Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Ok mi niliwahi tokewa na hali hiyo nikiwa njombe miaka hiyo.

Tiba yake ni PILITON meza kidonge kimoja tu hali hiyo inapokutokea. Ukitumia kama siku 3 hivi basi haitatokea tena maishan mwako.
Pia jaribu kuepuka kuoga maji ya baridi weka vuguvugu na uoge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama bada hujapona.

Unapata vipele kwenye kiwiko(kipepsi)? Luna vipele vidogovidogo vidoleni? Unawashwa Sana usiku ukilala? Unasikia vitu kama vinakutembea mwilini? Kuna saa unawashwa kiunoni?

Kama unapata his dalili nijibu nikuelekeze dawa pharmacy.. Zinauzwaga 8,000 -10,0000( elf nane hadi kumi)
Ndioo
 
Kama bada hujapona.

Unapata vipele kwenye kiwiko(kipepsi)? Luna vipele vidogovidogo vidoleni? Unawashwa Sana usiku ukilala? Unasikia vitu kama vinakutembea mwilini? Kuna saa unawashwa kiunoni?

Kama unapata his dalili nijibu nikuelekeze dawa pharmacy.. Zinauzwaga 8,000 -10,0000( elf nane hadi kumi)
Mkuu nitajie hiyo dawa nami nina hilo tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mtaalamu wa afya lakini nikiri kwamba watu wengi walio vijana au wasio na ugonjwa serious hawafuatilii kujua impacts au athari za vitu au vyakula tunavyokula na athari za kuacha kula vyakula tiba hii hupelekea matatizo mengi ikiwemo miwasho mwilini na maumivi ya viungo yasiyoeleweka na kuhangaika kila hospitali au kupewa dawa mbalimbali. Kukabiliana na tatizo la muwasho au maumivu yasiyoeleweka napendekeza njia tatu kuu

i. Kwanza tuchunguze vitu vya usafi na hali ya hewa vinavyotuletea tatizo la kuwashwa, badili kimoja baada ya kingine ili ujue kipi kinakusumbua, mfano aina ya maji ya kuoga, joto la maji ya kuoga,sabuni ya kuogea, dawa ya meno, athari za vumbi, hali ya hewa baridi(huleta muwasho kwa baadhi ya watu) n.k. Kwa kifupi jichunguze unaweza kuondoa tatizo kubwa pengine kwa kubadili kitu kimoja tuu kati ya nilovyovitaja.

ii. Tusisubiri mpaka uambiwe una kisukari au presure ndio tupunguze vyakula vya wanga,red meat au vilivyosindikwa badala yake tuongeze kula matunda,mboga mboga,white meat,nuts na maji kwa wingi.Ndugu zangu wanga na vyakula vilivyosindikwa haviwazuru wenye kisukari tuu lakini pia ni chanzo cha matatizo mengi sana ikiwamo too much acid, maumivu,miwasho,vitu kutembea mwilini,ukosefu wanguvu za kiume,wanga ni breeding ground of most diseases, ukijua undani wake utasema kwanini ulichelewa kujua, yaani ata mwili au viungo kuwa na mafuta mengi inawaza kuwa matokeo ya wanga converted to fats.Yaani nakuhakikishia ukifuata hii utaondoa matatizo mengi na kurejesha furaha ya maisha.

iii. Tule vyakula tiba kutibu na kujikinga na matatizo mengi kila siku. Jamani kuna vitu ata havigharimu, mfano ukijiwekea kila siku unywe chai ya tangawizi,au green tea au limao kwa asali nakuhakikishia utatibu na kujikinga na maradhi mengi saana pia unaweza kutumia vitunguu saumu au vya kawaida, nuts mbali mbali (e.g peanuts,wallnuts.) .Wakuu kwa ujumla vyakula tiba ni spices,nuts,vegetables au fruits.

Ukifuata ushauri huu unaweza kubadilisha kabisa maisha yako.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu nna ndugu yangu analalamika anatatizo la kuwashwa kama vinyweleo vikipigwa upepo anahisi kama katembelewa na kitu hilo ni tataizo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la kuwashwa baada ya kuoga wengi huwa wanawashwa wakioga maji ya baridi (sijajua uhusiano wake kitaalamu) ila ili kuzuia Hali hii inabidi ujipake mafuta pindi tukirudi utokapo kuoga usichukue muda mrefu nikalia kujipaka mafuta...... Pia usafi wa Taylor na nguo za kujikausha ni muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari JF Doctor na wana jamii wote.

Mdogo wangu wa kiume (23yrs) ana tatizo la kuwashwa mwili mzima tokea mwaka 2002. Nimezunguka naye takribani hospitali zote kubwa hapa Dar lakini hatujafanikiwa kupata ufumbuzi wa tatizo lake.

Kwa ufupi ni kwamba alianza tu kuwashwa jichoni, macho yakavimba, akaenda hospital (Burhani) akapatiwa dawa za kutuliza allergy (cetrizine) ile hali ikatulia kwa siku mbili tu, ya tatu mwasho ukarudi tena.

Tukaenda Aga Khan akapimwa kuanzia choo, mkojo, damu lakini hakukutwa na minyoo, wala gonjwa lolote la zinaa akapewa tena cetrizine na ndizo anaendelea nazo mpaka leo kutumia, miaka nane sasa ule mwasho bado upo.

Akijikuna pale panapowasha panavimba mithili ya mdudu amekukojolea au mithili ya mtu aliyewashwa na washawasha, na ni mwili mzima unakuwa unawasha, mpaka anywe cetrizine ndo muwasho unatulia, hii dawa hutuliza kwa km siku nne tu baada ya hapo muwasho pale pale. Alishameza dozi za fungus kama mara nne hivi kwa siku kumi na tano lkn tatizo bado lipo pale pale.

Hofu yangu ni kuwa hizi cetrizine zinaweza zikamletea madhara in a long run. Sasa daktari saidia hapo yawezekana ni nini sababu ya huu ugonjwa?
=====
WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI:


===

===

===


===



===


===


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:

===


===


===


===


===


===


===


===


===


===
Kumbe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za jioni wapendwa. Polen na kazi.

Mimi nasumbuliwa na maradhi ya kuwashwa mapajani na sehemu nyingine za mwili kama miguuni, tumboni, kifuani, kwapani, mgongoni na makalioni.

Tatizo hili limeanza muda mrefu na nimeshaenda vituo mbalimbali vya afya lakini bado sijapata tiba stahiki ya kutibu ugonjwa huu.

Nakumbuka mara ya mwisho nilienda hospitali ya Kisarawe daktari akaniandikia kipimo cha HIV, VDRL na kipimo cha kupima mchafuko wa damu lakini sikukutwa na magonjwa ya vpimo nilivyiandikiwa na daktari.

Mwisho, daktari aliniambia kuwa pengine naweza kuwa na allergy ya kitu ambacho sikukitambua, basi akaniandikia dawa na sindano lakini kwakweli hazikusaidia hata kidogo.

Baada ya hapo nikashauriwa kutumia dawa ya fangasi na niliambiwa pengine fangasi iliingia mpaka kwenye damu. Nilitumia dawa fulani inaitwa gresiofulvin kama sikosei ambayo dose yake ni vidonge 30 lakini pia haikusaidia.

Baadae nilitumia dawa ambayo ilikuwa ni anti-bacteria lakini nayo pia ilidunda; nikatumia dawa ya minyoo pia nayo ikadunda daah.

Yaani nimetumia dawa nyingi lakini kwakweli sijapata relief so nilikuwa naomba ushauri wenu jamani, yaani nateseka mnoo. Usiku silali nahangaika tu kujikuna mpaka asubuhi.

Halaf ikifika asubuhi vinaacha kuwasha pale itakapogonga mishale ya saa moja tu jioni, vurugu znaanza tena. Yaani hapo ni kukesha tu mpaka asubuhi.

Msaada wa ushauri na mawazo. Please, ndugu zangu.
 
Nitakuhoji mambo kadhaa, univumilie.

Tatizo limeanza lini?
Muda mrefu sio muda maalumu, nitajie miezi kadhaa au miaka kadhaa.
 
Back
Top Bottom