Nahitaji maelezo kuhusu pampu ya maji ya ardhini

fixit KEM

Member
Oct 26, 2014
89
63
Habari wadau,

Nimeamua kujiajiri katika kilimo cha mboga mboga, lakini napata changamoto ya maji.

Naomba mwenye uelewa na hizi pumpu za maji za ardhini anipe mwanga wa gharama ya pump na pia ina uwezo gani, pia ina tumia pipe ya inchi ngapi.....
NB: Chanzo changu cha umeme ni generator

Ahsanteni
 
Habari yako mkuu, swali lako halijajitosheleza bado. Utaratibu huanzia na watalaama watakaokuja kupima maji shambani kwako.

2. Baada ya kupima watakupa majibu kina cha maji , utafata uchimbaji kutokana na kina ulichoambiwa, wakishamaliza kuchimba utasafisha kisima na kufanya pump test, zoezi hili ni muhimu sana sababu ndio swali lako litakapojibiwa, sababu pump test ikifanyika ndio utaweza kujua kwa saa moja kisima chako kinaweza kuvia maji kiasi gani ili tuweze kupata jibu pump itaweza kusukuma maji lita ngapi kwa saa. Hapo ndio utakutana na 0.75 Hp mpaka 3 Hp, Mengine yatakayofata utaangalia umbali kutoka chanzo cha maji mpaka shambani.

Maranyingi pv pipe huwa ni nchi 1, pump zipo aina mbalimbali, mimi natumia pump kutoka China kwajiri ya gharama nafuu.

Wajuzi zaidi watakuja kutujuza zaidi.
 
Nashukuru sana mkuu, kisima kipo kina kina cha ft30, Mimi shauku yangu ni kujua gharama ya hiyo pump.
 
Kama walifanya watakuambia pump unayotakiwa kutumia ni HP ngapi, kutegemea na wingi wa maji katika kisima chako, nahisi itakuwa kati ya 0.75Hp au 1 Hp ikizidi sana itakuwa 1.5 Hp kama ni zakichina Itakuwa kwenye 350,000/= mpaka 450,000/= Aina ya Doyng. Ukitaka za Ulaya ni kwanzia 800,000/= mpaka milioni kadhaa kwa Hp hizo hizo but kupata uwakika wabei nenda kariakoo gerezani, au kiungani na nyamwezi ndio kuna maduka mengi sana ya mambo hayo.
 
Walifanya pump test?

Mkuu sorry, ni watu gani waliokupimia uwepo wa maji na hao hao waliochimba kisima au aliyepima na aliyechimba ni tofauti?. Huwa naona kama conflict of interest mtu huyo huyo mmoja kupima na kuchimba.
 
Waliochimba ndio waliopima uwepo wa maji na wakahakikisha wanayapata lakini tulishindana kwenye bei ya kunisetia pampu maana ilibidi initoke 4m kwa DC pump sasa nkaona ni gharama
 
Kama unauhakika maji yapo ya kutosha kuna mambo mawili utumie pamp kwa umeme wa jenereta au pampu ya solar hapo pampu ya 0.5 hp inatosha
 
Kwa solar pump naweza pata kwa kiasi gani?

Walau yenye uwezo wa kusukuma kama futi kama 30 hivi.
Nisaidie kama unajua bei ya hiyo pump.....uzuri wake solar panels ninazo za kutosha
 
Kama unazo panel haiwezi kuwa ghali sana sbb complite na panel zake ni kama ml 2
 
Nashukuru sana mkuu, kisima kipo kina kina cha ft30, Mimi shauku yangu ni kujua gharama ya hiyo pump.
Mkuu unamaanisha Mita30 au 30futi...!!! kama ni Futi 30 manake itakuwa kama 9Mita sasa kwa Kisima cha mita 9....Labda kama kina Maji mengi kama kidogo utakuwa unaitengeneza kila siku sababu itakuwa inanyonya hadi michanga Haitakawia kuJAM...kama ni 30mita angalau hii unaweza kutumia 0.5HP....ambayo uwezo wake ni kuanzia Mita 50
 
Kwa solar pump naweza pata kwa kiasi gani?

Walau yenye uwezo wa kusukuma kama futi kama 30 hivi.
Nisaidie kama unajua bei ya hiyo pump.....uzuri wake solar panels ninazo za kutosha
Jilidhishe kwanza urefu wa Kisima then uje nitakupa maelezo yote Pamoja na Panel ngapi utumie za Solar ili Pump ifanyekaz vzr...hizi ndio Shughuli zetu
 
sawasawa mkuu, ntakutafuta kama vip naomba nisaidie namba yako PM ili nikucheki hewani
 
Back
Top Bottom