Nahodha na majina ya walarushwa uhamiaji - achukua hatua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha na majina ya walarushwa uhamiaji - achukua hatua!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha, amewanyooshea vidole maafisa wa Idara ya Uhamiaji ni vinara wa rushwa katika utoaji wa hati za kusafiria na kuwaingiza wahamiaji haramu nchini.

  Katika kuthibisha kuwa vigogo hao wanahusika na rushwa, Nahodha alisema tayari ana majina ya maafisa nane wa makao makuu ambao wametajwa na wateja kuwa wamekuwa vinara wakuu wa kupokea rushwa katika Idara ya Uhamiaji.

  Waziri Nahodha alisema hayo mjini Morogoro wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa tathmini ya utendaji wa kazi kwa viongozi na watendaji wakuu wa idara hiyo kutoka makao makuu, mikoani na mipakani.

  Alisema kuwa idara ya uhamiaji hivi sasa inahusishwa na urasimu,vitendo vya rushwa, kuingiza na kukumbatia wahamiaji haramu pamoja na ukosefu wa maadili ya kazi.

  "Kuna vitu ambayo vinaweza kutolewa maamuzi kwa hata siku moja au tatu, lakini nyinyi maafisa wetu mnawazungusha mpaka mwezi mmoja ili kutaka kujiharalishia vitendo vya rushwa," alisema. Kuhusu kukithiri kwa rushwa katika Idara hiyo,Waziri Nahodha alisema kuwa ilifanyika tathmini kwa idara za serikali zinazoongoza kwa rushwa na Uhamiaji ilitajwa kushika nafasi ya tatu.

  Alifafanua kuwa maafisa hao wamekuwa wakijihusisha katika kupokea rushwa kwa kuwaombea hati za uraia wa Tanzania baadhi ya wageni kwa kupindisha sheria na taratibu zilizopo za kuomba uraia baada kupewa fedha na wageni hao.

  "Kuna afisa mmoja alikuja ofisini kwangu akitaka niidhinishe uraia wa Tanzania kwa Mhindi mmoja katika barua ya kumuombea, alitaja kuwa alichimba visima viwili vya maji kusaidia wananchi," alisema Nahodha na kuongeza:

  "Visima hivyo hata Mtanzania anaweza kuvichimba,nilikataa kufanya hivyo najua tayari alishampa rushwa." "Na mwingine alileta hati ambayo haijakamilika na kueleza kuwa huyo ni mwekezaji ana bekari ya mikate hivyo nimpe hati ya uraia wa Tanzania. Hivi kuwa na bekari ni uwekezaji unaojitosheleza kumpatia uraia?" alihoji.

  Waziri huyo alisema Idara ya Uhamiaji hivi sasa imekosa uadilifu na maadili kwa kuwa kila mtu anajifanyia anachotaka huku wakimpelekea yeye (Waziri) kazi ambazo zinapaswa kufanywa na maofisa. "Kuna maafisa wanawaambia wateja wao kuwa faili lako lipo kwa Waziri baada ya kuchukua kitu kidogo, na wale wanakuja kwangu moja kwa moja wakitaka nishughulikie mafaili yao wakati mimi sikai na mafaili hayo," alisema

  Kuhusu maofisa wa Uhamiaji waliopo mipakani, alisema wanajihusisha na vitendo vya kuwaingiza wahamiaji haramu, baada ya kuwapatia fedha kiasi kisichopungua Dola za marekani 1,000, hali inayosababisha wahamiaji kuzagaa nchini.

  Alisema licha ya kuwaingiza wahamiaji hao, pia maafisa hao wamekuwa wakiwalinda jambo ambalo alisema alikubaliki na ni kinyume cha maadili.

  Kadhalika, alisema vitendo hivyo ni aibu ikizingatiwa kuwa idara hiyo ni sehemu ya ulinzi na usalama wa nchi. "Ninawapa mwezi mmoja maofisa wa mikoa mlete taarifa ya namna mlivyodhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu na changamoto, ikishindikana sitakubali niadhibiwe na Bunge.

  Nnyinyi ndio mtakuwa wa kwanza na nalisema hili si kama natania au ni mazoea ya wanasiasa, mtaona wenyewe," alionya. Hata hivyo, alisema ili kumaliza tatizo hilo, Idara ya Uhamiaji inapaswa kuanza kushirikiana na Jeshi la Polisi na Magereza kwani vyombo hivyo viko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Kwa upande wake, Kamishna wa Uhamiaji, Magnus Ulunga, alikiri kuwa baadhi ya maofisa wa idara hiyo wanajihusisha na rushwa na kuongeza kuwa tatizo hilo pia lipo katika idara nyingine za Serikali.

  IPPMedia
   
 2. K

  Kampemba Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hii Kampuni ya Uhamiaji imesajiliwa Brela kweli maana sidhani kama ni ni moja ya Idara za serikali sababu iko kibinafsi zaidi,Ni mtazamo tu wana JF
   
 3. b

  blacktanzanite Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wametujazia wachina maskini wenzetu,ongera sana..
   
 4. D

  Divele Dikalame Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhamiaji siku hizi wameanzisha kitengo cha intelijensia kumejaa wasanii kibao,wala rushwa mtu hata kiingereza kidogo tu hajui hii tabia ya kupeana kazi kindugu ni mtihani sana.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Cha ajabu anasema ana majina ya vigogo ngazi ya juu na wengine wameingia hadi ofisini kwake kushawishi apitishepitishe mambo, sasa kama anajua hivyo kwa nini asichukulie hatua badala ya kulalamika jukwaani kama mie?
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  wakuu uhamiaji pameoza! Wame na wanatuharibia nchi.wahindi wahamiaji haramu wamejaa,kwanini wasivamie maofisi ghafla waone? Uhamiaji wanaharamisha haya na maafisa wanao deal na wahindi tunawajua!
   
 7. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mhariri NIPASHE
  28th October 2011

  "Juzi akifungua mkutano wa siku tatu wa tathmini ya utendaji kazi kwa viongozi watenfaji wakuu wa Idara ya Uhamiaji kutoka makao makuu,Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsa Vuai Nahodha, aliwaonyooshea vidole maafisa wa idara hiyo kuwa ni vinarawa rushwa katika utoaji wa hati za kusafiria na kuwaingiza wahamiaji haramu nchini."

  Hii ni kali sana.

  Wananchi wanafahamu hivyo, Serikali nayo inafahamu hivyo. Ni lini hatua zitachukuliwa?

  Kuichekea rushwa kunarudisha nyuma maendeleo.

  Katika pita pita zangu wiki hii nimepata hanbari kuwa ile kampuni inayofanya utafiti wa mafuta pwani ya Mtwara/Lindi wanataka kuhamishia shughuli zao huko Msumbiji kwa vile wansumbuliwa sana na kuombwa rushwa na Uhamiaji, ili kupata visa.

  Tukumbuke meli hii ndiyo iliyozinduliwa huko Korea na Waziri Mkuu,Mh Pinda.

  Ni kichekesho vile vile wakati DCI Manumba akipambana na Al Sbabab, na kuna tetesi kuwa wanapata pasi za kimipango Wizara hiyo hiyo ya Mambo ya Ndani!!!!
  Nji hii bwana!!!
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  atachukua hatua kwani ni nchi yake?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kama walivyo weng.ne jukumu lake yeye ni kuongea tu,tanzania hakuna utamaduni wa KUSAFISHANA,ila kuna utamadun wa watu kulalamika kua WANACHAFULIWA,nahodha mwenyewe anaonesha ameelemewa
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Haka kaidara kama kamesahaulika! Ni idara nyeti sana pale rushwa ni live kwa wahamiaji haramu hasa wahindi.sijui system inafanya vp kazi.hakuna watu wa TISS mle watoe tahadhari ya hatari hii? Mbinu za namna ya kuishi hapa wanatoa hao hao uhamiaji.nachukia sana jinsi wahindi na siku hizi wachina kugeuza nchi hii shamba la bibi na hata ukizungumza na wageni hao wanatubeza tu! Lazima pale uhamiaji pawekwe intelejinsia makini ili kuwafunza adabu watumishi wa ovyo.watumishi wa uhamiaji watoto wao nao wanahangaika na ajira while wao wanasaidia wahamiaji haramu wanaokuja kama maexpert feki wanaishia kufanya kazi za kawaida kabisa.naomba vijana wajue uhamiaji ndio adui wao wa tatizo la ajira kwa sasa nje ya mambo ya kisiasa.
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  kila mhindi utakae muona ofisini jua ni mhamiaji haramu! Wahindi wakibongo wachache sana wengi tunaowaona maofisi details zao feki na uhamiaji wanajua na hawajawahi kufanya operation za siri maofisini
   
 12. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,212
  Likes Received: 3,822
  Trophy Points: 280

  Porojo tu hamna chochote. Atanyamaza huyo Vuai, ni sautinya maporomoko ya maji, yatazoeleka
   
 13. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
 14. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mpaka tupate rais makini, serious na mwenye dhamira ya kushughulikia mambo hayo
   
 15. A

  Akiri JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  huyu anachekesha eti ana orodha ya majina nane ya vigogo wanaopokea rushwa hapo uhamiaji, yaani majina nane tu ndiyo yanakuwasha mpaka unatangaza. mwenzio jk anayo orodha ya majina ya wara rushwa , wauza madawa ya kurevya na wezi wa epa lkn kauchuna tu, we majina nane unaitisha waandishi. we jaribu kuyapeleka kwa bosi wako akayaunganishe na yale mengine , ili meza yake izidi kujaa makabrasha.
   
 16. S

  STIDE JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bora hata Wahindi, hakuna mdudu aliyembaya na simtaki kama Mchina!! Hivi hii serikali inatutakia nn!!? Yaani utashangaa vichina vinauza sasa maua, machinga hadi mafundi Randa wamo nchini!! Kibaya zaidi vunasema "Tz imo mifukoni mwetu!!"
  Tz watu wanaingia kama wanaenda BUCHANI!! Serikali inaangalia tu, na hawa ndugu zangu ndio mkosi wa ajira nchini!
  Ndg zangu wana jf, jitahidi utoe siku moja tu na utembelee makampuni ya Waarabu, wahindi na wachina uone ndg zenu wanavotaabika na kunyanyaswa, ni aibu tupu!! Angalia maisha ya wafanyakazi hao, mi waambia ukimuona mfanyakazi ana kiatu ama nguo mpya, toa taarifa mods wanipige ban mwezi mzima!!
  Tz tz tz tz tz tz TANZANIA!!!!
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  naanza kuwaelewa wa south africa walituchukia hadi sisi wenye rangi kama yao! Hii ni hatari!!
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Idara nzima imeona hadi kamishna wao angalia alivyojibu hoja ya rushwa idarani kwake!!ni aibu na anastahili kuwajibishwa kabisa anasema hata idara zingine zina rushwa!!kwelii!!!badala kutaja mikakati kupambana na hizo rushwa na uhamiaji haramu mipakani yeye anasema kama idara zingione za serikali!!!
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kama waziri anatakiwa kuchua hatua sio kulialia.
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  business as usual,inakera kweli!! We jua tu kila mhindi na mchina unaemuona 90% ameingia ki magumashi.nchi yenyewe changa hii effect inakuwa kubwa sana
   
Loading...