Kwa muda mrefu, kumekuwepo na hoja kutoka kwa baadhi ya watu kuwa dini tunazozifuata ni matokeo ya kuletwa na meli, na hivyo wanadai kuwa kuzifuata ni sawa na kuwa mtumwa kwa waliozileta. Nina maswali kidogo kwa watu wanaodai hivyo. Na bila shaka wanapotoa madai hayo, wanatoa kutokana na kwamba ni watu wenye elimu, walioelimishwa vizuri darasani, sasa
1. Je, elimu tunayotumia hapa Tanzania, yenyewe haikuletwa kwa meli? Na je, lengo lake nayo haikuwa kulahisisha utawala kwa wakoloni kama wanavyodai kuwa dini zilikuwa chambo cha kurahisisha utawala wa kikoloni?.
2. Nguo tunazotumia, je kwa mara ya kwanza zilivumbuliwa Afrika? Je, kabla ya wenye meli kuja, hatukuwa na mavazi yetu? Mbona hata leo hii kuna baadhi ya nguo kama vile suti zinaagizwa hukohuko kwa waliotuletea dini kwa meli?.
3. Wale wanaodai kuwa Mungu hayupo(Atheists), je ni watanzania ndio walioibua hoja za kuwa Mungu hayupo? Au nadharia za kuwa Mungu hayupo nazo chanzo chake sio kwa waliotuletea dini kwa meli?.
4. Simu, kompyuta, gari na teknolojia nyingine nyingi, zenyewe zilianzishwa hapa Afrika? Au na zenyewe zililetwa kwa meli?.
5. Yapo mambo mengine mengi tunayoyafuata na chanzo chake ni ulaya, mfano mpira, n.k
Je, kuyafuata hayo nayo ni utumwa kama wanavyodai kuwa kufuata dini ni utumwa tulioachiwa na wazungu? Kwa nini kama hatutaki mambo yaliyoletwa na wazungu, tusiwe na mambo yetu wenyewe yaliyo tofauti na wao. Nawasilisha hoja.