Nahitaji kwenda Ruaha National Park

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,446
6,308
Habari wakuu,

Naitaji kwenda mbuga ya Ruaha sasa shida yangu ni maelekezo ya njia ya kufika Ruaha kutoka Iringa mjini.

Niko Mbeya na Iringa napajua sasa kutoka Iringa mpaka Ruaha ndio shida sasa kwa mtu yoyote ambae anaweza kunielekeza please naomba msaada kwenye tuta.
 
Ukifika Iringa pale Samora junction kunja kulia, mbele kama mita 150 ivi utakuta stand ndogo uliza njia ya kwenda Kalenga, ukifika pale kwa mtwa mkwawa (Kalenga) uliza njia ya kwenda Tungamalenga, huwezi kosa abiria kadhaa wa kwenda nao hadi Tungamalenga, hapo tunga utapewa directioin hadi getini Ruaha national park. Travel safe.
 
Ukifika iringa pale samora junction kunja kulia, mbele kama mita 150 ivi utakuta stand ndogo uliza njia ya kwenda Kalenga, ukifika pale kwa mtwa mkwawa (Kalenga) uliza njia ya kwenda Tungamalenga, huwezi kosa abiria kadhaa wa kwenda nao hadi Tungamalenga, hapo tunga utapewa directioin hadi getini Ruaha national park. travel safe

Thank you so much
 
Lazima ufike iringa mjin juu kabisa,tax gharama 50000 had Lakimoja ila kama utatumia gari za tour 200000. Umbali hadi unafika Tungamalenga getini kilomita 120 toka round about Samora Iringa. Ukipanda basi upendo nauli ni 4500. Mengineyo kuazia getini tongamalenga kuingia hifadhin hayo, nagari utapandia panaitwa Mlandege kama ni bus utatumia.
 
Nimefurahi sana kiongozi mana mi napenda sana utalii wa ndani na nilishaenda mbuga ya Ruaha. Kwenye safari yangu nakumbuka kutoka Iringa mjini ad mbuga ya Ruaha palipo ndani kabisa ya mbuga kwenye ofisi zao na nyumba za makazi nilitumia masaa kama 5 hivi sababu kubwa ni barabara ya kwenda uko ni rasta hivo mwendo ni mdogo mana madereva wanaogopa kuchana tairi au gari kuharibika ukienda kwa spidi kubwa.

Nilifarijika sana na naamini lazima nitarudi tena kufanya utalii, ni mbuga nzuri mno na simba wako wengi sana tena makundi.
 
Gharama za kulala kwenye lodge za serikali zikoje?
 
Gharama za kulala kwenye lodge za serikali zikoje?
Mie nilienda tukiwa group la watu wengi Ivo sikujua malazi kwa mtu mmoja mmoja ilikua kiasi gani Ila kulikua na option kwa ambao walikua couple kuongeza elfu 20 kulala kwenye bandas wakiwa couple.
 
Ukifika Iringa pale Samora junction kunja kulia, mbele kama mita 150 ivi utakuta stand ndogo uliza njia ya kwenda Kalenga, ukifika pale kwa mtwa mkwawa (Kalenga) uliza njia ya kwenda Tungamalenga, huwezi kosa abiria kadhaa wa kwenda nao hadi Tungamalenga, hapo tunga utapewa directioin hadi getini Ruaha national park. Travel safe.
Tawire
 
GOOGLE MAP tu, kajipe shavu
64264174_2411052189125579_2824154585843630080_n THM.jpg
 
Mmh unless unambie unataka kujua about kitu gani haswa, coz nimepata uzoefu mwingi kwenye mambo mengi
1.Njia bora zaidi ya kufika hifadhini (kutokea Mbeya)
2.Gharama ya kiingilio, usafiri hifadhini, malazi na chakula ndani ya hifadhi
3.Aina ya wanyama waliopo hifadhini
4.Changamoto zozote uwapo hifadhini.
 
Back
Top Bottom