Nahitaji kutengeneza Android Application lakini sijui lugha yoyote ya kompyuta sehemu ya kwanza (01)

matthew2000

New Member
Apr 6, 2021
4
45
SEHEMU YA KWANZA:
MAHITAJI(TOOLS) YA KUWEZA KUFANIKISHA UUNDWAJI WA ANDROID APPS

Kuna programu kadhaa ambazo zinahitajika ili kuweza kuunda hizi apps, programu hizo ni kama zifuatazo:
1. kompyuta inapaswa iwe na JAVA Development kit (JDK)
Apps za android kwa asilimia kubwa huundwa kwa kutumia java hivyo ni vizuri ukapata SDK ya javaa ambayo ni latest kabisa, unaweza kuipata kwa kutumia link ifuatayo,

Java SE Development Kit 8 Downloads
(https://www.oracle.com/java/technologies/javase/javase-jdk8-downloads.html)

2. Android SDK ambayo imeambatanishwa na Android Studio IDE
Hizi tools zipo kwa ajili ya platform(OS) tofauti tofauti, kwangu mimi nitakuwa natumia windows na si linux lakini ukitaka kwa upande wa linux pia zipo.

Android Studio ndio ambayo tutaitumia katika kuandika codes, hii ni IDE rasmi ya android kwani zamani Eclipse IDE ndio iliyokuwa inatumika.

links.

kwa ajili ya windows,
Download Android Studio and SDK Tools | Android Studio
( Download Android Studio and SDK tools | Android Developers )

TUJARIBU KAMA TOOLS ZINAFANYA KAZI IPASAVYO.
Natumai umeweza kuinstall hizo tools pasina na tatizo lolote, fungua Android studio hiyo android na kwa mara ya kwanza utakutana na inteface mpya


Chagua "Start a new Android Studio project", Baada ya hapo
Hiyo sehemu ya application name unaweza kuipa jina lolote ambalo unalolita, badala ya hapo utabonyeza next,

Na baada ya hapo bonyeza next na itakuja interface ambayo itakutaka kuchagua muonekano wa jumla wa app yako jinsi itakavyoonekana kwenye simu ama tablet na utachagua "empty activity". na utabonyeza next na kisha finish.

Badala ya kumaliza hayo yote, ufuatao ndio general environment ya Android studio IDE, tutaendelea kujua tools zote ambazo zinapatikana kwenye hizo ide,

Kwenye title bar kuna "activity_main.xml" na "MainActivity.java",

"MainActivity.java" ndilo java file ambalo source code za java na maswala yote ya logic huandikwa.

"activity_main.xml" hili ndilo file la xml ambalo hufafanua muonekano wa jumla wa app. kwenye android studio activity_main.xml file zipo kwenye miundo miwili, 1. muundo wa maandishi(xml source codes) 2. mundo wa kimuonekano wa simu design.

kwa hiyo unaweza kuchagua muundo gani ni rahisi ili kuunda interface unayoitaka kama ni "Text" au "Desin".

line 1 ambayo ya blue inawakilisha sehemu ya kubuild na ku-run app project , lakini kama ya ku-run app unatakiwa uweze kutengeneza android virtual device (AVD), hii ni emulator (mfano wa simu za android) ambao upo kwenye muundo wa software kwa kila ukimaliza project na kuirun basi result za hiyo app zitakuwa zinatokea kwenye hiyo emulator, bonyeza AVD manager ambayo imewakilishwa na line 2 nyekundu kuunda emulator. pia unaweza kutumia simu halisi ku-run apps.

Baada ya kutengengeneza AVD basi run project hakikisha emulator imetokea na kukuonyesha result ya "hello World!", kama imekubali basi kila kitu kipo sawa na tuwe tayari kwa ajili ya kujifunza zaidi.

itaendelea...

kujifunza zaidi kwa njia ya video

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom