nahitaji mkopo wa tiles!!

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,569
13,376
wakuu,nimekwama kumalizia kakibanda kangu ili nihame kwa mama mwenye nyumba!!tatizo ni wapi ninaweza kukopa tiles na kulipia kidogokidogo nimalizie hii ishu yangu!!

wasalaam
 
Kwanini usihamie tu then tiles uweke baadae utakapokuwa tayari?

ni kweli nafikilia kufanya hivyo!!lakini nilikuwa nataka hata kidogo za ******!!si unajua tena waswahili wanasema uzuri wa nyumba choo ndugu yangu!!
 
Jaribu pale clock tower kama una kadi ya gari wanaweza kukuelekeza kwa wanaokopesha kwa riba kisha ukapata hiyo tile, ila mie nakushauri ukakae hivyohivyo tu
 
Jaribu pale clock tower kama una kadi ya gari wanaweza kukuelekeza kwa wanaokopesha kwa riba kisha ukapata hiyo tile, ila mie nakushauri ukakae hivyohivyo tu
Ahsante mama Joe!
kadi ya gari sina,nilitaka watu tutakao elewana nao kwa kupafahamu ninapojenga na kuandikishana kwa serikali za mitaa!

ila hilo wazo la kuhamia hivyo hivyo nalipokea!nitahamia hivyo kwani kwako ni kwako,nilikuwa tu natafuta alternative lakini kama haitapatikana nahamia kwani kwa mama mwenye nyumba nini siku 30 za kujidai!
 
kama ni mfanyakazi wa Serikali nenda pale tunakopesha, au kama mwajili wako atakuwa tayari kukudhamini,
unajua hilo la kuweka nyumba au gari mara nyingi kisheria linawashinda wenye maduka na hata wenye idara zingine za mikopo (kama Tunakopesha), hawa ni tofauti sana na benki, kwa sababu mabenki hiyo ndio kazi yao ya kukopesha na kuweka dhamana, sasa hata tunakopesha wamesajiliwa lakini hawana mamlaka ya kushika property ya mtu, na hata kama akishika hiyo property basi atakuwa yupo nje ya sheria (Haya maelezo niliyapata pale Tunakopesha),. Tunakopesha mwanzo walianza kuchukua property kama dhamana na mpaka sasa wana blue book na hati za nyumba nyingi tu lakini hawana mamlaka nazo kwa sababu kisheria hawakusajiliwa kukopesha kwa dhamana ya property, nadhani ni same case na wenye maduka, kwa hiyo jaribu kupita kwenye maduka na kuongea nao wewe kama wewe na kuwekeana makubaliano baina yenu
 
huyu jamaaa bana yeye anasema tiles mimi nilifikiri milango bana, tiles utaweka na hiyo pesa ya kodi utakapohama......shtuka chukua hatua
 
huyu jamaaa bana yeye anasema tiles mimi nilifikiri milango bana, tiles utaweka na hiyo pesa ya kodi utakapohama......shtuka chukua hatua

Hamia tu hivyo hivyo, si unajua tena ukichelewa lazima umlipe mwenye nyumba, sasa hizo za mwenye nyumba utazitoa wapi? Nyumba Choo bwana sio Tiles.
 
wakuu,nimekwama kumalizia kakibanda kangu ili nihame kwa mama mwenye nyumba!!tatizo ni wapi ninaweza kukopa tiles na kulipia kidogokidogo nimalizie hii ishu yangu!!

wasalaam

ukweli ni kuwa watanzania hatuaminiki,huwezi pata mkopo wa tiles kwani wafanyabiashara hawataki kudai,
ushauri nenda katika duka ulilokuwa unanua vifaa vyote vya ujenzi,anaweza kukukopesha kufuatana na kiwango cha manunuzi uliyokuwa ukifanya,

Je hiyo nyumba ipo sehemu gani? naweza kukushauri zaidi
 
wakuu,nimekwama kumalizia kakibanda kangu ili nihame kwa mama mwenye nyumba!!tatizo ni wapi ninaweza kukopa tiles na kulipia kidogokidogo nimalizie hii ishu yangu!!

wasalaam

Kama upo Arusha nenda Masua Interprises wanakopesha hapo
 
Zamaulid zama ndani wewe. Kama umeweka milango, madirisha, nyavu za mbu, choma ndani mwanagu(hongera), nakshi baadaye wewe....marumaru, ceiling board/gypsum nk baadaye wakati ume-enjoy privacy kwako...kupanga utumwa jamani...hasa kule kwetu kwa mama mwenye nyumba...karaha tupu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom