Nahitaji mnitie nguvu

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Kipindi hiki cha Corona kinazidi kunipa mawazo ya kukata tamaa ya kusoma na kuona tutazidi kuchelewa kumaliza nimekuwa ni mtu wa kulala tu na kuamka na kuwa na mawazo yasiyoisha 24 hrs kuhusu kusoma kwangu mbona naona kama mambo yangu hayaendi nimekuwa ni mtu wa huzuni tu naona kama kila mtu ananiangalia mimi mana niliacha kazi na kwenda kusoma saizi nakosa hata ela ya vocha jamani najiona tofauti tu na binadam wengine jamani kuna baadh ya watu nawakimbia naona aibu kuonana nao.
 
Usije ukafikiria kujiuwa tu kila kitu ni champito na changamoto za maisha kila mtu anazo kipindi hiki unatakiwa kuwa mvumilivu tu.
 
Mkuu hauko peke yako.
Mimi ni kama wewe tu mambo yote yamesimama.
Mwaka huu nilikuwa na malengo kibao ila naona yote yatafeli.
Niko hapa asubuhi nimeamka nimekunywa uji nimerudi kitandani, nimeamka nimekula tena wali kidogo nimerudi kitandani. Navuta vuta mda hapa nisonge ugali nile.
Maisha yanaboa sana ni kula na kulala na kuchangia thread zote za jf.
Muhimu sana kipindi hiki kutokukosa bundle.
 
Mkuu punguza presha chukulia kawaida kwan kipindi hichi kila MTU analia, sema wengine ni majasiri hawataki kuonyesha matatizo yao hadharani Ila kiukwel hali ni mbaya
 
Mkuu hauko peke yako.
Mimi ni kama wewe tu mambo yote yamesimama.
Mwaka huu nilikuwa na malengo kibao ila naona yote yatafeli.
Niko hapa asubuhi nimeamka nimekunywa uji nimerudi kitandani, nimeamka nimekula tena wali kidogo nimerudi kitandani. Navuta vuta mda hapa nisonge ugali nile.
Maisha yanaboa sana ni kula na kulala na kuchangia thread zote za jf.
Muhimu sana kipindi hiki kutokukosa bundle.
Haaahh mkuu umenchekesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza pole sana mkuu,nimeona nianzie huku japo nimeona pia uzi wako mama!!

Nachotaka kushauri mkuuu ni kama ifuatavyo,

Moja ya side effect ya lockdown ndio hii,wapo wengi wanaopatwa na shida kama hizi mkuu ila goja nijikite kwako

_ kwa kipindi hiki nakushauri sana ujiepushe kukaa peke yako, kama ikiwezekana naomba (kama ni mpenzi wa kusikiliza nyimbo) sikiliza ukiwa peke yako chumbani au popote,hii itakufanya u relax na kusahau hili.

_pili fanya mazoezi, kimbia ukiwa unachukua tahadhari za corona, unaweza ukawa una tune hata ka muziki kidogo then automatically you will start forgetting this!

_ ongea na wanafunzi wenzako,mbadilishe mawazo wao wanafanya nini kipindi hiki wawapo nyumbani, kufanya vile utajikuta unaona kitu cha kawaida

Kingine kikubwa mkuu punguza kuwaza kuhusu mtihani, hebu kabla hujawaza vile fikiria ni wangapi wamekumbwa na hili tatizo? Je uko peke yako? Hivyo chukulia ni janga la kidunia kikubwa tuzido kuomba kwani ni wengi wamekutana na shida hizi pengine yako ni ndogo!! Labda ni kupe mkasa mmoja though it's not so good to share it here in!!

Kuna mama mmoja anafanya kazi kiwanda fulani stakitaja,alinipigia simu anauliza kama serikali watafunga yaani tutawekwa lockdown, yule mama anasema ndani hana chakula,kodi ya nyumba imeisha,mtoto wake ambaye ni mwanafunzi anazurura hovyo,mama yake mzazi anaumwa sana,then nikampa pole akaniambia ameamua kufunga na kusali ili Rais asifunge yaani kuwekwa lockdown maana hajui ataishije!!!

I was shocked kusikia vile lakini kiukweli yule mama alikuwa analia nikaelewa kiukwel watu wanapitia magumu, coming to the main point, shukuru sana ndg hata kwa hatua hiyo uliyofikia then sali kwani Mungu atatusikia, ni wengi wenye shida ndg!!

MTANGULIZE MOLA WAKO, EPUKA KUSIKIA HABARI MBAYA HASA ZA CORONA IKIWEZEKANA USIFUATILIE TAARIFA KAMA HIZO KWANI ZITAKUONGEZEA STRESS NDG!! MUNGU YU PAMOJA NASI,ATATUVUSHA!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hauko peke yako.
Mimi ni kama wewe tu mambo yote yamesimama.
Mwaka huu nilikuwa na malengo kibao ila naona yote yatafeli.
Niko hapa asubuhi nimeamka nimekunywa uji nimerudi kitandani, nimeamka nimekula tena wali kidogo nimerudi kitandani. Navuta vuta mda hapa nisonge ugali nile.
Maisha yanaboa sana ni kula na kulala na kuchangia thread zote za jf.
Muhimu sana kipindi hiki kutokukosa bundle.
Aises pole sana mkuu!
Hauna back up plan usikae idle kiasi hicho
 
Back
Top Bottom