Nahitaji kutumia bati zilizokataa kushika rangi kiwandani AKA reject

mumewanguu

JF-Expert Member
Mar 2, 2018
261
259
Kuna bati zinauzwa mtaani yaani ni mpya sema rangi yake imebabuka babuka haijashika vizur nahitaji kuzitumia katika ujenzi wa nyumba Mana Bei ni rahisi 13000 ft 10
Je Kuna yeyote anayejua vizur ubora wa bati hz
 
Labda kujengea mabanda ya mifugo ila kwa nyumba yako mwenyewe huto itendea haki na hujitendei haki kama una haraka bana matumizi kama bia punguza round uweke bati zinazofaa
 
Kuna bati zinauzwa mtaani yaani ni mpya sema rangi yake imebabuka babuka haijashika vizur nahitaji kuzitumia katika ujenzi wa nyumba Mana Bei ni rahisi 13000 ft 10
Je Kuna yeyote anayejua vizur ubora wa bati hz

Mkuu kwanza pata elimu kuwa hakuna bati reject iliyokataa kushika rangi bali hiyo ni mibati garasa kutokana na chuma chakavu toka maduka ya wahangaikaji wa mjini hivyo muda si mrefu wewe utapigwa na baada ya mwaka mmoja ukiwa ndani ya nyumba yako utakuwa unaliona jua toka linavyotoka mpaka linapozama na usiku unaona mbalamwezi kama TV yenye chenga chenga, nakushauri kupata bati reject za uhakika nenda pale kiwanda cha ALAF karibu kabisa na Tazara pata mtumishi mmoja hasa kutoka kitengo cha sales atakuelekeza namna bora ya kupata bati hizo toka kiwandani au atakupatia contact namba za mfanyabishara mwaminifu ili euende kupata mahitaji yako bila kutapeliwa, angalia nati zimekaza balaa usije kuwa mbuzi wao wa sikukuuu
 
Mkuu bora upaue kwa bati chache vyumba vichache uhamie kuliko kuweka bati kimeo ambazo baada ya muda mfupi unarudi kwenye tabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom