Nahitaji walimu wa kujitolea: Nataka kufungua NGO inayohusika na maswala ya elimu tufanye kazi

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
269
1,000
Kama kichwa cha habari kinavyojielezea nipo njiani kufungua NGO yangu ambayo itakuwa ina deal na maswala ya ELIMU YA TANZANIA

Kazi tutakazokuwa tunafanya ni kama ifuatavyo:

1. Kufundisha mashuleni kwa mfumo wa club

2. Kuandaa matamasha mbali mbali ya kielimu mashuleni

3. Kutoa mafunzo kwa walimu

4. Kupima IQ test completion kwa wanafunzi

5. Kutoa consultant kwa maswala ya kielimu kwa wamiliki wa shule na wakuuu wa shuleni

Karibuni sana hata kama wewe sio mwalimu; karibu tupige kazi kidogo kinachopatikana tutakuwa tunalipana
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,035
2,000
Wazo zuri mkuu. Ukipata watu wenye nia ya dhati mtafika mbali. Kila kheri boss
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,782
2,000
Unafungua NGO lakini unataka watu wa kujitolea?

Maelezo yako hayashawishi,wapo watu wengi wasio na ajira ni kweli lakini waambie baada ya kujitolea mtaishia nao wapi na watapata nini, we unasema tu kujitolea ndo kitu gani.
 
Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
269
1,000
Unafungua NGO lakini unataka watu wa kujitolea?

Maelezo yako hayashawishi,wapo watu wengi wasio na ajira ni kweli lakini waambie baada ya kujitolea mtaishia nao wapi na watapata nini,we unasema tu kujitolea ndo kitu gani.
Kwa kifupi tuu sina uwezo wa kuwalipa walimu mshaharaa ila uwezo wangu tutakuwa tunalipana posho baada ya kupiga kazi hela inayopatikana tunagawana.

Kwa kifupi tu ninahitaji watu wa kufanya nao kazi.
 
HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,193
2,000
Ungefungua kwanza hiyo kitu ndio uje kutafuta watu.

Halafu hiyo kitu sio rahis kama ulivyoelezea hayo majukumu ya NGO yako.
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
431
500
Kama huna hela na unataka kufungua NGO hiyo NGO haitadumu. Ushauri ni kuwa changanya objectives nyingi kama 6 kwenye katiba yako udeal na mambo tofauti tofauti kama mazingira, magonjwa/ afya, uongozi bora, sheria na haki za binadamu n.k.

Hayo uliyoeleza hapo iwe tu part ya project. Na kama ndiyo project uliyoanza nayo hiyo basi jua umeanza na chaguo sio sahihi kwa NGO inayoanza utashindwa kwenye documentation wakati wa ku submit taarifa ya mwaka wizarani
 
Asante kwa taarifa na ushauli wako nitaufanyia kazi broo
 
Matts

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
247
1,000
huko kwingine kote umemshauri vizuri,shida ipo hapo kwenye haki za binadamu,akisaidia kuelimisha kuhusiana na haki za binadamu kwa nchi hii atajikuta sio mtanzania na hiyo NGO itafungwa ndani ya muda mfupi sana
Kama huna hela na unataka kufungua NGO hiyo NGO haitadumu. Ushauri ni kuwa changanya objectives nyingi kama 6 kwenye katiba yako udeal na mambo tofauti tofauti kama mazingira, magonjwa/ afya, uongozi bora, sheria na haki za binadamu n.k.

Hayo uliyoeleza hapo iwe tu part ya project. Na kama ndiyo project uliyoanza nayo hiyo basi jua umeanza na chaguo sio sahihi kwa NGO inayoanza utashindwa kwenye documentation wakati wa ku submit taarifa ya mwaka wizarani
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,249
2,000
Kwa kifupi tuu sina uwezo wa kuwalipa walimu mshaharaa ila uwezo wangu tutakuwa tunalipana posho baada ya kupiga kazi hela inayopatikana tunagawana.

Kwa kifupi tu ninahitaji watu wa kufanya nao kazi.
Utawalipa posho kutoka chanzo gani au ndio ushapata sponsors then unataka kuwafuja watoto wa wenzako?
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
431
500
huko kwingine kote umemshauri vizuri,shida ipo hapo kwenye haki za binadamu,akisaidia kuelimisha kuhusiana na haki za binadamu kwa nchi hii atajikuta sio mtanzania na hiyo NGO itafungwa ndani ya muda mfupi sana
Hapana unafuata misingi ya sheria inavyotaka. Hapa inamaana kutoa msaada wa kisheria through reconciliation and counselling. Kuna baadhi ya migogoro inaweza kutatuliwa kabla ya kwenda mahakamani. Na utatuzi huu unaweza kufanywa na mtu wa mwenye elimu ya kawaida tu kama paralegal . Kuna mashirika kama Winlak, Tamwa, LHRC, Morogoro Paralegal, Temeke Paralegal hutoa huduma za msaada wa kisheria na haki za binadamu. Uendeshaji wa NGO ni shughuli na hizo ndizo moja ya shughuli ambazo unaweza kuzitoa bila hata shirika kuwa na fedha. Kama wanavyofanya baraza la kata au baraza la ardhi la kijiji.
Njia hii pia kuna taasisi hutoa ruzuku kwa kukaribisha proposal kama Legal Service Facilities, The Foundation for Civil society, Tanzania Women Fund, kwenye mazingira kama Tanzania Forest Fund n.k. Hayo ni baadhi tu ya mashirika ya ndani ya Tanzania hutoa ruzuku kisha akibahatika na kupata uzoefu anaanza kutuma proposal kwa watoa ruzuku kama USAID, n.k
Pia kwenye haki za binadamu kuna miradi hutoaga ruzuku kutokana na nyakati mfano kuelimisha kuhusu haki ya upigaji kura na utawala bora kwa jamii ikifika wakati wa karibu na uchaguzi.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,752
2,000
Usiishie Dar tu njoo hadi huku Rungwe, kata ya Mwakaleli kijiji cha Isange.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom