Nahitaji mnunuzi wa mitiki(Teak wood)

kindege534

Member
Jul 28, 2014
97
22
Imekomaa, ina 20years of age, urefu ni zaidi ya futi 20, ina average diameter ya 14cm. Ekari 16.
Shamba lipo korogwe Tanga Tanzania. Nataka mtu atakaenunulia moja kwa moja shambani.
Pia naomba mnishauri pa kuwapata hao wanaohitaji. Shukrani.
Picha hii ni eneo mojawapo la shamba
 
Attachments

  • 2014-08-05 13.23.14.jpg
    2014-08-05 13.23.14.jpg
    456.3 KB · Views: 701
Nenda Amani, Handeni Tanga. Wapo wanunuzi wengi wa mitiki wamenunua miti kwenye misitu ya serikali na wamejenga sawmill za kupasua mbao na zote zinapelekwa nje ya nchi.
 
Nenda Amani, Handeni Tanga. Wapo wanunuzi wengi wa mitiki wamenunua miti kwenye misitu ya serikali na wamejenga sawmill za kupasua mbao na zo te zinapelekwa nje ya nchi.
Asante ndugu Majimoto, nitakwenda huko. Unafahamu jina la hicho kiwanda?
 
Last edited by a moderator:

Vipo vingi vya wachina wahindi... majina yao sivijui, ukipanda daladala zinazoenda Amani milimani mwambie kondakita akushushe kwenye viwanda vya mbao, ingia ndani ufanye biashara... ukifanikiwa usisahamu mirinda baridi....
 
Hahahhah.....umenifurahisha hapo! Na kweli ntafanya hivyo..hahahhah
 
Ndugu Majimoto nimekwenda kijiji cha Amani kama ulivyoniagizia. Ila amani ipo Muheza na sio handeni. Na ni kweli kuna viwanda vingi vya teak. Ila vimeachana umbali wa kilomita kama tatu nne. So unatembea kutoka kiwanda kimoja hadi kingine.
Nimejifunza mengi huko: nimesikitishwa na familia maskini za wakazi wa amani, hawana nyumba bora wakati kwny kijiji chao kuna estate ya Mitiki na viwanda.
Nimefanikiwa pia kukutana na wafanyabiashara ya teak, ila kule viwanda vingi ni branch za viwanda vya huku dar. Nipo kwny mchakato
 
Samahani kwa kujichanganya, ni kweli Amani ipo Muheza, pole kwa usumbufu.
 
Vipi ile mirinda baridi alikutumia Mpwa tugawane japo kizibo tu? hii project ni bab kubwa, inalipa sana sana hio miti ni ghali sana nashangaa kwanini Mpwa wangu hadi atafute soko wakati "naskia" ukiwa nayo hio wanakutafuta wenyewe.
 
Wahindi wa kule wamenipa ahadi hewa tu. Mkuu Majimoto mpaka leo hawajachukua. Sijui cash imekua ndefu sana au nin! Kama unafahamu pengine ni PM nitakwenda. Soda yako ya nguvu na ya maana iko palepale ntakukatia
 
Last edited by a moderator:
Wahindi wa kule wamenipa ahadi hewa tu. Mkuu Majimoto mpaka leo hawajachukua. Sijui cash imekua ndefu sana au nin! Kama unafahamu pengine ni PM nitakwenda. Soda yako ya nguvu na ya maana iko palepale ntakukatia

Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) imetoa idhini kwa waombaji wafuatao kuweza kupata mgao wa miti katika baadhi ya mashamba ambayo yanamilikiwa na wakala kwa mwaka 2014/2015

Orodha ifuatayo ni wafanyabiashara walioruhusiwa kuvuna miti kwenye msitu wa Shume, jaribu kuwasiliana nao Mkuu

http://www.tfs.go.tz/uploads/SHUME.pdf
 
Nashkuru mheshimiwa..nimejaribu kuwatafuta baadhi yao kwa njia ya posta sijajibiwa mpaka sasa
Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) imetoa idhini kwa waombaji wafuatao kuweza kupata mgao wa miti katika baadhi ya mashamba ambayo yanamilikiwa na wakala kwa mwaka 2014/2015

Orodha ifuatayo ni wafanyabiashara walioruhusiwa kuvuna miti kwenye msitu wa Shume, jaribu kuwasiliana nao Mkuu

http://www.tfs.go.tz/uploads/SHUME.pdf
 
kindege534, Jaribukumtafuta mke wa raisi wa awamu ya nne, kuna kipindi alinunua maeneo ya Rufiji huko kijiji sikijui, alihamasisha sana upandaji wa hiyo mitiki kipindi aliponunua, kila la heri, vinginevyo kwa nini usiuze kwa reja reja ukatuuzia akina sie, mie nna milioni tatu ntapata mingapi?
 
Back
Top Bottom