Mbunifu Mwaminifu
Member
- Dec 13, 2012
- 67
- 352
Habari zenu wanajamvi.
Naulizia ili kufahamu kwa niaba ya rafiki yangu.
Rafiki yangu alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni fulani hapa jijini Dar es Salaam na alikuwa akifanya kazi na hiyo kampuni kwa takriban miaka mitano.
Kwa kawaida kampuni ambayo alikuwa akifanya nayo kazi ilikuwa inawapatia wafanyakazi mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Yani kama mfanyakazi ametumikia kampuni kwa miaka kumi, maana yake ni kwamba mfanyakazi huyo amesaini mikataba kumi katika kipindi hicho.
Kwa mwaka 2020 (kabla mripuko wa COVID-19), kampuni iliwapatia wafanyakazi mkataba wa miaka miwili kila mfanyakazi, ila kutokana na hofu ya mripuko wa COVID-19 kampuni iliamua kuwapa baadhi ya wafanyakazi likizo ya mwezi mmoja (Annual leave) ili kupunguza msongamano wa wafanyakazi ofisini hapo.
Bila kutarajia, baada ya wafanyakazi kumaliza likizo, kampuni ikaamua kuwaitisha kikao baadhi ya wafanyakazi wao na kuwapatia barua za kusitisha mikataba yao huku wakiwalipa mshahara wa mwezi mmoja baada ya mwezi wa kusitisha mikataba yao. Yani kama mfanyakazi alikwenda likizo kuanzia Tarehe 1 Aprili na kuripoti kazini tarehe 29 Mei, alilipwa mshahara wake wa mwezi Aprili (ambao alikuwa likizo, kisha baada ya kupatiwa taarifa ya kusitishwa kwa mkataba wake alipatiwa mshahara wa mwezi Mei).
Naomba msaada, je hapo mfanyakazi hawezi kisheria kudai malipo ya mkataba wake kuwa terminated bila ya kupatiwa notice?
Na kama alipatiwa mshahara wa mwezi mmoja zaidi, ni halali kuvunjwa kwa mkataba wa kazi bila kupatiwa notice?