Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,720
- 21,778
Habari zaidi!
Nahodha, Shamuhuna kuhitimu OUT
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Saturday,October 25, 2008 @00:03
Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu wake, Ali Juma Shamuhuna, ni miongoni mwa wanafunzi takriban 1,000 watakaotunukiwa vyeti vya kuhitimu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yanayofanyika leo.
Viongozi hao wa juu katika SMZ walikuwa miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho wanaohitimu mwaka huu, waliohudhuria mkutano wa 18 wa wanazuoni uliofanyika chuoni Biafra, Dar es Salaam.
Nahodha atatunukiwa Shahada ya Uzamili katika Utawala na Biashara (MBA) wakati Shamuhuna ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, atatunukiwa Shahada ya Kwanza ya Uchumi.
Mbali na viongozi hao, pia Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Zainabu Kwikage atahitimu Shahada ya Kwanza katika mahafali hayo ya 20 yatakayofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni. Akizungumza katika mkutano wa jana, Nahodha aliwataka wahitimu wenzake kufanya kazi kwa bidii na kwa utaratibu, ikiwa ni pamoja na kuendelea kusoma masuala mbalimbali.
Alisema ni vigumu kutawala katika nchi zinazoendelea hivyo baada ya kupata cheo hicho cha Waziri Kiongozi, ndipo alipoamua kujiunga na chuo hicho na kuwataka Watanzania kusoma ili kuongeza uelewa wa mambo mbalimbali kila wakati. Aidha, Nahodha aliwaasa Watanzania kutopenda kupata vyeti vya urahisi kwa kutafuta vyeti bandia au kusoma katika vyuo visivyoeleweka, bali wajiunge katika vyuo vinavyotambulika na serikali.