Nahitaji msaada wa mawazo na ushauri nini nifanye juu ya hii Tsh Milioni 8

muhala.jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
726
1,000
Njoo kweny biashara ya mkonge tuu tena weka mil 4 fixed account njoo na nne. Utakuja nishukuru badae baada ya mwaka utawez jenga nyumb ya kisasa kabisa
 
kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,932
2,000
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili
fungua biashara mkuu uza bia za jumla depot flani hivi wekeza kama milioni 5 hivi alafu iyo tatu iwe kama emergency ukiwa unataka kuanguka inakua inakupa back up bia ni biashara ambayo sio pasua kichwa kwasababu kreti zinahesabika
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,950
2,000
Umepataje? Kama ni kwa njia ya biashara nasisitiza irudishe huko huko kwenye hiyo biashara.

Kama zali (kubeti, kuokota, kurithi, umeiba..etc), jaribu biashara ila lazima iyo biashara uwe ushaianza uongeze tu mtaji.

Hiyo hela haitoshi nyumba labda uwe kiwanja unacho na upo mkoani.
Hii dhana ya ujenzi wa mikoani ni cheap sio kweli kwa baadhi ya sehemu, mm nimejenga nyumba ya kwanza Arusha ya pili nimekuja kujenga Dar baada ya kuhamia kikazi qisee nakuhakikishiq ujenzi wa Dar ni rahisi sana ukilinganishq na wa Arusha. Hata viwanja Arusha almost mji wote viwanja bei juu start from 15M mfano Moshono etc. Wakati hapa nimepata kiwanja kigamboni kikubwa kwa 7M, gharama za mafundi Arusha ni kubwa ukilinganisha na hapa, Material like wise Dar ni cheap, unapata wapi ujasiri wa ku generalize kuwa mkoani ujenzi ni rahisi?
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,950
2,000
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili
Katika kosa kubwa ambalo wengi tunafanya ni kuamua kujenga wakati tunatambua kuwa fedha hiyo haitamalizq ujenzi kwa maana ya nyumba kuwa asset.
Nakushauri ndugu yangu, wekeza kwenye biashara, baadae faida itokanayo na biashara hiyo ndo itumike kujenga na nyumba itaisha kwa sababu income generation itakuwa inapatikana assuming that everything will be constant!!
 
Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
917
1,000
acha woga kijana jifanye kam hukuwahi kupata pesa kabisa, usiitolee macho m8! chukua bajaj m7.5 tu uko road laki tano tenga pesa ya reseni na uanze mchaka mchaka..!
 
iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,898
2,000
Million 8 haiwez kumaliza vyumba vitatu unaweza kuipandisha boma ila ukashindwa kupaua na kwasasa ndo balaa maana Vifaa vya ujenzi vimepanda bei

Bora ufanye biashara na kwenye biashara usiweke hiyo hela yote unaweza kuipoteza, kwakua upo geita tumia 3Million kuanzisha biashara kiasi kingine kinacho bak uweke akiba kwa kununua mazao yaweke ndani, maana ukisema uweke mfukon utaitumia na itaisha fasta ila ukiwa na mazao ndan unaweza kuja kunufaika kama yatapanda bei, kwa Sasa unaweza kununua mpunga ukaweka ndan kwakua mpunga huwa hauliwi na wadudu na ukizingatia mvua mwaka huu ni chache badae inaweza kufumuka bei.

Hiyo 3M izungushe kwenye biashara ambayo unaona unaweza kuimudu, kwa geita Kuna maeneo mengi ya karibu yenye machimbo hasa wachimbaji wadogo, kajichanganye huko fungua kibanda chako kidogo uza vinywaji, maji yanauzika sana huko, soda , juice ndo usiseme wapelekee hata juice ya mua, alaf hapohapo unakua na sehem ya kuchajisha simu unaokota 300 kila simu, au uza chakula machimbon huko ndo vitu vinavyo uzika sana maana kula ni lazima kutokana na kazi ngumu, wanakula sana nyama choma na ugali , mbuzi huko kwa siku unaweza kuchoma mbuzi wawili , mbuzi mmoja mkubwa anauzwa kwanzia tsh 40,000/=

Ukiona hiyo ya machimbo inakuzingua nunua boda boda piga kaz hapo hapo , kwa siku hukos elf 10+ na kwakua itakua ni yako faida utaiona na utatuza baiki yako, fanya haya yote tu ilimrad hiyo hela izunguke ukiendelea kujifikiria utashangaa imeisha ghafla tu na hautajua imepitia wapi , zingatia usiingize yote kwenye biashara moja utaipoteza anza kidogo na ukiona biashara hiyo imekubali ndo uongeze taratibu kwa tahadhari.
 
Kideme

Member
Apr 13, 2020
96
125
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili
Jenga kwanza, mwenyewe unakiri kwamba huna uzoefu wa biashara yoyote, utapoteza fedha zako bure
 
Sibaru

Member
Aug 29, 2017
39
125
Njoo kweny biashara ya mkonge tuu tena weka mil 4 fixed account njoo na nne. Utakuja nishukuru badae baada ya mwaka utawez jenga nyumb ya kisasa kabisa
mkuu funguka kidogo kuhusu hiyo biashara ya mkonge wahitaji tupo wengi hapa
 
Sosoma Jr

JF-Expert Member
Aug 7, 2020
266
250
mkuu funguka kidogo kuhusu hiyo biashara ya mkonge wahitaji tupo wengi hapa
Funguka macho hamka usingizini kuna mdau hapo juu amesema katika 8M chukua 4m nenda katafute shamba mkoani kanunue ekari 10 hata 2m haishi wekeza katani katika hekari zako hizo 2m nyingine nunua miche panda weka mtu wa kukuangalizia na 4m nyingine wekeza kwenye ujenzi wa nyumba unaosema nikimaanisha anza msingi ishia kati vyumba vyako vitatu masta, jiko, choo ndani kwa ndani halafu tulia baada ya mwaka shamba litatema bidhaa za kutosha zitarudisha hela zaidi ya mara kumi ya hela uliowekeza na utakuja kumalizia nyumba yako ilioishia kwenye foundation.
Wazo hili lifanyie kazi utakuja kunitafuta na kunishukuru kwa mchango wangu kwako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom