Nahitaji msaada wa mawazo juu ya biashara ya mifugo (ngombe & mbuzi)

Asante kwa maoni yako mkuu, ila ningependa kuuliza kitu.

Unapoamua kuwaachia ngo'mbe wazurule kwenye eneo kubwa labda hekari 50-100,maana yake ni unawafuga kama vile wako kwenye mbuga na kutegemea uoto wa sehemu husika? Au unamaanisha wapate tu nafasi ya kutembeatembea huku nikiwahudumia kwa chakula?
Wajiokotee kidogo (uoto uliosalama).
Wapatie suppliments (za kununua).

Kikubwa kinachopatikana kuwaachia wazurure ni wao kuweza kula kwa wakati na kiasi wanachohitaji.
Ng'ombe wa kufugwa bandani wanalazimishwa kula kila wanapolia, lakini ikumbukwe sio milio yote ni njaa. Akivimbiwa uzalishaji ni mdogo sana.

Kingine anayezurura anapata mazoezi, yanasaidia mmengenyo wa chakula. Ikumbukwe Ngombe hucheua na kutafuna tena. Huyu wa kufungwa uwezo wake wa kucheua ni mdogo kulinganisha na mzururaji kwenye padoki.
 
Kwa Ufugaji wa kisasa wenye tija eneo hilo ni dogo kulinganisha na idadi ya ng'ombe anayoilenga mwenye eneo.

Ng'ombe 100 kwa ekari 50 ni wastani wa ng'ombe mbili kila heka. Kila ng'ombe na nusu eka. Bado haujaondoa maeneo ya Barabara za ndani, maeneo ya kutunzia vyakula na vitendea kazi, majosho, pits za kutunzia hays. Na hapo ni kama eneo lote ni tambarare na kavu, kama kuna vilima ns maji navyo vinachukua eneo la shamba. So mwisho wa siku inakuwa ni ngombe mmoja kwa robo eka. Eneo halitoshi. Litatosha tu kama ng'ombe ni wa bandani. Ng'ombe wa bandani hakupi maximu profit hata siku moja.

Ng'ombe anahitaji kutembea tembea ili azalishe maziwa mengi na nyama nyingi.

Tembelea Ranches na vituo vya mifugo
Mkuu binafsi naona inawezekana japo yaweza kua gharama maana anaweza kutumia
1. Rotational grazing ambapo ataweka kitu kama padock /cage /kizuizi ng'mbe wanachunga eneo la ekari kadhaa huku eneo jingine limefungwa ng'mbe awawezi kucross kwenda upande mwingine then pale upande mmoja umepungua malisho unafungulia upande mwingine mzunguko unaenda hivo kule wakimaliza huku pia panakua tayari malisho yameshakua kutumika.

2.Established pasture hii njia anaweza kua anapanda majani yake mwenyewe kama chloris gayana ,cenchrias ceriaris na n.k so itasaidia kuhakikisha uwepo wa malisho ya kutosha kwenye maeneo yake.

3.Kustore malisho kama kutengeneza hay na silage ni njia moja wapo bora ya kutunza malisho.

4.kutumia mabaki ya mazao mfano utakuta kwenye eneo lake kuna wakulima wa mahindi baada mavuno anaenda kuomba mabua anayakusanya kwa wingi anapereka shambani kwake yanachanganywa na molases kuongeza ladha ng'mbe wanatumia.

5.kutumia concentrates zenye mashudu ya pamba au alizeti,pumba ,madini nk
 
Mkuu binafsi naona inawezekana japo yaweza kua gharama maana anaweza kutumia
1. rotational grazing ambapo ataweka kitu kama padock /cage /kizuizi ng'mbe wanachunga eneo la ekari kadhaa huku eneo jingine limefungwa ng'mbe awawezi kucross kwenda upande mwingine then pale upande mmoja umepungua malisho unafungulia upande mwingine mzunguko unaenda hivo kule wakimaliza huku pia panakua tayari malisho yameshakua kutumika.
2.established pasture hii njia anaweza kua anapanda majani yake mwenyewe kama chloris gayana ,cenchrias ceriaris na n.k so itasaidia kuhakikisha uwepo wa malisho ya kutosha kwenye maeneo yake
3.kustore malisho kama kutengeneza hay na silage ni njia moja wapo bora ya kutunza malisho
4.kutumia mabaki ya mazao mfano utakuta kwenye eneo lake kuna wakulima wa mahindi baada mavuno anaenda kuomba mabua anayakusanya kwa wingi anapereka shambani kwake yanachanganywa na molases kuongeza ladha ng'mbe wanatumia.
5.kutumia concentrates zenye mashudu ya pamba au alizeti,pumba ,madini nk
Daaah mkuu unajitoa sana katika kuelimisha, unapatikana wapi?
 
Pia anaweza kupotezea madume kabisa akawa anafanya Artificial Insermination.

Hii itamsaidia sana pia kiamua ni ndama wa breed gani anamtaka. Itampa nafasi kubwa ya kuchagua breed kuendana na mazingira na uhitaji wake. Mfano anataka breed inayovumilia joto au baridi, inayovumilia ukame au breed inayotoa nyama zaidi au maziwa zaidi.
Kwa upande wa Artificial insemination tz bado atujaanza kuvuna mbegu kwa madume wa ng'mbe asilia AI inatumika zaidi kwa ng'mbe wa kisasa kama frisiean na arshire only pale naic arusha wanafanya hio.
Ila pia hio ni expensive kumlipa mtaalamu
 
Hao ni ng'mbe aina ya ankole

Ukitaka pia dizain hii tunaweza kuwasiliana
IMG_20211102_205357.jpg
 
Back
Top Bottom