Nahitaji msaada wa haraka kabla stress haijapanga chumba moyoni mwangu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
Mwanadamu asipotumika katika Mema basi atatumika katika Mabaya, asipomtumikia Mungu atatumikishwa na Shetani, usiposababisha makwazo utasababishiwa,

Nifanyeje ili niweze kusamehe watu wanaonikosea kwa haraka bila kuumia kila siku kwa kukumbuka ubaya wanaonifanyia hasa wale ambao wananikwaza sana kila wakati au kila siku?

Napata wakati mgumu sana jamani naombeni msaada wa namna yoyote ile ambayo naweza kuitumia ili moyo wangu usifadhaike.
 
Jaribu kujiweka mbali nao, kama ni ngumu kuwa nao mbali basi jijengee tabia ya kuwazoea, yani ukishamjua mtu tabia zake hawezi kukukwaza.

Hali ikizidi kuwa mbaya nenda hospital upate msaada wa kitaalam
 
Jitahidi kujiweka mbali na watu au mazungumzo yanayosabisha usononeke!

Halafu tafuta shughuli ambayo huwa inakupa furaha kama kusikiliza muziki, kama mpenz wa movie angalia au Hata kwenda sehemu tulivu ( kupata vinywaji kama soda , beer etc)
 
Nguvu ya msamaha inaonekana pale unapoweza kusamehe bila kuombwa msamaha au wakati mwingine hata aliekukosea hajui kama alikukosea... wewe kumsamehe aliekukosea ni kwaajili yako wewe mwenyewe. Ukisamehe unalinda amani yako ya moyo ambayo ni kitu muhimu...
 
Mwanadamu asipotumika katika Mema basi atatumika katika Mabaya, asipomtumikia Mungu atatumikishwa na Shetani, usiposababisha makwazo utasababishiwa,

Nifanyeje ili niweze kusamehe watu wanaonikosea kwa haraka bila kuumia kila siku kwa kukumbuka ubaya wanaonifanyia hasa wale ambao wananikwaza sana kila wakati au kila siku? Napata wakati mgumu sana jamani naombeni msaada wa namna yoyote ile ambayo naweza kuitumia ili moyo wangu usifadhaike.
Pole sana.
Jitahidi kuto kupata taarifa yoyote kutoka kwa hao wanaokusababishia maumivu kwani ni kuwasamehe na kuwakataa kihisia.
Usipende mazoea nao hata kama Mkaa mtaa mmoja usiwape nafasi yoyote ya kukuelewa nini malengo yako au unampango gani juu ya walichokufanyia.
Usiache kuwasalimia kwani wewe kuwasalimia watabaki anateseka Moyoni bila wewe kujua.
Fanya mambo mema kwao ili kuwaumiza zaidi.
Kama una bibilia Soma Zaburi 140
 
Hakuna kilevi utakachotumia kikakuondolea mawazo big no, unachotakiwa kufanya ni kumchukulia mtu jinsi alivyo na chukulia hayo makwazo kama sehemu ya mapungufu yake utaweza kudeal na kila aina ya mtu.

Kila binadamu ana mbaya na makwazo yake, sasa usipojifunza kusamehe utaweza kuwabeba wangapi ktk moyo wako??

Jifunze kuachilia moyo la sivyo utajitafutia matatizo kama pressure, kisukar na hata kukosa mwili. Mkuu nakushauri tu samehe kama imani ya dini yako inavyokuelekeza!
 
Mwanadamu asipotumika katika Mema basi atatumika katika Mabaya, asipomtumikia Mungu atatumikishwa na Shetani, usiposababisha makwazo utasababishiwa,

Nifanyeje ili niweze kusamehe watu wanaonikosea kwa haraka bila kuumia kila siku kwa kukumbuka ubaya wanaonifanyia hasa wale ambao wananikwaza sana kila wakati au kila siku? Napata wakati mgumu sana jamani naombeni msaada wa namna yoyote ile ambayo naweza kuitumia ili moyo wangu usifadhaike.


Ndugu yako akikukosea
1. Mweleze alitambue kosa lake na atubu na kuomba msamaha. Usipofanya hivyo hata wewe una makosa.

2. Asipotubu lieleze kanisa limuonye.

Akitubu Msamehe.
Asipotubu baada ya hatua hizo, dhambi yake haiko juu yako.
 
Pole sana ila ndio tulivyo wanadamu.

Ushauri wangu uchague moja ya vtu vifuatavyo kuondokana na the so called 'stress'

1. Sex sanaa!!, ikiwezekana kwa wiki mara 4/5

2. Jichanganye san club hasa kweny mziki

3. Tumia angalau chupa 3 za castle lite kwa wiki mara 4/5

4. Angalia sana katuni hasa animations aisee huta amini vile utakuwa una relax

5. Cheza sana video games 'PS'

NB: Hizo njia apo juu tumia moja wapo tu!, usichanganye mbili au tatu au zote kwa mpigo utaishia kujivuruga zaidi.

Na usisahau too much is harmful.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom