Nahodha ahimiza siasa za Jino kwa Jino Mbeya!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha ahimiza siasa za Jino kwa Jino Mbeya!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Akili Kichwani, Feb 6, 2012.

 1. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [h=2]hebu soma hapo kwenye blue chini...................

  Nahodha bado auota urais Z`bar[/h]


  Asema kuvunjika koleo siyo mwisho wa uhunzi  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha


  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, bado anauota urais wa Zanzibar baada ya kudai kuwa mwaka juzi alipowania nafasi hiyo, kura hazikutosha kwa bahati mbaya na kwamba kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.

  Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara jijini hapa wakati wa maadhinisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika Uyole uwanja wa Kibonde Nyaso.

  Nahodha alieleza kuwa mwaka juzi alipowania nafasi hiyo, kura hazikutosha na kwa kuwa anamini kwamba CCM ndio chama bora chenye demokrasia ya kweli nchini, kwake anafananisha hatua ya kura kutotosha ni sawa na koleo kuvunjika kwani si mwisho wa uhunzi.

  Kauli hiyo ya Vuai ilionyesha kuwa kiongozi huyo bado anakusudia kurudi ulingoni kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar, ingawa hakubainisha kuwa lini ataitekeleza.

  “Nadhani nyote mnajua kuwa CCM ndiyo chama chenye demokrasia ya kweli nchini, kama mjuavyo mimi mwenyewe mwaka 2010 niliwania kiti cha urais wa Zanzibar, kwa bahati mbaya sana kura hazikutosha lakini kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi,” alisema Nahodha.

  Alisema kwa kuwa yeye hivi sasa ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), anaamini atashirikiana na wananchi kukiinua Chama na kuhakikisha kinapata ushindi.

  Nahodha aliwataka wanachama wa CCM Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi wazalendo na waadilifu katika uchaguzi wa ndani ya chama utakaofanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na upinzani kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na hatimaye kuyakomboa majimbo mawili yaliyochukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  “Najua kuwa yule Mbunge wa Mbeya Mjini maarufu kwa jina la Sugu, (Joseph Mbilinyi) atajitokeza tena kwenye uchaguzi mkuu ujao, hakikisheni mnamuwekea mtu anayelingana naye,” alisema.

  Jimbo lingine ambalo lipo chini ya Chadema ni Mbozi Magharibi ambalo Mbunge wake ni David Silinde.

  Nahodha aliwataka viongozi, wanachama na wafuasi wa CCM mkoani Mbeya, kujibu mapigo ya kauli za wapinzani badala ya kukaa kimya hata pale wanapotupiwa matusi ya nguoni kwani kwa kufanya hivyo Chama kinazidi kuchafuliwa na kupunguza mvuto kwa wananchi.

  “Ni lazima sasa mjibu mapigo kwa matusi ya wapinzani, wakimtukana mwenyekiti wako wa chama na wewe mtukane mwenyekiti wa chama chake, akimtukana baba yako na wewe mtukane mama yake, akimtukana mkeo na wewe lazima ujibu mapigo,” alisema Nahodha.

  CHANZO: NIPASHE@ Home
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kweli CCM vichaa wanadhani sisi wananchi mandondocha hatujifahamu safari ijayo hata kura moja haitaibiwa ajiulize juzi mbeya vijijini wananchi waliwafanyaje wezi wa Kura aache ujinga huyo bishoroo wa Zenj
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Naam! Nuff said...
   
 4. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  wamekata tamaa busara wameficha makalioni
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Na za CDM naona zimefichwa chumvini
   
 6. c

  chilubi JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 3,038
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Froida hata kama nahodha ametokea zenji kuwa na heshima na zenji kama zenji, tusi umpe yeye km yeye na sio kuongeza "wazenji",,,, unaonekana una bifu na wazenji eee?!!! Huyo ameishi bongo hivo amechukua sifa za kibongo, zanzibari huwa hatujibu matusi bali tunajibu kwa hoja au tubakaa kimya kuonesha kama tuna busara zaidi na wavumilivu, sasa apo amekufanya wewe ndondocha kaona ni sifa yenu watu km ww, ukitukanwa na ww unatukana :D
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ile kesi ya mke wa Katibu Mkuu wa Chadema kuzini nje ya ndoa imeishia wapi?
   
 8. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Siasa za huyu bwana tangia ameingia kwenye fani ya siasa hazina ushawishi wala mvuto.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Well, hana historia ndefu katika siasa, hata hivyo alichosema hapo juu si cha kukibeza! Chadema wana siasa gani zaidi ya kutukana?
   
 10. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  naona unatekeleza alichosema mh. Mzenji
   
 11. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  halafu mtu huyo huyo ni waziri wa wizara muhimu ya nchi yetu, kazi kweli kweli
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  CCM bwana wanavaa makoti makubwa na kuchana nywele kumbe ni watupu.Huyu mzanzibari anaongea haya huko Mbeya anadhani ni CUF ? Haya mwache aone mwisho wake atavuna nini .Pole zao CCM badala aongelee umasikini mkubwa wa Watanzania na migomo anaongelea kuongeza matatizo ?
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Zaidi ni mwanasiasa! Hivyo usishangae sana
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ila tamu kuila...
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Umaskini? Serious?
   
 16. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ikiwa raia anahatarisha amani ya nchi hupigwa mabomu, hukamatwa na hata kushitakiwa hasa akiwa ni mwanachama wa chama kingine cha siasa tofauti na ccm. Je, waziri mwenye dhamana ya usalama wa raia afanywe nini? Naomba mwongozo wa umma wa watanzania.
   
 17. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Wewe tumia muda kupumzika, thread nzima unajibu wewe tu, usilazimishe umaarufu kirahisirahisi namna hiyo.
   
 18. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Huyu jamaa zenji walikwisha malizana nae, sijui watanganyika mnamfugia nini? wizara nyeti kama hii kupewa mzembe, angalia cv yake utalia usingizini, kasoma lugha thats it.
   
Loading...