Nahodha ahofia amani kutoweka nchini

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Na Peter Twite

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, amesema kuna dalili za kutoweka maadili miongoni mwa jamii jambo linalotishia kuwepo machafuko yanayoweza kusababisha kutoweka amani nchini.

Bw. Nahodha aliitoa kauli hiyo, alipozungumza katika ibada maalumu ya kuwekwa Wakfu Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God Tanzania (PAG) jana jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ibada hiyoiliyofanyika katika Kanisa hilo,Kinondoni, Bw. Nahodha alisema anaona kila dalili za kutokuwepo maridhiano, upendo, upole na uaminifu miongoni mwa jamii ya Watanzania mambo ambayo yanaweza kuleta machafuko katika jamii yetu.

"Naziona kila dalili kwenye ubao, naziona dalili za kutoweka kwa maridhiano, upendo, upole miongoni mwa Watanzania,uaminifu katika jamii yetu,mashauriano miongoni mwa viongozi, mambo haya yasipokuwepo ni hatari kwa taifa letu linalosifika kwa amani na utulivu kwa miaka mingi," alisema.

Aidha, Bw. Nahodha alisema kuwa zipo dalili zinaanza kujitokeza nchini watu wanaanza kutazamana kwa misingi ya dini zao, hakuna kuhurumiana jambo ambalo ni hatari kabisa kwa kujenga misingi ya umoja wa katika taifa letu.Bw. Nahodha alishauri ni vema viongozi wa serikali wakawa tayari kushauriana na viongozi wa dini badala ya watu kuanza kukosoana kwenye magazeti kwakuwa kwa kufanya hivyo watajenga mazingira mazuri kwa viongozi kuliongoza taifa letu kwa amani na utulivu.

Pia, Nahodha alisema kuwa kuwepo kwa viongozi wasio waadilifu katika jamii ni kielelezo cha matokeo ya viongozi wa dini kushindwa kutekeleza wajibu wa kusimamia na kufundisha maadili nchini jambo ambalo linalosababisha kupatikana kwa viongozi wasio waaminifu na wala rushwa.

"Jamii imekuwa ikifanya tathimini ya maadili mabovu kwa wanasiasa pekee yao wanasahau kuwa wanasiasa ni zao la dini zetu, wanasiasa wakiwa wala rushwa ni wazi kuwa viongozi wa dini wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kusimamia na kuelekeza jamii na waumini wao katika maadili mema," alisema Bw. Nahodha.

Pia, Bw. Nahodha alisema kuwa msongamano mkubwa wa mahabusu aliouona hivi karibuni katika magereza, baada ya kufanya ziara ni kielelezo cha tosha kuwa maadili katika jamii yetu yamemong'onyoka jambo ambalo analiona ni hatari kwa taifa letu ambalo linasifika kwa amani.

Hata hivyo, Bw. Nahodha alisema kuwa wizara yake ina mpango mkakati wa kumaliza kabisa matatizo ya wizi wa silaha, wa kalamu na wa kutumia nguvu unatoweka kabisa hapa nchini na kufanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.

"Najua kuna watu watasema kuwa Bw. Nahodha anaotandoto lakini kila kitu kilianza kwa kuwa ndoto, mimi kama Waziri wa Mambo ya Ndani nina ndoto hizo za kuhakikisha kuwa siku moja wizi wa kalamu na wa kutumia nguvu unatoweka kabisa nchini Tanzania," alisema Nahodha.

Pia, Bw. Nahodha amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na mashauriano na serikali katika mambo yote yanahusu maslahi ya taifa letu, na serikali iko tayari kuwasikiliza badala ya kuwa na kawaida ya kukosoana katika magazeti.

Vile vile, amewataka viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao katika kulijenga taifa kwani kazi ya viongozi wa dini pamoja na kuwaelekeza watu kumjua Mungu bali pia ni wajibu wa viongozi wa dini kuwaandaa watu kumudu maisha yao kwani ndipo wataweza kumtumikia vema Mungu.

Naye, Askofu Mkuu aliyesimikwa wa kanisa hilo Daniel Awatt akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, alisema viongozi wa dini wataendelea kushirikiana na serikali, vile vile amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuahidi kuunda Tume ya kushughulikia suala la Katiba mpya, pamoja na kumtaka kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba mpya unawashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini.

Awali, akizungumza katika ibada hiyo maalumu, Katibu Mkuu wa Kanisa la PAG, Askofu, Charles Kanika, alisema kuwa kanisa hilo mbali ya kujishughulisha na huduma za kiroho, pia limekuwa likifanya kazi katika huduma za jamii kwa kuungana na serikali katika wito wake wa kuelimisha jamii.
 
Naye, Askofu Mkuu aliyesimikwa wa kanisa hilo Daniel Awatt akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, alisema viongozi wa dini wataendelea kushirikiana na serikali, vile vile amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuahidi kuunda Tume ya kushughulikia suala la Katiba mpya, pamoja na kumtaka kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba mpya unawashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini.

Huyu askofu anajikanyaga bila ya kujijua...........TUme ya JK nidhuluma kwa raia wa nchi kwa sababu JK hana mamlaka ya kisheria ya kurekebisha Katiba na Tume hii haikundwa kwa nguvu ya kisheria na wala kutoa nafasi na fursa sawa ya watanzania katika kuiunda sasa utaitegemeaje ishirikishe raia wote wakati uundaji wake ni uvunjaji wa sheria?
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, (pichani amesema kuna dalili za kutoweka maadili miongoni mwa jamii jambo linalotishia kuwepo machafuko yanayoweza kusababisha kutoweka amani nchini.

Amani inajengwa kwa miundo mbinu ya kuimarisha misingi ya utu na kufuta dhuluma na udhalimu dhidi ya raia wanyonge.......................Kwa hiyo kuhofu tu bila ya kujua kiini cha amani yetu hakutusaidii kamwe.............................
 
Nahodha, in the absence of freedom, justice and equality,peace will always elude this country,which doesn't serve any one but the greedy corporates and corrupt politicians.
 
Tatizo lililopo ni wale waliopo madarakani kutokubaliana na swala zima la katiba mpya,kulikuwa hakuna maana ya kuunda tume ambayo hata raisi mwenyewe anayo mamlaka ya kukataa ama kukubali kile kitakachopendekezwa na tume,mimi nilidhani kama viongozi walioko madarakani wangekuwa si walevi wa madaraka swala la katiba lingefanya haraka iwezekanavyo pasipo kuwa na uundwaji wa tume ambayo mwisho wake ni utumiaji wa pesa nyingi pasipo na matunda tuyategemeayo

nadhani hakuna asiyejuwa kuwa katiba yetu ni ya wakati uliopita kila mtu ajuwa hilo,hata viongozi walioko madarakani cha kushangaza ni kuwa tunajifanya hatujui thats why tunaunda tume ili zitupe ukweli ambao tunaujuwa

Tanzania tuamke,kuna maamuzi hayaitaji kuingia Darasani kupekuwa vitabu kwani swala la katiba kila mtu anaelewa tunahitaji mabadiliko tena yale mabadiliko yalio ya kweli
Amani itatoweka kama hatutakubaliana na kile wengi wanachokihitaji

mapinduziiii daimaaaaaaa:ban:
 
sasa ka amani iko hatarini yeye anachukua hatua gani? Amwamishe ocd zuberi wa arusha na rpc wake vinginevyo kitawaka tu. Na pia watu wakinyimwa haki wataitaka kwa nguvu na ndio mwanzo wa vagi
 
Back
Top Bottom