Nahitaji ushauri kwa tatizo hili

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
11,108
19,985
Habari za asubuhi wakuu. Ni mara yangu ya kwanza kupost katika jukwaa hili la Jf Doctor. Naimani nitapata ushauri wa hili tatizo langu maana ni kama siku ya nne sasa linajirudia pamoja na dawa kutumia nilizoandikiwa na daktari. Mchana ninakuwa vizuri tu nakuendelea na shuguri zangu za kila siku, ila ikishafika jioni kuanzia mida ya saa moja hali hubadirika; nasikia baridi sana, joto la mwili linapanda sana, kichwa kuuma na kukosa hamu ya kula huku tumbo likikwangua kama njaa hivi lakini si njaa.
Hali hii huwa hivyo mpaka mida ya saa saba usiku joto likiwa kali sana mwili unahitaji hali ya ubaridi. Nalazimika kulala na AC niki regulate kadri ya mwili unavyohiyaji ubaridi mpaka asubuhi.
Binafsi nilijua ni malaria, nilinunua Orodar nikameza. Tangia zamani huwa nikiumwa malaria dawa niliyokuwa nikitumia na kuniponyesha malaria mara moja ni fansida, ila nina muda mrefu sijazitumia hizi dawa. Pamoja nakunywa hizi dawa hii hali irijirudia tena usiku wa juzi. Jana mchana nilienda hospitali na kupima malaria kwa kipimo cha B/S kikaonesha no parasite seen, Neutrophils noted high daktari akaniandikia dawa za kutuliza maumivu tu na kuniambia kama hali itaendelea hivyo nirudi hospitali baada ya siku mbili. Wakati nachukua dawa kwa mpharmasia akaniongezea Cipro incase ni kama nina infections.
Sasa wakuu hii hali imejirudia jana usiku, kwakweli inanitesa sana. Naomba ushauri humu maana najua humu kuna wabobezi wa afya na madaktari. Tatizo linaweza likawa ni nini?
 
Fika hosp Pima hivi vipimo: blood group na full blood picture , then tuambie majibu kwanza,, na je hukohowi sana usiku?
 
Back
Top Bottom