Nahitaji tajiri au kampuni yoyote tuweze kuungana kuieta Wenge Musica BCBG Dar

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Nikiwa kama mfuasi namba moja hapa Tanzania kama siyo Afrika ya Mashariki wa Bendi ya Wenge Musica BCBG inayoongozwa na Bingwa au Fundi au Mtaalam mwenyewe Kiongozi Jean Bedele Tshituka Mpiana najitokeza leo mbele yenu nyie MATAJIRI au WAKUREGENZI wa KAMPUNI KUBWA mbalimbali hapa Dar kuwaombeni kuwa tushirikiane ili tuweze kuileta hii Bendi kwani nina amini kwa UMAHIRI wa hii BENDI hata mkiweka kiingilio cha Tsh 500,000 ( Laki Tano ) au Tsh 1,000,000 ( Milioni Moja ) tutajazana hadi pomoni.

Kama kuna tajiri au kampuni ipo tayari basi iwasiliane na Mimi kwa PM ili tuweze kufanya mchakato wa kuileta Wenge Musica BCBG Dar ili Watanzania waamini kuwa JB Mpiana na Bendi yake ni habari nyingine kimuziki si tu DR Congo au Afrika bali hata duniani kote.

Hatutaki viingilio kama vile vya Koffi Olomide vya Tsh 3,000 ( Elfu Tatu ) au Tsh 10,000 ( Elfu Kumi ) kwani mtatujazia mno Wezi na Vibaka ukumbini na hata Wabakaji na isitoshe kuweka kiingilio hiki kidogo kwa JB Mpiana na kwa HADHI yake kubwa na UWEZO wake mkubwa ni KUMVUNJIA HESHIMA.

Nina uhakika wa 100% kwa kiingilio hicho cha kuanzia Shilingi laki tano viti vya kawaida na Shilingi milioni moja viti maalum halafu show ikifanyika uwanja wa Taifa Watu watajazana sana hadi kupita idadi ya uwezo wa uwanja wa Watu 60,000 ( Elfu Sitini ) na mtapiga HELA / PESA ambayo itavunja rekodi hadi hata Mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.

Wale wana Wenge Musica BCBG wenzangu tafadhalini tuungane ili tuweze kumleta MOTO PAMBA, MUKULU YA BAMUKULU, PAPA CHERIE, DE LA PATRIA, SOUVERAIN PREMIERE, BIN ADAM, LEADERE CHARISMATIQUE na LOKIA BILO DA KOKOO ( JB Mpiana ) ili tuwaonyeshe wale Koffi team na Werrason team kuwa bado wana safari ndefu ya wao kujipambanisha na Wenge Musica BCBG.

Nitawashukuru sana na Mungu ibariki Wenge Musica BCBG na Mungu mbariki sana JB Mpiana na Mungu tubariki wana Wenge Musica BCBG wote na uwalaani wale TEAM Koffi na Werrason ambao kutwa WANATUONEA WIVU na kutusema vibaya tena washindwe na walegee!
 
Back
Top Bottom