumzia fikra zake na kutoa maoni yake katika kila jambo, liwe linahusiana na siasa, afya, elimu, miundo mbinu na hata muungano ILA haki hiyo haimpi mwananchi kutenda jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wake mwenyewe, usalama wa jamii inayomzunguka na taifa kwa ujumla.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Wamezoea kupewa amri na waarabu. Tutawasaidiaje?
   
 3. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  My take on Zanzibar issue... the Zanzibar Government knew this issue for a long time and kept quite all along... and they have let is be so for years so it is time they start to act on this issue if they true serious..
   
 4. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Martin David
  Serikali ni wananchi, viongozi wafanye vile wananchi wanaona inafaa.
  Mimi nadhani Serikali ipo right kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao. (not kuchoma makanisa).
  Wapeleke tu kura ya maoni.
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Karibu ZNZ amir l muuminin.
   
 6. W

  Wakumulika Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu waislam tufanye harakati ambazo ajenda zake tunazifahamu, kama huyu naibu amekuja toka oman hata kikinuka yeye atakuwa wa kwanza kukimbilia oman, hebu jiulize ndugu yangu mzanzibar wa makunduchi,kojani pemba na kwingineko zanzibar ambaye hata mlo wa siku moja unatusumbua hata kuweza kupata nauli ya kupanda sea bus huna utakimbilia wapi? hebu tushabikie mambo yanayo lenga kutupa maendeleo na siyo yale yanayolenga kumpa sifa na kumtukuza mtu
   
 7. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Saturday, 02 June 2012 09:34 0digg

  Salma Said, Zanzibar
  KIONGOZI Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) ambaye pia anadaiwa kuwa mfadhili wa kundi hilo, Sheikh Azzan Khalid Hamdan amewasili jana jioni katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar kutoka nchini Oman alipokwenda kwa ajili ya matibabu, kisha kukamatwa na polisi.

  Sheikh Azzan ni miongoni mwa viongoni waliokuwa wakisakwa na polisi akihusishwa na vurugu zilizotokea wiki iliyopita ikiwa pamoja na kufanya maandamano bila kibali.

  Baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege, Sheikh Azzan alikwenda moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Mfenesini kujisalimisha na kutoa taarifa kuhusu kuvunjwa kwa milango ya nyumba yake wakati akiwa safarini.

  Kukamatwa kwake kumekuja siku moja tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ally Mohamed Shein atoe ahadi ya wahusikawa vurugu hizo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

  Sheikh Azzan alisema hakutoa taarifa za ujio wake huo kutokana na kuogopa mkusanyiko usio rasmi ambao ungeweza kusababisha kutokea vurugu nyingine visiwani humo.

  “Unajua hamasa za watu ni kubwa hasa vijana wangekuwa wamepata taarifa za kuja kwangu basi wangejaa hapa uwanja wa ndege na jambo hilo lingeweza kuhatarisha shughuli za uwanja huu ndio maana nikaamua kuja kimya kimya,” alisema Sheikh Azzan muda mfupi baada ya kushuka katika ndege ya Shirika la ndege la Oman Air.

  Wakati Sheikh huyo akiwa safarini Oman, Zanzibar kulitokea maandamano ambayo yaliandaliwa na viongozi wa jumuiya yake yalioanzia Viwanja vya Shule ya Lumumba kupitia barabara ya Kinazini, Michenzani, Biziredi na kuishia katika viwanja hivyo vya Lumumba, kisha kufanyika mhadhara mkubwa uliozungumzia suala la mfumo wa elimu na matokeo mabovu ya mitihani Zanzibar.

  Hata hivyo, maandamano hayo yalibandikwa jina la matembezi ya amani yalikwisha salama na waandamanaji wakarudi majumbani, lakini baada ya muda, kulizuka ghasia muda mfupi baada ya kiongozi na mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma kukamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.

  Kiongozi huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Madema Mjini Zanzibar na kusababisha mamia ya vijana kufika katika kituo hicho wakitaka aachiwe, na waliapa kutoondoka kituoni hapo hadi asubuhi, kitendo ambacho kiliwalazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi usiku kucha na vurugu hizo kuendelea hadi siku ya pili.

  Jeshi la polisi bado linawatafuta viongozi wengine wa jumuiya hiyo walioandaa maandamano hayo akiwamo Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Abdallah Said Madawa, Sheikh Fikirini Majaaliwa Fikirini, Sheikh Suleiman Juma, na Sheikh Sadifa Haji Sadifa.


  Katika vurugu hizo makanisa matatu yalichomwa moto na mali kadhaa kuteketea ikiwamo magari na nyumba za watu.

  SOSI; Mwananchi!
   
 8. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hawa uamsho walikuwa wanasema hawana wafadhili inakuaje tena leo mfadhili wao amekamatwa tena
   
 9. B

  Bull JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kumekuwa na mipango ya makusudi liliyoandaliwa na Makanisa wakishirikana na Viongozi mafisadi kujaza Makanisa Zanzibar na kuhodhi ardhi ya Wazanzibari,

  Makanisa hayo yamejazana kama uyoga yakfuatiwa na Migahawa ya nyama ya Kiti moto, baa na umalay uliokithiri mitaani

  Zaidi ya 98% ya WaZanzibari ni Waislam, ukuwaji wa makanisa hauwiani kabisa na idadi ya wakiristo wahamiaji waliopandikizwa kwa ajili ya kuaribu mila na dasturi za Wazanzibar

  Kama Wazanzibari hamtokuwa makini, basi mtakuwa kama Wapalestina walivyo porwa ardhi yao na Waizraili
   
 10. salito

  salito JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  chenga..
   
 11. M

  Mathy laut nyami Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini zanzibar si sehemu ya tanzania sasa inakuwaje mseme watu wa bara wamepandikizwa na nani kakuambia malaya ni wakristo tu au ndo dhihaka zenyewe hizo.
   
 12. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180


  mmmhhhh
   
 13. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  waropokaji hao
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Wabara tumezubaa sana. Ingekuwa juu yangu walahi wangejuta hawa Wazanzibari.
   
 15. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Inferiority Complexion.


  Siku zote mtu duni humuogopa mgeni kwa kutambua kuwa uduni wake utamfanya apoteze alichonacho.

  Unazungumzia umalaya kama kitu kigeni ambacho kinaletwa na wanaotoka bara...unachekesha sana wewe. Kaa hapo Hotel inayoitwa Adams Inn halafu angalia chini huku Malindi Guest House mida ya asubuhi kisha uniambie wale ni Wabara?

  Mimi nimewahi kuona watu wakiendekeza ngono lkn hii ya ZNZ ni mpya kwa watu kuingia Gesti saa 2 asubuhi na vitoto vidogo sawa na binti zao. Mibaibui mnayojifunga ni kuficha sura zenu ili msibainike mnapoingia gesti.

  Huku upande wa Makumbusho niliona wanaume wanajiuza kama wanawake na polisi wako nao kama wanachofanya ni sawa. Je, na huu utaratibu wa kuingiliana wanaume kwa wanaume nao umetoka bara? Au ndio ustaarabu wenu mnaoogopa utapotea endapo wageni watakuja?

  Kinachokufanya uogope kanisa ni nini? Kama unaamini watu ni waislamu kwa hiari yao basi acha makanisa yajengwe, si yatakuwa tupu kwa kukosa waumini au shida yako nini?

  Hivi kitimoto kama huli unakiogopea nini? Wasiwasi ni kwamba dini yenu watu wapo kwa kulazimishwa. Unajua kuwa kukitokea second option watu watahamia huko na ndio maana mnapinga kwa vurugu. Just preach yours kama kweli mnajiamini, nini vurugu?
   
 16. M

  MTU WA VITA Member

  #16
  Jun 2, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo hapa ni kushughulikia muungano kwanza tuoondoe utata uliopo na kupingana ka katiba ya muungano na zanzibar
   
 17. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Apigwe mvua huyo kama hosain mubarak au taylor.
   
 18. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,316
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  [h=2][/h]
  [FONT=&amp]Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza.
  Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini.

  Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar.

  Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini.

  Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu. [/FONT]

  [FONT=&amp]Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini." [/FONT]

  [FONT=&amp]Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini.
  Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia.

  Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini.

  Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza![/FONT]

  [FONT=&amp]Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko.

  Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhalimu ya Tanzania.

  Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere.

  Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa?

  Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini.

  Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo.

  Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere?

  Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini.

  Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda.

  Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika.

  Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada.

  Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama.
  Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo.

  Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni.

  Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini".

  Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani.

  Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika.

  Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa.

  Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika.

  Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma.
  Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba.

  Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara.

  Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza.

  Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula.

  Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo.
  Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso.

  Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma.

  Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena.

  Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao.

  Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza.

  Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka.
  Lakini, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhahiri shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani.

  Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani.

  Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake.

  Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu.

  Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu.

  Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu.
  Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda.

  Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.[/FONT]

  [FONT=&amp]Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?"

  Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake.
  Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao.

  Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao.

  Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa.

  Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa.

  Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

  Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.[/FONT]
   
 19. k

  kichakare Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  zanzbar ni Tanzania na hatuna utamaduni wa kubaguana kwa udini wala ubara na uzanzibari. maendeleo hayaji kwa kuwa na watu wa aina moja tena wenye fikra mgando kama alivyo BUll. ina maana mashoga na machangudoa wote ni watu wa bara? anapaswa akamatwe kwa uchochezi.
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  kwamwewe Mkuu, hii "khabari" yako hapa ina"khusiana" na nini ku"khusu" Mfadhili wa Uamsho mbaroni?