Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

mkuu nakushauri uongeze thamani hapo ndio penye kula penyewe. mawazo ya kiwanda kiwanda. tengeneza jam ya papai. tengeneza ambayo haina sukari ili kukwepa kuongeza gharama. otesha aina ya papai ambazo ni tamu na zina sukari asilia. ukiingia sokoni tumia hiyo ama mbinu ya kibishara kuwa jamu yako huweki sukari. pia unaweza kuwa unaichanganya na matunda ya msimu maana huko uliko ndio kwenyewe. watu wanapenda mixed fruit jam ziaidi ya yenye tunda moja. unaweza kujifunza ujasiriamali huo sido au veta. ukajua namna ya kufungusha. kuweka label. na pia kupata sehemu ya kufanyia kazi ambayo imethibitishwa na tfda na tbs. tupo pamoja.
 
Soko la papai wakati hata MCHE hujapanda!
Nashauri upande miche unayofikir, ikifika umri wa miezi minne, ndipo uanze kusaka soko
Kuna nyuzi kadhaa humu ambazo unaweza kuzitumia kama kiongozi chako Kwa shughuli unayetaka kufanya.
Ni sawa kutafiti kuhusu soko kabla ya kuanza kilimo chochote.
 
Soko la papai wakati hata MCHE hujapanda!
Nashauri upande miche unayofikir, ikifika umri wa miezi minne, ndipo uanze kusaka soko
Kuna nyuzi kadhaa humu ambazo unaweza kuzitumia kama kiongozi chako Kwa shughuli unayetaka kufanya.

Hatua alizoanza nazo ni sahihi kabisa huwezi kuanza kulima kitu bila kuuliza soko likoje na utamuuzia nani nawengi wanaanguka kwenye kilimo kwajiri hiyo.
 
Habari wanajukwaa! Mimi ni kijana nlieamua kujihusisha na kilimo.

Nakusudia kulima papai mapema mwakani na nimedhamiria kuwa na mipapai takriban mia saba.

katika hiyo mia saba, mia tatu nakusudia kuifanyia kilimo cha umwagiliaji na ilobaki kilimo cha kutegemea mvua.

ENEO LA KILIMO, Nakusudia kulima kijiji cha SEGERA wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

HITAJIO KUU: Nahitaji kujua wapi ntapata Soko la uhakika na aina gani ya papai inapendwa Sokoni.

Karibuni wadau.
michango yenu katika hili ni muhimu sana kwa kijana mimi nlie hamasika na kilimo

Hongera ndugu kwa wazo hilo karibu kwenye kilimo. Na umeanza vizuri kutaka kujua soko kabla ya kuingia kulima. Soko la papai lipo kubwa ni ubora wa papai zako ubora utatokana 'a huduma yako, na aina papai mapapai ya jamii nyingi ila mimi nitakuelekeza kwa muonekano tu mapapai yanayopendwa sokoni nilaye yenye umbo refu kama yai sio yae ya duara japo hata hayo unaweza kuuza pia.

Pili ningekushauri wewe mwenyewe pia kwenda masokoni kuonana na wateja kujua wanataka nini na kwasababu gani?.

Tatu ukitoka huko utajua sasa soko lako litakuwa wapi hapo utaangalia mradi wako wa kilimo ufanyie wapi kutegemea na ukaribu wa soko.kadiri unavyokuwa mbali na soko ndio faida inapungua.

70X70mt inaingia mipapai 1000 mpaka 1200 hivyo kwa hiyo 700 sio mbaya na kawaida kabisa kwakuwa utakapokuwa unalima utapata changamoto zake.
 
Hatua alizoanza nazo ni sahihi kabisa huwezi kuanza kulima kitu bila kuuliza soko likoje na utamuuzia nani nawengi wanaanguka kwenye kilimo kwajiri hiyo.
Mkuu nimesema hivyo kwa uzoefu, sio utafiti.
Kumbuka huyu ndugu ndo Kwanza anawazo, hata shimo hajachimba ukiacha mambo mengine yenye changamoto zake.
Angalia jukwaa hili uzi unaohusu, pata ushauri juu ya kilimo cha papai
 
Habari wanajukwaa! Mimi ni kijana nlieamua kujihusisha na kilimo.

Nakusudia kulima papai mapema mwakani na nimedhamiria kuwa na mipapai takriban mia saba.

katika hiyo mia saba, mia tatu nakusudia kuifanyia kilimo cha umwagiliaji na ilobaki kilimo cha kutegemea mvua.

ENEO LA KILIMO, Nakusudia kulima kijiji cha SEGERA wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

HITAJIO KUU: Nahitaji kujua wapi ntapata Soko la uhakika na aina gani ya papai inapendwa Sokoni.

Karibuni wadau.
michango yenu katika hili ni muhimu sana kwa kijana mimi nlie hamasika na kilimo
Mapapai yale makubwa, marefu, yenye rangi ya carrrot iliyokolea na mbegu nyeusi, na yana sukari na maji mengi. Tafuta hiyo mbegu kwanza then uendelee na kilimo.
 
mkuu nakushauri uongeze thamani hapo ndio penye kula penyewe. mawazo ya kiwanda kiwanda. tengeneza jam ya papai. tengeneza ambayo haina sukari ili kukwepa kuongeza gharama. otesha aina ya papai ambazo ni tamu na zina sukari asilia. ukiingia sokoni tumia hiyo ama mbinu ya kibishara kuwa jamu yako huweki sukari. pia unaweza kuwa unaichanganya na matunda ya msimu maana huko uliko ndio kwenyewe. watu wanapenda mixed fruit jam ziaidi ya yenye tunda moja. unaweza kujifunza ujasiriamali huo sido au veta. ukajua namna ya kufungusha. kuweka label. na pia kupata sehemu ya kufanyia kazi ambayo imethibitishwa na tfda na tbs. tupo pamoja.
Hizi ni ndoto sasa, nadhani akizalisha then haya ndio yaanzaje
 
cheki na tafuta mawasiliano na madalali wa matunda soko la matunda ilala au kariakoo pia soko la matunda mwananyamala ..... natafuta mbegu fupi ya papai

Kama itakua rahisi kwako pale SUA morogoro kuna mbegu nzuri sana fupi za papai unaweza kujaribu pale
 
Soko la papai wakati hata MCHE hujapanda!
Nashauri upande miche unayofikir, ikifika umri wa miezi minne, ndipo uanze kusaka soko
Kuna nyuzi kadhaa humu ambazo unaweza kuzitumia kama kiongozi chako Kwa shughuli unayetaka kufanya.

So unamshauri aingie gharama kwanza then ndo afanye utafiti kujua kama uwekezaji wake utamlipa sio? Its amazing!!
 
Mkuu nimesema hivyo kwa uzoefu, sio utafiti.
Kumbuka huyu ndugu ndo Kwanza anawazo, hata shimo hajachimba ukiacha mambo mengine yenye changamoto zake.
Angalia jukwaa hili uzi unaohusu, pata ushauri juu ya kilimo cha papai

Kiongozi yupo sahihi kabisa kulifahamu soko kwanza kabla ya kuanza kuzalisha, ni hatua muhimu sana kabla ya kuanzisha biashara yeyote (kwa maana kilimo nacho ni biashara).

Uwekezaji hautaki mazoea
 
Habari za muda wanajamvi! kutokana na dhamira yangu ya kulima papai naomba kueleweshwa yafuatayo:

.Ekari moja kuingia mipapai 1000-1200 ni kwa umbali gani wa mche hadi mche na mraba hadi mraba?

.Kutokana na michango nlopata humu jamvini na kwingineko, imenidhihirikia kuwa papai lipendwalo sokoni ni lile refu lenye umbo la yai- swali, je dukani naweza pata mbegu ya mipapai chotara ya mapapai marefu matupu?
 
Mbegu upate kwa supplier wa kuaminika vinginevyo utachakachuliwa. Halafu nawaza hivi haiwezekan kununua sokoni hayo mapapai na kuzitoa zile mbegu
 
Habari za muda wanajamvi! kutokana na dhamira yangu ya kulima papai naomba kueleweshwa yafuatayo:

.Ekari moja kuingia mipapai 1000-1200 ni kwa umbali gani wa mche hadi mche na mraba hadi mraba?

.Kutokana na michango nlopata humu jamvini na kwingineko, imenidhihirikia kuwa papai lipendwalo sokoni ni lile refu lenye umbo la yai- swali, je dukani naweza pata mbegu ya mipapai chotara ya mapapai marefu matupu?
Mbegu upate kwa supplier wa kuaminika vinginevyo utachakachuliwa. Halafu nawaza hivi haiwezekan kununua sokoni hayo mapapai na kuzitoa zile mbegu
 
Hatua alizoanza nazo ni sahihi kabisa huwezi kuanza kulima kitu bila kuuliza soko likoje na utamuuzia nani nawengi wanaanguka kwenye kilimo kwajiri hiyo.
Hapana siyo sahihi,, alipaswa kuuliza soko la mapapai likoje? Hapo ndio angepewa maelezo mazuri lakini kusema natafuta soko la papai inamaanisha tayari unayo unategemea kuvuna kesho kesho. Sasa fikri umeuliza hivyo anajitokeza mtu anasema nahitaji tani 3 za mapapai utasemaje? Utamwambia hata sijalima ngoja niende nikalime? Huo ndio mwanzo wa kupoteza wateja na hawatarudi tena. Hivyo tujifunze namna ya kuuliza!
 
Habari za muda wanajamvi! kutokana na dhamira yangu ya kulima papai naomba kueleweshwa yafuatayo:

.Ekari moja kuingia mipapai 1000-1200 ni kwa umbali gani wa mche hadi mche na mraba hadi mraba?

.Kutokana na michango nlopata humu jamvini na kwingineko, imenidhihirikia kuwa papai lipendwalo sokoni ni lile refu lenye umbo la yai- swali, je dukani naweza pata mbegu ya mipapai chotara ya mapapai marefu matupu?
Mkuu kama uko karibu na Morogoro nenda pale SUA utapapenda kwa mbegu za mipapai hiyo mirefurefu tena inaanza kuzalia chini hata mtoto wako wa miaka miwili anaweza kuchuma tunda!! Kama unataka ekari 1 ikupatie miche kama 1200 fanya spacing iwe 2 m x 2 m (yaani msitari hadi msitari iwe mita 2 na shimo hadi shimo iwe mita 2) kwa nafasi hiyo utapata kama miche 1225 hivi.
 
images(2).jpg
wadau wengi nimeona unaulizia upatikanaji wa mbegu jamani mbegu zipo madukani tembelea duka lolote la pembe jeo na mifugo ulizia mbegu ya papai hybrids , utapewa kazi ni kwako kuchagua unataka mapapai yepi yenye rangi nyekundu, karogi nk ni wewe tu

Mbegu hii huitaji kuiotesha wewe ni kuandaa mashimo vizuri kisha kuipanda nakuanza kuitunza tu

Hiyo mipapai katika picha ina miezi sita tu

Soko la papai lipo na kubwa tu sema watu hawastukia , unaweza tengeneza soko lako mwenyewe kwa kuwauzia mama lishe wa mitaani, pia katika hotel, pia katika hospital za mikoa, wilaya nk , haitaji utoe zao lako mkoani kupeleka dar hapo hapo ulipo unaweza fanya biashara

Wazo hili nilitoa hapa hapa JF nikalifanyia kazi na limezaa matunda, napokea sm kila siku watu wakitaji mapapai sababu ishajulikana namiliki mipapai kila mwezi na uhakika wa kutengeneza laki tano

Bei ya mbegu za hiyo mipapai inanzia elfu therathini na tano, inategemea na eneo ulilipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom