Nahitaji kusoma kwenye chuo cha afya nchini Marekani

jembelamkono

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
2,733
2,003
Habari wakuu,

Nahitaji kwenda kusoma nchini Marekani katika kozi za Afya especially nursing, nategemea kujigharamia mwenyewe gharama zote mpaka kumaliza masomo.

Naomba kupewa taarifa na wazoefu, ni vyuo gani vinavyotoa kozi za afya kwa muda mfupi,mfano miaka 2?

Na je gharama na taratibu za udahili zikoje?

Karibuni tupeane maarifa,wadau wenye habari juu ya hili.

Wasalaam.
 
Ingia google utapata maarifa mengi sana kuhusiana na jambo lako,huku uje kuongezea uzoefu wa wadau.
 
Jembe la mkono Salaam..

Najua hizi purukushani zilianza muda mrefu sana na ndugu Daby japo sijui siku hizi yupo wapi japo mara ya mwisho alikua Bondeni

Najua lengo lako ni kuzamia(kuanchana na dunia hii ya 3 hususani TANZANIA nchi yenye udongo wenye rutuba usiostawisha)

Nakupa uzoefu wangu (Binafsi nilipata Visa ya CANADA ya kusoma kwa miaka 2)


kwa Marekani sikushauri kabisa kwasababu gharama zao zipo juu sana kwenye kusoma kutokana na dola kua juu ukilinganisha na TSHS.

Hivyo naomba nikushauri kitu kimoja, Elimu yako ni degree ya kitu gani? kisha tafuta collage za CANADA zipo nyingi sanaa kwa gharama nafuu

ukiwa na 56,000,000 milion unaingia ubalozini na visa unapewa
 
Back
Top Bottom