Nahitaji msaada wa mawazo na ushauri nini nifanye juu ya hii Tsh Milioni 8

Sipajua Katoro na sijui wingi wa watu huko ila ningeshauri fanyia uchunguzi hiz biashara

1. Vifaa vya pikipiki na baiskeli
2. Kuna zile biashara machinga wanauza kama sosi, mikanda, saa n.l
3. Mahitaji ya vitu vya ndan - Mangi shop
Katoro ni kamji ka madini huko geita , na kuna uwezekano mkubwa hata mdau ni mtu wa madini , maana the way anaielezea hiyo pesa definety inatoka katika mazingira ya zari... Kuna jiwe ameuza I guess

Biashara hizo ulizomshauri zinaweza zikamsaidia haswa kwa location ya katoro.
 
La hajui ni biashara gani afanye utampoteza , biashara inataka kwanza taarifa za kutosha nini ufanye , sio juu kea juu na hela yako unafanya biashara , utachoma pesa yote

Wewe ulidhani baada ya ushauri wangu, jamaa angeenda kuzianika fedha barabarani bila hata kupata tips 2, 3 kuhusu biashara!??? Hivi hudhani kusema ^anzisha biashara^ ni package ya vitu vingi!??? Which school did you go even!???
 
Wewe ulidhani baada ya ushauri wangu, jamaa angeenda kuzianika fedha barabarani bila hata kupata tips 2, 3 kuhusu biashara!??? Hivi hudhani kusema ^anzisha biashara^ ni package ya vitu vingi!??? Which school did you go even!???
Shule yetu hii haisaidiii kwenye biashara za mitaji midogo kama hiii let alone mikubwa !
Biashara ni art, wastaafu wangapi Wanachoma pension zao kwa kufanya biashara kichwa kichwa , tena millions of shillings ndani ya muda mfupi na wanakufa masikini ?

Huyu jamaa hiyo pesa kwanza ni ndogo na inaonekana amebahatisha sehemu . Kama unamshauri biashara basi iwe ya kumshika kabisa na mkono under your guidance or else anapoteza pesa yote wiki nyingi.

'Biashara ni package ya vitu vingi' sikatai Ila kama huna taarifa za kutosha usifanye biashara .
 
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili
Milion 5 peleka kwenye ujenzi. ...milion tatu wekeza kwenye biashara ya mashuka na vifuniko vya asali...inalipa sana ukitaka connection na masoko tuwasiliane
 
Natumai wewe ni mtumishi na hiyo pesa umekopa kwa marejesho ya miaka mitano so ushauri wangu nenda kajenge hata vyumba vitatu unavosema hamia kibishi alafu tafuta pesa nyingine ndio unanze beating ya biashara sasa maana were ni mwajiriwa so hiyo pesa ikikata kuja ipata nyingiane ukajenga ni zali so jenga jenga narudia jenga bi
 
Milion8 kwa nyumba ya vyumba vitatu kisha ibaki milioni mbili? Inamaana nyumba vyumba vitatu utakuwa umejenga kwa mil.6? Kweli mkuu?
Inawezekana vyumba vitatu vilivyofuatana, bila jiko, sebule sijui dining na anaezeka slope.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
je kwa mfano dada angu kwa mtu mwenye uzoefu na biashara ya kununua madini kwa huu mtaji si unamtosha kabsaaa nishauri tafadhari.....nataka kuanza hii biashara hapo kimtaji na milioni 10
Unatosha sana mkuu...ila kuwa makini..inawezekan kns ndan ya mwaka 1 ukawa huna hela kbs..tunaita "kukatika"
 
Chukua milioni mbili tu. Anza kufanya biashara ya mazao,hio nyingine usiiguse kabisa mpk uone unaijua hio biashara. Angalia hapo ulipo bei za mazao ukilinganisha na mjini piga hesabu anza kazi taratibu. Baada ya muda tumia faida kujenga nyumba yako wakati huohuo ukiwa na biashara yako.
 
Nilitaka kusema ilete nikuwekee mwanangu ila acha tu.

Nyumba ndio kitu muhimu kwa hiyo vyumba 2 vya masta sebule na chumba kidogo kama jiko ukisimamia mwenyewe 100%, waweza weka hadi bati la kibongo lakini baadae ukamalizia hizo finishing kidogo kidogo.

Biashara ni kama kamari waweza kula au kuliwa.

Yote kwa yote omba Mungu akusimamie.
Bonge la hekima!
 
Katoto mwanangu mbona unajenga? Hiyo hela inatosha! Ila biashara kwa Katoro ungetoka, labda hutaki! Ulitaka kuweka kwenye biashara gani?
Kwa biashara ndio sijui nifanye ipi maana sina experience hivyo nikaona niweke humu wazo langu la kuomba ushauri ili nione nielekee uelekeo upi, hata nikipata mtu akanishika mkono itasaidia sana sema ndio hivyo sina mtu huyo!
 
Jenga nyumba yako chenji inayobaki olea anza kutafuta nyingine. Kama unae mke wote hamuwezi kua hamna experience ya biashara muulize mkeo anaweza do biz gan mpe mtaji bakisha kidogo ya kuingia nayo viwanja ukisubiri breaking🤒🤒🤒🤒🤒
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom