Nahitaji msaada wa mawazo juu ya biashara ya mifugo (ngombe & mbuzi)

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
10,409
19,925
Habari zenu wana JamiiForums, mimi kama kijana mtafutaji na mwenye kiu ya mafanikio, nimeamua kuja kwenu Ili nipate ABC juu ya mada tajwa hapo juu. Nimejaribu kupitia maada mbalimbali za zamani juu ya hii maada ila sikufanikiwa kupata data nilizokuwa nazihitaji, hasa ukizingatia taarifa za zamani huenda zisiwe applicable miaka hii.

Nina eneo la hekari 50 ambalo liko nje ya mji, ni muda mrefu sana nilikuwa na ndoto za kufuga ngo'mbe kwaajili ya biashara ila sina uzoefu na hiyo biashara, hivyo nilikuwa naomba kujua namna ya uendeshaji (ufugaji), Mtaji, Masoko na Faida ya hii biashara, bila kusahau chamgamoto zote za hii project.

Napatikana Mwanza, na eneo langu ninalolizungumzia lipo CHATO, ndoto yangu ni siku moja nimiliki ngo'mbe wengi kuanzia 100 nakuendelea.

Msaada wenu tafadhali.
 
salmin siraj

Senior Member
Oct 10, 2017
195
185
Ranchi zetu ndo zinaongoza kufeli katika nchii hii

Lakini pia kwa ekari 50 arthi yake ni kubwa tu anawez kufanya wonders katika ufugaji
Hongera sana kwa kumiliki ardhi kubwa lakini kwa vision uliyonayo hiyo ardhi Bado ni ndogo.

Tembelea ranch yeyote au vituo vya huduma na za kilimo utapata mwanga.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
5,258
18,776
Hongera sana kwa kumiliki ardhi kubwa lakini kwa vision uliyonayo hiyo ardhi Bado ni ndogo.

Tembelea ranch yeyote au vituo vya huduma na za kilimo utapata mwanga.
Ukubwa ni relative sana mkuu

Kwa hekari hizo ni sawa na square mita 202,342.82 ambapo kwa wastani ni sawa na upana wa mita 449 kwa urefu wa mita 449. Ukubwa huu si haba mkuu kwa ufugaji wa ng'ombe 100.
 
Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
10,409
19,925
Mkuu unataka kuanza na ng'ombe wangapi?
Nafikiria kuanza na Ngo'mbe 25 Ili niuosme upepo kwanza, ikiwa mambo yataenda kama jinsi ambavyo natarajia, nitaongeza wengine ishirini.

Bado naumiza akili juu ya uwiano utakaofaa, Kati ya madume (nzagamba) na majike, kuna jamaa hapo juu kanisahuri nitembelee ranch mbalimbali Ili kujionea mambo yanavyokwenda, natarajia kufanya hivyo.
 
salmin siraj

Senior Member
Oct 10, 2017
195
185
Nafikiria kuanza na Ngo'mbe 25 Ili niuosme upepo kwanza, ikiwa mambo yataenda kama jinsi ambavyo natarajia, nitaongeza wengine ishirini.

Bado naumiza akili juu ya uwiano utakaofaa, Kati ya madume (nzagamba) na majike, kuna jamaa hapo juu kanisahuri nitembelee ranch mbalimbali Ili kujionea mambo yanavyokwenda, natarajia kufanya hivyo.
Kama ulimskia mweshimiwa spika ndungai juzi aliziponda sana ranchi za hapa tanzania kwamba ni mbovu na ni kwel ranchi zetu nyingi ubabaishaji so kama unataka ushauri ni vema zaidi ukaenda kwa wafugaji wenyewe au ranchi binafsi ambayo sijui kama tz zipo

Ila kwaupande wa ratio ya majike na madume mara nyingi hua 25 :1 au 20:1 dume la mbegu moja linauwezo kuwadumia majike 20 -25 muhimu ni kuhakikisha dume anashiba na afya ipo.

Unaweza kuselect breed nzuri mfano boran au wale ankole ambao ukuaji wao uko haraka na wanagain uzito kwa speed hapo faida utaiona.
 
Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
10,409
19,925
Kama ulimskia mweshimiwa spika ndungai juzi aliziponda sana ranchi za hapa tanzania kwamba ni mbovu na ni kwel ranchi zetu nyingi ubabaishaji so kama unataka ushauri ni vema zaidi ukaenda kwa wafugaji wenyewe au ranchi binafsi ambayo sjui kama tz zipo

Daaah, inaonekana una uzoefu mkubwa sana juu ya ufugaji wa ngo'mbe.

Mimi kuna kipindi wakati niko chuo,nilinunua ngo'mbe 6 majike ila kwakua sikuwa na muda niliamua kuzipeleka (kuwekesha) kwa mjomba wangu ambae alikuwa na Ngo'mbe zaidi ya 350,ambazo aligawanya katika maeneo mbali mbalimbali yaani Chato, Runazi na Kakonko. Walizaliana wakafika 17,ila baadae alipofariki kilitokea ugomvi mkubwa sana wa mali nikaona niziache tu, maana ni bora uhai kuliko mali.

Now nimejipanga nataka nijenge nyumba kwaajili ya wafugaji, nijenge zizi zuri , alafu nipeleke ngo'mbe huko. Nafikiria kufuga ngo'mbe aina ya nyankole.
 
Ni kwel ni nauzoefu mkuu na ni taaluma yangu nilisomea chuo kikuu cha kilimo sokoine (SUA) nauzoefu wa maswala ya ranchi nimekaa kongwa na ruvu ranchi operation zake nazijua. Idea yako naisuport kwa asilimia zote uskatishwe tamaa fanya utapata tu matokeo mazuri. Uliza swali la kitaalamu la aina yeyeto kuhusu ufugaji sitosita kukukwambia mkuu
 
Hao ni ng'mbe aina ya ankole

Screenshot_2021-05-30-23-46-24-1.jpeg
 
Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
10,409
19,925
Hawa ukipeleka Comoro unapiga ela ndefu sana,au ukawauzia wafanyabiashara wa Comoro ruvu mnadani,ata ukiwa nao mia mbili wanaisha Sikh hiyo hiyo
Vipi bei yake mkuu, kwa mfano labda nataka kununua jike ambaye hajaanza kuzaa kabisa.
 
Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,980
2,446
Heka 50 ni ndogo duh watu bana
Kwa Ufugaji wa kisasa wenye tija eneo hilo ni dogo kulinganisha na idadi ya ng'ombe anayoilenga mwenye eneo.

Ng'ombe 100 kwa ekari 50 ni wastani wa ng'ombe mbili kila heka. Kila ng'ombe na nusu eka. Bado haujaondoa maeneo ya Barabara za ndani, maeneo ya kutunzia vyakula na vitendea kazi, majosho, pits za kutunzia hays. Na hapo ni kama eneo lote ni tambarare na kavu, kama kuna vilima ns maji navyo vinachukua eneo la shamba. So mwisho wa siku inakuwa ni ngombe mmoja kwa robo eka. Eneo halitoshi. Litatosha tu kama ng'ombe ni wa bandani. Ng'ombe wa bandani hakupi maximu profit hata siku moja.

Ng'ombe anahitaji kutembea tembea ili azalishe maziwa mengi na nyama nyingi.

Tembelea Ranches na vituo vya mifugo
 
Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,980
2,446
Kama ulimskia mweshimiwa spika ndungai juzi aliziponda sana ranchi za hapa tanzania kwamba ni mbovu na ni kwel ranchi zetu nyingi ubabaishaji so kama unataka ushauri ni vema zaidi ukaenda kwa wafugaji wenyewe au ranchi binafsi ambayo sjui kama tz zipo

Ila kwaupande wa ratio ya majike na madume mara nyingi hua 25 :1 au 20:1 dume la mbegu moja linauwezo kuwadumia majike 20 -25 muhimu ni kuhakikisha dume anashiba na afya ipo.

Unaweza kuselect breed nzuri mfano boran au wale ankole ambao ukuaji wao uko haraka na wanagain uzito kwa speed hapo faida utaiona.
Pia anaweza kupotezea madume kabisa akawa anafanya Artificial Insermination.

Hii itamsaidia sana pia kiamua ni ndama wa breed gani anamtaka. Itampa nafasi kubwa ya kuchagua breed kuendana na mazingira na uhitaji wake. Mfano anataka breed inayovumilia joto au baridi, inayovumilia ukame au breed inayotoa nyama zaidi au maziwa zaidi.
 
Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
10,409
19,925
Kwa Ufugaji wa kisasa wenye tija eneo hilo ni dogo kulinganisha na idadi ya ng'ombe anayoilenga mwenye eneo.

Ng'ombe 100 kwa ekari 50 ni wastani wa ng'ombe mbili kila heka. Kila ng'ombe na nusu eka. Bado haujaondoa maeneo ya Barabara za ndani, maeneo ya kutunzia vyakula na vitendea kazi, majosho, pits za kutunzia hays. Na hapo ni kama eneo lote ni tambarare na kavu, kama kuna vilima ns maji navyo vinachukua eneo la shamba. So mwisho wa siku inakuwa ni ngombe mmoja kwa robo eka. Eneo halitoshi. Litatosha tu kama ng'ombe ni wa bandani. Ng'ombe wa bandani hakupi maximu profit hata siku moja.

Ng'ombe anahitaji kutembea tembea ili azalishe maziwa mengi na nyama nyingi.

Tembelea Ranches na vituo vya mifugo
Asante kwa maoni yako mkuu, ila ningependa kuuliza kitu.

Unapoamua kuwaachia ngo'mbe wazurule kwenye eneo kubwa labda hekari 50-100,maana yake ni unawafuga kama vile wako kwenye mbuga na kutegemea uoto wa sehemu husika? Au unamaanisha wapate tu nafasi ya kutembeatembea huku nikiwahudumia kwa chakula?
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom