Nahitaji nafasi ya kumsaidia Rais kukuza uchumi

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Nina imani hili jukwaa linasomwa na watu walio karibu na rais au hata rais mwenyewe. Nawaomba wanifikishie ombi langu kwa mheshimiwa rais wangu.

Nafikiri sio mimi peke yangu, nadhani kuna watanzania wengi wenye mawazo bora kabisa na ni wasomi waliobobea kwenye nyanja tofauti na wangependa kuiona nchi inapaa kupitia taalama zao, lakini kutokana na kutokuwa na majina au umaarufu hawawezi kuonekana kwa mheshimiwa.

Badala yake wanaoteuliwa ni makada wa CCM na maprofesa wanaojulikana. Kwa niaba ya wachumi wenzangu na wasomi wengine ambao hatujulikani naomba kuchukua nafasi hii kumuomba mheshimiwa rais anipe nafasi ya kumsaidia katika jitihada zake za kuipaisha hii nchi.

Kusema kweli rais anafanya mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi hivyo anahitaji watu sahihi kuwa karibu yake kumsaidia mawazo mengine mazuri ya kuipeleka Tanzania sehemu anayoitaka. Mimi ni mtaalamu wa uchumi na ni mtaalamu wa fedha wa kiwango cha juu kabisa. Elimu yangu nimeipata nje ya mipaka ya Tanzania.

Hivyo mbali na elimu yangu pia nina exposure na practical experience ya nchi zilioendelea. Hivyo mchango wangu utakuwa wa kipractical zaidi kuliko kinadharia.

Naweza kuyaelezea mawazo yangu hapa na namna nitakavyomsaidia rais kuipaisha hii nchi lakini naona si jambo jema kuanika kila kitu hapa maana mambo ya kiuchumi ni mapana sana.

Naomba niishie hapa. Wahusika tafadhalini sana fikisheni ombi langu kwa mheshimiwa. Wengine hatuna majina ya kuonekana ili tuteuliwe, tunaweza kufa na ujuzi wetu.
 
ipaishe familia yako mkuu, njaa zitakuua, umeamua kuja na id ya msukumu original ili iwe kutuaminisha kwamba ukabila umetamalaki kwenye utawala wa juma ponda mali aka jpm?
 
Msukuma Original yaani wewe ujiunge tu jana tu 02/10/2018 hapa JF na utake kumsaidia Rais, kwani huna kazi nyingine hapo nyumbani kwako? au kwa vile ni kabila lako
una miradi mingapi umeifanya, kwanini usiende ziwani ukawape elimu ya majangwa na amna ya kujiokoa Ziwani, kuna migodi haitemi tena na imeng'ang'aniwa na wageni mpaka wanajificha vyooni kuna mifugo
1538545022569.png

hapo ni Dar wajanja wote hao walisave baada ya kivuko kuchafuka, ww ungetoa maoni gani wakakusikia km Msukuma?
 
Back
Top Bottom