Nahitaji msaada wa kisheria wa jinsi ya kulipa deni langu kwa mkupuo

Achinsyene

Member
Jan 28, 2017
24
21
Habari ya asubuhi wakuu. Mimi ni mfanyakazi wa serikali. Mwaka 2014 nilichukua mkopo kwenye benki moja kwa mashart ya kukatwa kwenye mshahara wangu kwa muda wa miezi 48 (miaka minne).

Lakini pia mkataba uliruhusu kulipa kwa mkupuo binafsi baada ya kukatwa kwenye mshahara wangu kwa muda usiopungua miez 8.

Nimekatwa kwenye mshahara wangu kwa miezi 34 sasa ila nilipowaomba balance ili nilipe kwa mkupuo mimi mwenyewe, wamekuwa wakinizungusha kwa muda wa miezi miwili sasa, na mara ya mwisho wamenijibu haiwezekani.

Naomba ushauri wenu wajuvi wa sheria nichukue hatua gani?
 
Hakuna uongozi hapo....? Nenda kwa uongozi achana na idara inayoshughulikia na suala lako. Kama kwenye mkataba Kuna hicho kipengere kinachokuwezesha kulipa cash. Panda ngazi, utapata jibu kwa nini wanakiuka mkataba.
 
Hapo Watumie Demand Notice Kwamba Unataka Uwalipe Na Uwe Discharged From The Loan Agreement,Waambie Wasipokubali Utaenda Mahakamani Kwa Sababu Wanavunja Terms Za Huo Mkataba Wenu.... Wasipokubali Unaenda Kufungua Kesi Unaiomba Mahakama Itoe Order Ya Specific Perfomance Ili Wewe Uwalipe Hela Yao Kama Mkataba Unavyosema!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom