Nahitaji ushauri wa tatizo hili!!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Habari zenu wana-Jf Doctor,.

Mimi ninasumbuliwa na uchovu wa kila wakati, iwe asubuhi, mchana au jioni mwili wote unakuwa na maumivu yasiyoisha!!


Nimeshafanya vipimo vya x-ray mara kadhaa lakini hamna tatizo lolote lililo onekana,.

Kuna wakati kifua kinabana sana na pumzi inakua nzito sana wakati wa kuvuta hewa ndani,.

Nimeshatumia dawa nyingi ikiwemo dawa inayoitwa KoAct ambayo nimemaliza dozi hivi karibuni bila kuona mabadiliko yoyote,..


NB: Nilikuwa nikifanya mazoezi ikiwemo kuinua vyuma kwa muda fulani kisha nikaacha ghafla na kuanzia hapo nikaanza kupata matatizo niliyoyaeleza hapo awali,.


Je nitakaporejea kufanya mazoezi naweza kuondokana na tatizo linalonikabili?


Naombeni ushauri tafadhali,.
 
Habari zenu wana-Jf Doctor,.

Mimi ninasumbuliwa na uchovu wa kila wakati, iwe asubuhi, mchana au jioni mwili wote unakuwa na maumivu yasiyoisha!!


Nimeshafanya vipimo vya x-ray mara kadhaa lakini hamna tatizo lolote lililo onekana,.

Kuna wakati kifua kinabana sana na pumzi inakua nzito sana wakati wa kuvuta hewa ndani,.

Nimeshatumia dawa nyingi ikiwemo dawa inayoitwa KoAct ambayo nimemaliza dozi hivi karibuni bila kuona mabadiliko yoyote,..


NB: Nilikuwa nikifanya mazoezi ikiwemo kuinua vyuma kwa muda fulani kisha nikaacha ghafla na kuanzia hapo nikaanza kupata matatizo niliyoyaeleza hapo awali,.


Je nitakaporejea kufanya mazoezi naweza kuondokana na tatizo linalonikabili?


Naombeni ushauri tafadhali,.





pole sana mr ,kwa tatizo mungu atasaidia utapona
kwa hali ya maelezo yako its mean kwamba una symptoms(dalili) kama chest tightness, shortness of breath and fatigure
umefanya investigation only x-ray
umetumia dawa ya kurekebisha mifupa kwa maana ya kukomaza mifupa koact
hiyo hali inaweza kuwa imesababishwa na mazoezi au kuacha mazoezi uliyokuwa unafanya
magonjwa yafuatayo yanaambatana na hali yako
1)pneumothorax(collapse of lungs) hutokea pale hewa ya mapafu inapoingia kwenye mianya au sehemu inayozunguka mapafu na kuwa kubwa kwakuwa moyo uko karibu na mapufu ,hali ya pleural kujaa hewa inaubana moyo .kwahiyo moyo unapata kazi kusukuma damu kupeleka kwenya misuli yaani musle tissure na kufanya oxygen ifike kidogo na kusababisha utengenezaji wa ATP (NGUVU) Kuwa mdogo na kusabisha hali ya kujisika mchovu na huna nguvu, .hali hii huwatokea sana wafanya mazoezi yanayopelekea damage ya kifua na wacheza mpira
2)ISCHEMIC CARDIOMYOPATH inayoweza kuwa imesababishwa na mishipa ya arteri kuziba kutokana na mafuta yaani cholesterol kwa sababu ya kuacha mazoezi umeruhusu accumulation ya cholestol kwenye arteri ( arteriosclerosis)
MAONI

  1. rudi hospitali
  2. fanya CT Scan na ECG ikiwezekana na MRI
  3. fanya BLOOD TEST kwa ajili ya LIPID PROFILE yaani cholesterol na triglycerides
  4. coronary angiograph kwa ajili ya kuangalia kama arteri zimeziba
  5. pungunza chakula chenye mafuta mengi yanayotokana na product za wanyama
  6. PIMA pressure mara kwa mara
  7. fanya aerobic exercise siyo heavy weight lift
  8. kula vyakula kama matango ili kupunguza risk ya pressure
  9. kama wewe mnene punguza uzito
  10. usivute sigara wala kunywa tungi(pombe)
  11. punguza chumvi kwenye chakula
  12. kwa upande wa dawa mpaka utakapokamilisha investigation yaani vipimo ndipo nikushauli dawa zipi ziko ok kulingana na standard treatment ya nchi
 
shukrani mkuu Ndokeji, nilishafanya vipimo vya damu kubwa (Full Blood Check) na vipimo vikaonyesha sikuwa na tatizo lolote ila Red Blood Cells ( RBC's) zilikuwa zimezidi kiwango cha kawaida na dokta akaniambia damu yangu ni nzito akaniandikia na dawa tajwa hapo juu KoAct niitumie!! Pia nimeshapima pneumonia mara tatu lakini tatizo hilo halikuwepo mkuu!!


NB: Mara nifanyapo mazoezi kidogo napata ahueni lakini kwa majukumu niliyonayo muda wa kufanya mazoezi kwangu unakuwa finyu sana mkuu,..



Naomba ushauri wako,.
 
Last edited by a moderator:
Yawezekana kabisa kuna organi haifanyi kazi ipasavyo mwilini nakushauri urudi kwa dr akufanyie checkup ya mwili mzima au uende kwa consultant wa afya hakikisha ni medical personal by professional maaana madaktari wa mitaani ni wengi uone atakushauri nini au waweza wasiliana na huyu mmojawapo 0712294734 atakuwezesha sana mkuu
nawakilisha
 
Tatizo lako ni Kama langu!! Nimefanya mazoezi kwa 14yrs sasa ratiba yangu sasa hainiruhusu, ninapata maumivu na kuchoka! Njia ni kuendelea tu jaribu kufanya mazoezi walau Mara mbili kwa wiki au push up nyingi baada ya kuamka!!
 
Back
Top Bottom