Nahitaji msaada wa kiafya wa tatizo hili la kuwashwa

vampire123

JF-Expert Member
Apr 17, 2016
1,176
2,000
Habari zenu wakuu,

Naombeni msaada wa kiafya, mwezi wa 8 nilikumbwa na ugonjwa wa kuwashwa ambapo nilianza kuwashwa mikononi nilivyokuwa najikuna nilikuwa natoka na vipele nikaenda hospitali nikapimwa nikaambiwa ni allegy na kupewa dawa nitumie. Nilimaliza dozi ila sikuweza kupona mpaka ilifika hatua muwashwo ulisambaa hadi sehemu za siri(uume) ambapo usiku ulipokuwa unaingia nilikuwa nashindwa hadi kulala nilikuwa nawashwa muda wote nikijikuna kunatokea vipele vikubwa sana na kwenye eneo la kichwa cha uume kulikuwa kuna mchubuko kidogo ambao ulikuwa unatoa damu kidogo sana baadae baada ya kushauriwa na watu mbalimbali nikatumia dawa inaitwa BBE kwa kweli ilinisaidia sana lakini tatizo likabaki kwenye sehemu za siri muwashwo bado unaendelea lakini kwa namna ndogo mno na sehemu ya kichwa cha uume ni pekundu alafu kama kunanyauka namna fulani. NAOMBENI MSAADA WENU WAKUU ILI NIWEZE KUPONA

NB: Inasemekana ulikuwa ugonjwa wa mlipuko.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,606
2,000
Kuwashwa washwa kwako kunatokana na chanzo cha ini lako halipo sawa kiafya. Ndio maana una washwa washwa na huponi jaribu kulisafisha hilo ini lako utapona maradhi yako.

Ushauri wangu kwenye uume wako jipakae mafuta ya nazi kwa siku pakaa mara 3 asubuhi mchana na usiku, kuhusu kusafisha ini chemsha maji ya moto kisha kamulia limao koroga vizuri kisha kunywa asubuhi kabla ya kula kitu. Na pia ule punje 2 za Kitunguu saumu pamoja.

Kisha kaa kwa muda wa saa moja pasipo na kula kitu. Baada ya saa moja kupita waweza kula chakula cha asubuhi na mchana fanya hivyo na usiku fanya hivyo. Tumia hizo dawa kwa muda wa siku 7 kisha njoo ulete mrejesho wako hapa.

Vitu vya kujiepushe wakati unapo tumia hizo dawa >Usinywe pombe ,usivute sigara,usinywe soda ya aina yoyote ile na pia usile nyama ya aina yoyote kw muda wa siku 7 . Uguwa pole
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom