Nahitaji Mjamzito anipatie au nipate Mtoto (Kiume au Kike) ili nimlee mtoto kama wangu

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Nina uhitaji wa mtoto, sasa endapo atakuwepo mdada ambaye ni mjamzito miezi 5-8 nahitaji akizaa mtoto awe wakwangu anikabidhi basi tuwe tumemalizana nitamlea mwenyewe kwa vyovyote vile na nitamuingiza kwenye ukoo wangu. nafahamu kuna vituo vya kulelea yatima ila sihitaji huko mbali sana na process za kurithi ni ngumu sana.

Huu ni kama msaada kwa mama mjamzito kama atakuwa ni mtu ambaye labda hakupanga kuzaa ila imetokea na hayuko tayari kuwa na huyo mtoto.

cc Equation x

Au

Kusema ukweli nahitaji mtoto wa kike au wa kiume umri kuanza mwezi 1 hadi miezi 6, tatizo nililo nalo siwezi kulizungumzia hapa, ila naomba msaada namna ya kumpata, nafahamu vipo vituo vya watoto yatima, sitaki kwenda huko nahitaji nampataje sitaki process zote za serikali za kurithi maana zina mlolongo mkubwa. Je kuna uwezekano wa kumpata kwa namna gani,

Niombe nisiulizwe swali kama HUNA KIZAZI UZAE, MTAFUTA MKE UZAE NAYE.
 
Kusema ukweli nahitaji mtoto wa kike au wa kiume umri kuanza mwezi 1 hadi miezi 6, tatizo nililo nalo siwezi kulizungumzia hapa, ila naomba msaada namna ya kumpata, nafahamu vipo vituo vya watoto yatima, sitaki kwenda huko nahitaji nampataje sitaki process zote za serikali za kurithi maana zina mlolongo mkubwa. Je kuna uwezekano wa kumpata kwa namna gani,

Niombe nisiulizwe swali kama HUNA KIZAZI UZAE, MTAFUTA MKE UZAE NAYE...
Mtoto wa miezi hiyo si itabidi umhudumie akiwa kwa mama yake mzazi kwanza kisha umchukue akiacha kunyonya? Pia utamlea wewe mwenyewe au una mwenzi wa kukusaidia?

Kwa kifupi Tz hii ni hela tu ndio inaongea. Unatafuta binti, kisha mwambie unahitaji mtoto. Mwambie unataka kumlea wewe amzae na mtu yeyote. Kisha akiacha kunyonya anakupatia. Inabidi umwambie hela gani utampa. Pia tafuta. mwana sheria (advocate) akusaidie ili usidanganywe. Na pia ili ujue kama sheris zinaruhusu kufanya hivyo.
 
Sasa kama unaogopa mlolongo jinsi ya kumpata kupitia orphanage je kwa njia unayotaka wewe unadhani haitakuwa na mlolongo..?

Fuata mlolongo mzima ili upate kumlea kisheria pasipo mizengwe wala matatizo yatakayokuletea shida badae.

Otherwise Kama una mambo yako mengine nyuma ya pazia.
Agenda ya siri😊
 
Naam Mkuu...
Ila Serikali imeweka UTARATIBU wa kufuata ili kukulinda,kumlinda mtoto,wazazi wake ama walezi.

Achana na Mambo ya kienyeji,fuata sheria...

Mtoto ni Mali ya Serikali mpaka miaka 18,Sembuse huyo anayeendelea kutakiwa KLINIKI mpaka miaka 5?!!!

Nakutakia kila la heri katika kufuata njia hizo salama!!
 
Mtoto wa miezi hiyo si itabidi umhudumie akiwa kwa mama yake mzazi kwanza kisha umchukue akiacha kunyonya? Pia utamlea wewe mwenyewe au una mwenzi wa kukusaidia?
Yote sawa, akiacha kunyonya namchukua nimpe mama yangu kwanza akikua kabisa ndio ntakaa naye na housegirl
 
Kwa hapa ni ngumu sana mkuu. Kwa ushauri tu, angalia kwa ndugu zako wa damu itakuwa raisi kupata.
 
Kama unapesa hii inshu rahis sana,maana sku hz wanawake wanazaa hovyo hovyo kama mifugo,andaa million mpe singo mama Mdogo ambae itabid umsafirishe umuweke mbali na kwao umtunze hata KWA miaka 3 baadae ndo muachane
 
Yote sawa, akiacha kunyonya namchukua nimpe mama yangu kwanza akikua kabisa ndio ntakaa naye na housegirl
Tz ni pesa tu. Mimi binafsi kuna wadada wengi sana wanataka kuzaa na mimi sababu wanajua nina $$ na nitawahudumia. Sasa hapo fanya tu hivyo. Tumia $$ yako ikusaidie. Kama una tatizo la fertility, ongea tu na msichana au chagua pia mwanaume mwenye mbegu nzuri akusaidie kwa hilo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom