Nahitaji Ushauri: Kuanzisha biashara Arusha mjini nina mtaji Kama 2M

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,132
Wakuu,
Habari za Jumapili, wale wenzangu YESU KRISTO ASIFIWE. Namshukuru Mungu ni Jumapili ya Baraka kwa wakazi wa Dar tangu Jana Jion hadi mida hii Mvua ni non-stop, Polen nyote mlioathiriwa na Mvua hii pia.

Niingie moja kwa moja kwenye Mada, natarajia baada ya miezi mitatu kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kuhamishia makazi ya kudumu Huko , kwa maana ya kuanza maisha mapya.

Baada ya kuona Dar siwezi kuendelea na pia kutokana na ya hali hewa kwa upande wangu sio rafiki sana, nimeamua niondoke moja kwa moja na kama ni kurudi labda kwa Mishe zingine ila sio kwa kuishi tena.(Ila ni pazuri kwa kufanyia mission kama unajitambua)

Kwa upande wa jiji la Arusha nilishaenda nikafanya utafiti kadogo, Pale Mbauda (sokoni) nikawaza niweze kufungua Hata huduma ya kufanyia mihamala ya kifedha (M-PESA,tigo-PESA, MAX MALIPO n. k)

Nimepanga nitafute frem Lkn naona mtaji mdogo nikafikiria kuchonga vile Vibanda vidogo, labda Angalau ili kusevu pesa nyingine, kumbuka Ninaenda kwa maana pia hata mahala pa kuishi mimi binafsi inabidi nipange chumba nikae.

Kwa wajuvi wa Huko naomba kaushauri kama ni kubadilisha hili wazo la biashara au changamoto ( Najua Zipo) ambazo sizifahamu kwa Huko, pia maeneo ya kuishi ambayo mimi naweza kugharamia.

Mawazo yako ni ya Muhimu Sana.

NAWASILISHA.
 
Dar sio kwetu mkuu, Nilienda kufight tu maisha, wewe endelea kukaa kwa Shemej yako tu haina Shida, wenzako wanaenda dar kujaribu na wanafanikiwa
Wanaume wa dar nyie bogus kabisa,kufanikiwa ni kwenda kushtaki kwa BASHITE? halaf ndio mnataka kutuletea huo ujinga huku?
 
Dar sio kwetu mkuu, Nilienda kufight tu maisha, wewe endelea kukaa kwa Shemej yako tu haina Shida, wenzako wanaenda dar kujaribu na wanafanikiwa
Umeomba ushauri jukwaani,jitahidi kuwa na busara kwenye majibu kwa kuwa wewe ndiye mwenye shida.Kwa kawaida, wapo watakaokuponda lakini jitahidi kuvumilia.
 
Umeomba ushauri jukwaani,jitahidi kuwa na busara kwenye majibu kwa kuwa wewe ndiye mwenye shida.Kwa kawaida, wapo watakaokuponda lakini jitahidi kuvumilia.
Sawa mkuu, Ngoja niwe mpole Lkn roho inauma
 
Back
Top Bottom