Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Mohammed Shossi,
Dah! umenifumbua sana nitaendelea kupata ujanja na mawazo kutoka kwako. Nadhani pia ni vizuri ukaanza kilimo cha haya mapapai local breed na kutafuta masoko locally halafu ndipo uanze kujaribu kuingia kwenye export quality.
 
Kuna mbegu nyingi zilizofanyiwa utafiti duniani kama F1 Hybrid Taiwan Princess mbegu hii sio genetic kwahiyo inaweza kulimwa nchini na ni nzuri kwasababu shelf time yake ni kubwa kulinganisha na papai zetu za kienyeji na zinaweza kuuuzika nje ya nchi (Ideal for export)


Hizi mbegu za F1 Hybrid Taiwan Princess zinapatikana wapi mkuu? vp zinakubali katika mazingira ya pwani? Dar?
 
Mohammed Shossi,
Nimekupata uzuri mkuu, ndiyo maana nilitilia shaka ukubwa wa papai lenyewe kufaa kibiashara maana biashara ili iwe biashara, ina mahitaji maalumu kama ulivyofafanua hapo juu.

Thanks.
 
Hizi mbegu za F1 Hybrid Taiwan Princess zinapatikana wapi mkuu? vp zinakubali katika mazingira ya pwani? Dar?

Hizi mbegu zinapatikana India na Philippines inabidi uombe kibali kuziingiza. Papai ni tropical fruit na maeneo uliyoyasema yanatimiza vigezo vya kulima zao tajwa.
 
Mkuu kilimo kinalipa sana ila kinahitaji uvumilivu, mimi naweka mambo sawa nikimaliza najikita kwenye kilomo maana huko watu wa kodi hawasumbui na mazao (unprocessed) hayana kodi.

Kweli mkuu TRA hawakuvamii kabisa
 
Hivi hicho kilimo kinalipa kweli?

Kilimo cha mapapai ni kizuri sana, make utomvu wake pekee huwa unatafutwa sana, na kuna watu wanalima kwa sababu ya utomvu, ingawa hata tunda lake ni zuri sana na kwa wanao fuga kuku majani ya mipapai ni mazuri sana kwa kuku make ni dawa, na kuna artical nilisoma kwa west aftica wanatumia mbegu za papai kutibu Newcastle ua mdondo. Nikiipata nitaiweka hapa
 
Kilimo cha mapapai ni kizuri sana, make utomvu wake pekee huwa unatafutwa sana, na kuna watu wanalima kwa sababu ya utomvu, ingawa hata tunda lake ni zuri sana na kwa wanao fuga kuku majani ya mipapai ni mazuri sana kwa kuku make ni dawa, na kuna artical nilisoma kwa west aftica wanatumia mbegu za papai kutibu Newcastle ua mdondo. Nikiipata nitaiweka hapa

Mkuu utomvu unatumiwa kwa nini?
 
Mkuu utomvu unatumiwa kwa nini?
]

Mapapai mabichi hutoa utomvu ambao una kimeng'enyo (enzyme) kiitwacho Papain. Papain ni maarufu kwa kulainisha nyama (meat tenderizer). Papain huvunjavunja nyuzinyuzi zinazoshikamanisha misuli ya nyama na kuifanya nyama ambayo ni ngumu ikipikwa kuwa laini kabisa.

Ndiyo maana wakati mwingine watu hupika nyama kwa kuchanganya na vipande vya papai bichi au utomvu wake. Papain pia inatumika viwandani kutengeneza vitu mbali mbali na hutumika mahospitalini kwa tiba ya magonjwa mengi kwa hiyo papain inamatumizi mengi sana. Kuna steji maalumu ambapo matunda ya papai hukwaruzwa na utomvu wake unakusanywa, hukaushwa na kuuzwa.

Kwa nchi zenye watu serious zao la Mapapai ni zao maarufu! Biashara ya papain inaweza kuwa na kipato kuliko tunda lenyewe!
 
ntaanza kuifanyia kazi home niijaribu then ikiwork intaifanya kibiashara zaidi, thanks for info.
Poowaa!! Inabidi ufanye kama ka utafiti hivi! Unaweka vipimo tofauti tofauti hadi kieleweke! Inawezekana kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom