Nahitaji ushauri wenu kwa biashara ya usafi /kukusanya taka

angel2694

Member
Feb 27, 2018
11
45
Habari za wakati huu ndugu zangu, Mimi ni binti miaka 25 muhitimu wa chuo ngazi ya diploma ila sijaajiriwa na nimemaliza chuo tokea mwaka juzi.

Nakuja mbele zenu nikiomba ushauri juu ya wazo la kufanya usafi yaani natafuta watu nawaajiri wanakuwa wanakusanya uchafu katika kila kaya ambapo kwa wiki tunapita Mara mbili kwenye Nyumba za watu nachukua uchafu halafu wao wanajamii wananilipa elfu 3 au kiasi chochote tutakachokuwa tumepanga kulipana na mie nawalipa niliowaajiri nataka kuanza na mtaa mmoja kwanza ....

Vile vile usafi wa maofisini na majumbani Kama kufua nguo za watu nk

Kwa yeyote anayefanya kazi kama hii naomba pia mwongozo na jinsi ulivyoanza hadi hapo ulipo sasa

Sasa sijui pa kuanzia nilikuwa naomba ushauri wenu cha kufanya na pa kuanzia ili zoezi langu likamilike na mie niweze kujiajiri.

Napatikana Mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
elitee

JF-Expert Member
May 15, 2017
329
500
wazo zuri ila la kyk Kaya changamoyo ni nyingi kuliko faida,
I assume unatumia gari kukusanya hizo taka, shida itakuja ktk kulipa wengi ni wasumbufu mnoooo ktk ulipaji hvyo itakukwamisha ktk kurun..
Bora usafi wa maofisini ila ktk Kaya mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
teamsolution

Member
Jun 19, 2017
64
125
Wazo nzuri na la manufaa sana,
Chakufanya
Sajili kampuni maana naona wazo lako linaenda kuwa kamouni kubwa sana sana muda sio mrefu

Sambamba na huduma hiyo mkuu ndhani huduma zetu hapa chini zaenda sambamba kwa manufaa ya watanzania, hasa kwakl. Wasiliana nasi.

Ushauri ni bure

HUENDA WAHITAJI...
* Kusajili kampuni
* Hesabu za Kodi, Hesabu za Kampuni,
*Kuandaa Memorandum....
* Kuandika Business Plan, Business Profile,
* Kuandaa Tender documents, CRB
*Kutengeneza LOGO, Business Cards, Brochures, Banners
* Printing - All types of Books
*Digital Printing: T-SHIRTS, CAPS, BAGS, PLATES, CUPS, etc.
TUPIGIE/ MESEJI - 0684 205039: WATSUP TU 0652 411402
BEI ZETU HAZINA USHINDANI, MIKOANI PIA TUNAHUDUMIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
buffalo44

JF-Expert Member
May 8, 2016
1,649
2,000
Mkuu mimi nilikuwa na wazo hilo Waste management yaani nilichimba vitubu na kila material niliandika business plan. Kilichonikwamisha ni mtaji na kitambulisho cha taifa kusajilia kampuni. Nitafurahi ukionedha nia naweza kukushauri maana nimesoma sana hadi naelewa kwa upana waste management.
 
Aug 6, 2013
61
225
Kwa kukusanya taka majumbani.

Upo sehemu gani ? kwa hapa dar gali la tani 18 ni laki tatu kwa trip. na wanaenda kumwaga wenyewe dampo. gharama za kumwaga dampo haizidi elfu 20. dereva wa hilo gari posho ni elfu 10 wabebaji wa mtaani mara nyingi huwa wanalipwa elfu 10 kwa kila mfanyakazi kwa siku.

Km una kampuni tayari. changamoto kubwa utakayokutana nayo ni kwenye kukusanya pesa jitahidi sana mtu akulipe pale unapochukua taka. ukisema watu walipe kila mwezi au kwa week hii kazi utaiona ngumu.

vifaa vya muhimu unavyohitaji ukiwa unaanza.
groves kwaajili ya wafanyakazi,
tolori kwa watu wa mabondeni ambapo gari haliwezi kupita. toroli ukikodi halizidi elfu 3000 kwa siku.
kipataza sauti kwaajili ya kutangazia siku unapopita.
sale za kuvaa wafanyakazi.
kuna vimashine tra wanatoa utahitaji kuwa nacho kwaajili ya kutoa risiti.

Tenda kama hizi za usafi huwa zinatolewa serikali za mitaa. na waaombe wakupe mgambo uwe unapita naye pale unapokuwa mnakusanya taka.
 
DIVIDEND

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
1,819
2,000
Bila kupata mgambo wa kukusaidia kuwasweka ndani watu ambao awalipi ushuru jiandae kupata hasara kubwa sana
 
Hammy Js

JF-Expert Member
Sep 20, 2017
3,079
2,000
Habari za wakati huu ndugu zangu, Mimi ni binti miaka 25 muhitimu wa chuo ngazi ya diploma ila sijaajiriwa na nimemaliza chuo tokea mwaka juzi.

Nakuja mbele zenu nikiomba ushauri juu ya wazo la kufanya usafi yaani natafuta watu nawaajiri wanakuwa wanakusanya uchafu katika kila kaya ambapo kwa wiki tunapita Mara mbili kwenye Nyumba za watu nachukua uchafu halafu wao wanajamii wananilipa elfu 3 au kiasi chochote tutakachokuwa tumepanga kulipana na mie nawalipa niliowaajiri nataka kuanza na mtaa mmoja kwanza ....

Vile vile usafi wa maofisini na majumbani Kama kufua nguo za watu nk

Kwa yeyote anayefanya kazi kama hii naomba pia mwongozo na jinsi ulivyoanza hadi hapo ulipo sasa

Sasa sijui pa kuanzia nilikuwa naomba ushauri wenu cha kufanya na pa kuanzia ili zoezi langu likamilike na mie niweze kujiajiri.

Napatikana Mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa nadhani ushuru umesahau kuuhesabia, hii tenda lazima uiombe ktk halmashauri(sina hakika kama ni halmashauri) na kila unayemtoza pesa lazima umpatie risiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,328
2,000
Mtoa mada ukifabikiwa kuestablish kijana wa kazi nipo hapa,let me pray for you!
 
Danp36

JF-Expert Member
Jul 31, 2010
1,840
1,500
Hapa nadhani ushuru umesahau kuuhesabia, hii tenda lazima uiombe ktk halmashauri(sina hakika kama ni halmashauri) na kila unayemtoza pesa lazima umpatie risiti

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa sasa no halmashauri Kwa kata nyingi, kuna mitaa midogo ataiweza ,ila Kwa kata kidogo almashauri inahisika ,na uwe na magari na vitendea kazi vya kutosha .kupata tends pia uzoefu nawe na wataalamu wa afya bye kampuni yako.

Kama una nia tembelea kata na halmashauri
yako utapewa mwongozo ....baada ya hapo utupe mrejesho . naweza angalia contact na watu wanaofanya kazi hizo
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
4,120
2,000
Hapa nadhani ushuru umesahau kuuhesabia, hii tenda lazima uiombe ktk halmashauri(sina hakika kama ni halmashauri) na kila unayemtoza pesa lazima umpatie risiti

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii biashara ili aifanikishe vzr anatakiwa acheze na viongozi wa serikali za mtaa na kata halaf hao ndio wapeleke propaganda kwa raia wao.
Na kumbuka ktk hao raia Kuna wabishi ambao watapinga na Kuna watakaokubali na kuunga mkono.
Watakaopinga ww achana nao endelea na watakaounga mkono uwe unawabebea taka mara 1 kwa wiki Kisha wanachangia pesa mwisho wa mwezi.
Usitumie nguvu kubwa kuwalazimisha wananchi huduma bali iwe ni huduma ya hiari vinginevyo watapeleka malalamiko kwa Mh. Makonda iwe bonge la ishu.
 
Oct 26, 2018
78
125
Mkuu mimi nilikuwa na wazo hilo Waste management yaani nilichimba vitubu na kila material niliandika business plan. Kilichonikwamisha ni mtaji na kitambulisho cha taifa kusajilia kampuni. Nitafurahi ukionedha nia naweza kukushauri maana nimesoma sana hadi naelewa kwa upana waste management.
Mambo vipi kaka?
Nmependezwa na idea yako na uchimbuaji wako
Naomba tuwasiliane basi, 0745050340
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom