Nahitaji vijana ishirini (20) wenye mawazo ya biashara

tax compliant

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
1,211
1,195
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu, nahitaji vijana ishirini (20) wenye mawazo ya biashara na wanakosa pa kuanzia kwa sababu tu hawana mitaji, Kila mmoja awe na sifa zifuatazo;
1. Awe na wazo la biashara linalotekelezeka (implementable) litakalohitaji mtaji usiozidi shilingi za kitanzania milioni moja (Tshs 1,000,000).
2. Awe na kitambulisho cha taifa (national identity card).
3. Awe anatoka mkoa wowote wa tanzania bara.
4. Umri usiopungua miaka 23 na usiozidi miaka 45.
5. Awe na wadhamini wawili ambao watakua tayari kusaini bond ya shilingi 500,000 kila mmoja ili kama utakimbia basi wao wawajibike.
6. Awe mchapakazi na mtu mwaminifu anayeweza kujisimamia.
7. Wazo la biashara litakaloletwa kwa majadiliano liwe lile linaloweza kuzalisha si chini ya shilingi za kitanzania elfu ishirini (20,000) kwa siku.
8. Awe tayari kusaini mkataba utakaomfanya kuwa mbia (partner) na kumpa haki ya kuwa na umiliki wa asilimia hamsini (50%) ya rasilimali zote (assets) zitakazopatikana baada ya kuanza kuzalisha (mtaji wa 1,000,000 utakuwa si miongoni mwa rasilimali hizo) na atakuwa na mgao wa asilimia hamsini ya faida itakayozalishwa kutoka katika biashara. Yaani kama utazalisha 20,000 kwa siku basi utakupata mgao wa 10,000 be it Tshs or $.


NB: 1. Mawazo yote yatachakatwa (yafanane au la) ila yakidhi vigezo.
2. Mawasiliano yote yanaanzia PM.
3. Hakuna gharama zozote za awali (kutoka kwako) kabla ya kuanza kazi.
4. Mwisho wa kupokea mawazo ni 20.03.2019
5. Watakaokuja kwanza watapewa kipaumbele.
 
Back
Top Bottom