Nahitaji neno la wadada wote wa JF kwenye hili... Hata wanaume semeni pia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji neno la wadada wote wa JF kwenye hili... Hata wanaume semeni pia!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Sep 1, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Dada huyu anaitwa Amina(siyo jina halisi) aliolewa miaka 2 iliyopita,mumewe bwana Rajabu(siyo jina halisi)ni mfanyakazi kwenye kampuni moja ya uchimbaji wa madini.Tatizo ni hili:Amina na mumewe mwanzoni mwa ndoa yao ilikua njema sana kabla ya mumewe bwana Rajabu kupata jimama lililosababisha Rajabu kuisahau kabisa familia yake.Rajabu alianza vituko wakati mkewe ana ujauzito wa miezi 7,alikua akimpiga,hela ya matumizi akawa anatoa kidogo na wakati mwingine hatoi.Amina ikabidi amwite mama yake kutoka Tabora,nae mama hakusita,akaja lakini akashindwa kumweka sawa mkwe,yaani ndo akawa halali nyumbani.Akawa anarudi asubuhi kubadili nguo na kuondoka.Hali ikawa mbaya nyumbani,ndugu zake mume wa Amina walijaribu kumweka sawa ndugu yao bila mafanikio ndipo mdogo wake wa kiume mumewe Amina akawa anamhudumia shemejie kwa matumizi,wala mumewe Amina hakujali.Hata alipopelekwa kujifungua hostl ya Bugando,mumewe hakwenda,na alijifungua kwa upasuaji na bahati mbaya mtoto alifariki.Shemejie Amina ndo aligharamia kila kitu na alipotoka kodi ya nyumba aliyokua anaishi iliisha na shemejie alilipa.Mama wa Amina alishuhudia yote haya.Mumewe Amina alianza kumtuhumu mkewe kujihusisha kimapenzi na shemejie,eti kama hawana uhusiano mdogo wake asingemhudumia namna ile,jambo hilo lilisababisha mpaka mumewe Amina kukorofishana na mdogo wake,ilipofikia hapo Amina alitengana na mumewe na kwa msaada wa shemeji yake alipata kazi kiwanda cha bia Serengeti(Mwanza)Sasa imepita miezi 5,mumewe Amina anataka warudiane,Amina anadai hana hisia kabisa na mumewe.Yeye Amina kwa muda sasa amekua na hisia zaidi kwa mdogo wake mumewe,amejizuia lakini kila akikumbuka shemeji yake alivyokua anamjali na kuhangaika anazidi kutamani kuwa karibu nae,huwa wanawasiliana na wakati mwingine shemejie Amina humtembelea anakoishi Amina na Amina hajawahi kumwambia shemeji yake anavyojisikia.Amina hajui afanye nini,hataki hata kumuona mumewe na hisia juu ya shemejie zinamsumbua.Hebu funguka,afanyeje?Mumewe huwa mpaka analia kumsihi warudiane,lakini mkewe hataki,kumbuka shemejie Amina hajaoa,je inawezekana Amina na shemejie wakaoana?Nataka mtazamo wako,mimi wangu ninao,hebu nione wako!
   
 2. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,443
  Trophy Points: 280
  Aachane na hiyo kitu ya shemeji watauawa bure. Sana sana arudiane na mumewe kama anajisikia kunyanyaswa tena au hata kuambikizwa magonjwa kwani hajui mumewe kazoa nini
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kama ningekuwa Amina.......shemeji halali yangu.....
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mapenzi ni pamoja na care taking!kimsingi amina ana haki ya kupenda tena,ana haki ya kujisikia anapendwa.tatizo ni anayempenda ni shemeji(actually ni mdogo wa aliyekuwa mume wake)nafikiri kuna tofauti hapo!aha bwana eeeeeeenh najiuma uuuuuma! kwani kitu gani?waoane tu!
   
 5. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Haiwezekani mtu na shemejie kuoana!
   
 6. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  preta natafuta pa kukugongea like sipaoni bana!
   
 7. awp

  awp JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii ngumu kumeza. mimi nashauri (1). asirudiane na mumewe hata kama akatoa machozi ya damu. (2). asithubutu kumwonyesha au muktamkia shemeji yake kuwa nampenda kwani kufanya hivyo ataongeza uhasama mkubwa sana kwa familia zao. (3). avute subira atapata mwingine wa kumliwaza ukizingatia kwa sana mume anaye (KAZI).
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mtaishia kwenye uroda tu! Kuoana hakuta dumu!!
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Angetafuta mwingine tofauti na shemejiye.
  Hawa wanandugu watakuja kuuana hivi hivi.

  ILA KUNA USEMI HUU: KILA KIMLACHO MWENZAKE HAKIKA KINA NJAA!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hakuna haja ya kumrudia mumewe......

  ila hawezi kuwa na shemeji yake...... atulize akili hizo hisia sio za mapenzi....ni macare tu ndo yamemchanganya
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wewe............utani huo sasa!
  Hv si unajua mapenzi ama unasikiaga??


   
 12. n

  ngala moja Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  preta hapo ndipo wanawake wanapoingizwa mjini. kisa eti mkaka kamuonea kamsaidia ktk matatizo naye anamgawia kwa kulipa wema.huo ni kichaa.kuhusu hilo wala asithubutu maana katu hawatakua na amani maana ni kuvunja ukoo wa watu na tuhuma za awali zitahalalishwa na wao wajapo ingia ktk mahusiano. mdada ana kazi yake avute subira atapata mwingine atakayemjali nje ya ukoo huo. na afute kabisa wazo la kumtamani shemejie hata kama alimtendea wema maana kwa kiasi fulani shemejie alikuwa anafukia matendo maovu ya kakake ili yasidhihiri nje na kuwa aibu ya ukoo mzima japo juhudi zake ziligonga mwamba. maisha mbele kwa mbele.preta w end njema
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ninavyofahamu karne hii hakuna taboos lol
   
 14. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Mbona zamani kurithiana kupo ampe shemeji machine asukume mzigo
   
 15. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hii kitendawili nayo...

  With no intention to distort the motion....................vipi kama angekuwa rafiki wa kufa na kuzikana na sio mdogo mtu??????
   
 16. S

  SHIRIRAM New Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikia, uwezekano wa kuwawapenzi upo je shemejie amina anahisia kwa amina? bt 2kumbuke hawa ni ngugu atafute mwingine wakae wapeane raha sio shemejie
   
 17. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kimsingi kama huyo bwana hajatoa talaka bado ni mke wake! uzuri mmoja wa dini ya Kiislam ukishatoa/pata talaka basi anakua huru. Sasa huyu Amina hajapokea talaka, yeye amekimbia nyumbani kwa mumewe japokua mumewe ana makosa makubwa yasiyoweza kusamehewa. Kweli mi nachomshauri huyo Amina adai talaka ili awe huru na huyo kisirani. Yeye aliona mimba imefika miezi 7 hawazi tena kula mzigo kahimia kwa lijimama! Mtu kama huyu hapa kwetu Yemen, ni chakula ya Nguruwe, hafai kuishi na mtu. Huyo shemeji mtu nae anaweza kujiingiza kwenye matatizo kama huyo kisirani atagundua dogo anakula mzigo wake asiyoutunza. Ila kama shemeji analipa, dogo hana budi kuonja kidogo tu, yan SUNA
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  hahaha Preta bwana una vituko
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Cha msingi hapa naona aachane na wote
  Kwanza akianza mahusiano na shemeji itaanza kuleta migongano katika familia zao kwa ujumla
  Pili kama hana hisia na mmewe kabisa akae atulie inawezekana yupo mungu aliyempangia katika maisha yake
  Lakini kuanza mahusiano na shemeji yake aachane na hilo wazo kabisa..
  Uzuri wanaume bado wapo hawajaisha duniani kama hamuhitaji mmewe..
  *****************shemeji NO***************************
   
 20. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Preta Preata niatakusemelea kwa Ndallo weyeee....
   
Loading...