Nahujumiwa na Tanesco

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,730
519
familia yetu tumekuwa wateja wazuri saana wa tanesco tangu miaka ya 80, na tumekuwa tukilipa bili bila usumbufu, tatizo limekuja mwaka huu mwezi wa 5, nimeletewa bili ya mil 4, wakati sikuwa na deni lolote, na wastani wa units tulizokuwa tunatumia tangu 2005 ni 150 units, nilipohoji deni linatoka wapi, nimejibiwa kuwa msomaji wa mita wa tanesco alikuwa anasoma mita vibaya tangu 2009, wakasema huyo mfanyakazi watamwajibisha, nikahoji kama ndivyo ina maana katika matumizi yangu kabla ya 2009 yalikuwa sahihi, wakasema ndio. kama ndivyo iweje kusiwe na tofauti ya wastani wa matumizi ya bili, kwani ukiangalia wastani wa matumizi ya umeme 2008 na 2009 hakuna tofauti, ni unit 120 wastani wa miezi 5, nilienda makao makuu ya tanesco wakaniambia hayo mazungumzo uliyofanya na viongozi wa mkoa yawekeni kwa maandishi na wenyewe wakujibu kwa maandishi ndo uje huku, lakini viongozi wa mkoa wamegoma hata kupokea barua niliyoandika, ukienda wanasema lazima ulipe hili deni! naomba msaada wenu wa mawazo namna ninayoweza kufanya
natanguliza shukrani.
 
Tumia mawakili, waandikie barua ya kuomba maelezo ya maandishi ya yale mliyongea kwa mdomo siku za nyumba, ambatanisha na barua ya kusudio la kuwafikisha mahakamani!

Wakikaidi wafikishe mahakamani utashinda na kulipwa fidia zote,

Mawakili wengi kwa sasa ni bei rahisi sana mkuu, kama huna uwezo nenda pale kijitonyama pana kituo cha msaada wa kisheria watalisimamia suala lako mpaka mwisho
 
asante sana mkuu nitaenda mkuu, ni kijitonyama sehemu gani!
 
pole sana mkuu.hata sie kwetu wamekuja na wametukatia umeme mwez sasa tena hata maelezo kwan tulikuwa tukinunua umeme unakaa tulivyoenda kufatilia wakasema mna den wakati mita n ya luku,limetokea wapi!wakat wa uchunguz ilionesha mna unit nying kwenye luku wakat kwenye comp mmelipia kdogo.so mmenunua illegal units.mimi kama mteja tajuaje kama hz n illegal.yaan tanesco waonevu sana.
 
tatizo tanesco wanatumia ubabe, wakisha amua wameamua hakuna maelezo, hili ni tatizo
 
yani hawa jamaa nina hasira nao vibaya sana na j3 lazima niwawashie moto wa maana coz kwenye nyumba yangu ya mbeya ambapo yupo wife na mtoto walileta bili laki 6 ya mwezi 1,wakidai kuwa ni deni la nyuma wakati huo cjawahilimbikiza tangu 2004 na risiti zote ninazo. Hayo yote kafanyiwa wife! Juzi tena wameleta bili ya elfu 50 wakati umeme umekatwa mwezi na nusu sasa!
Hapa nipo njiani naelekea Mbeya kutoka Dsm. Yani hili ni shirika la uma kandamizi kuliko yote.
Watanzania tuinuke tupambane na huu uonevu wa hii serikali 'sikivu'
 
mkuu pole saana cha msingi tukomae kuhakikisha haki inapatikana
 
Dawa ni kuwaibia umeme tu wakija kukagua nafungulia mijibwa kama sita hivi senzi !!!!!!
 
Jaribu kumuona katibu mkuu Maswi au Waziri Mhongo Tanesco kuna watu wawili tu pale wengine wote ni sawa na kukanyaga tope. Ninapoongea hapa nina kesi nao iko mahakama kuu karibia mwaka sasa na mda wote huo natumia majenereta kwenye biashara yangu ya duka kubwa la madawa inabidi nitumie majenereta makubwa mawili ili kuyapumzisha. Nimekuwa nikitumia LUKU kwa miaka saba iliyopita lakini wameleta deni la 17,000,000/= eti ni la kabla sijafungiwa LUKU. Pale ni uchafu mtupu, ila wakati nafungua kesi kama Mhongo na Maswi wangekuwepo ningewaona kwanza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom