Nahitaji kuonana na Rais Magufuli kumuelezea ukwepaji mkubwa wa kodi nilioushuhudia

Babaako

Member
Mar 10, 2016
15
22
Jamani mwenye msaada wa kuniwezesha kuonana na Rais Magufuli naomba anisaidie. Mimi ni Certified Public Accountant (CPA).

Acha niende moja kwa moja kwenye point. Jana katika harakati za kutafuta wateja nimeshuhudia kodi ya mabilioni inayokwepwa kulipwa kwa njia ya udanganyifu mkubwa ambao hata TRA hawezi kung'amua jinsi hao wafanyabishara wanavyocheza na huo udanganyifu.

Naomba kuonana na Rais Magufuli ili nimuonyeshe jinsi hii inchi inavyochezewa. Kwa yale niliyoyashuhudia, kweli nchi hii tuna safari ndefu kupambana na ukwepaji kodi. Watu wanapiga mabilioni ya fedha halafu bila aibu wanadai kupata hasara na wakati mwingine wanaidai Serikali "tax refund".

Please mwenye kunisaidia kuonana na mheshimiwa Rais Magufuli atakuwa amefanya jambo la kizalendo sana. Naona wengi mnataka nielezee hapa hapa jinsi huo ukwepaji kodi unavyofanyika. Kwanza kwa ethics za taaluma yetu ya uhasibu hatuwezi ku-disclose sensitive issues kama hizo kwenye public.

Pili, kwa kile nilichokishuhudia kinahitaji mtu mwenye mamlaka ya juu kabisa kukisikia. Kwenda kureport fraud kama hii TAKUKURU au TRA nahisi huenda hii taarifa ikawarudia wahusika na rushwa inaweza kutembea hivyo tatizo likawa palepale au ndio kuzidi kabisa.

...Mnaikumbuka ile scandal ya yule jamaa aliyekuwa anatengeneza sijui milion 7 kwa dakika moja? Hii issue kidogo inataka kufanana na hiyo.
 
Mwenyewe ungekuwa na uzakendo si ungeweka humu ni jinsi gn huo ukwepaji unafanyika!! BTW hivi nani katuloga kuwa kila kitu ni lazima ifanywe na Rais tu???? Kazi ya taasisi km TRA, TAKUKURU, n.k pamoja na wasaidizi wa rais ni nn?
 
Kwani kuongea hilo na Raisi tu? Mbona hata wasaidizi wake au TRA wenyewe watakusiliza na kulifanyia kazi hili, Mkuu wapo watendaji wachini wazalendo kama wewe.
 
mwenyewe ungekuwa na uzakendo si ungeweka humu ni jinsi gn huo ukwepaji unafanyika!! BTW hivi nani katuloga kuwa kila kitu ni lazima ifanywe na Rais tu???? Kazi ya taasisi km TRA, TAKUKURU, n.k pamoja na wasaidizi wa rais ni nn?
Hao hawaaminiki hata kidogo! Wanafanya kazi pale wanapoagizwa na Rais baaas. Hivi hivi sahau. Hebu wewe nenda katoe taarifa uone kama hiyo infos haijamrudia mfanyabiashara husika ndani ya siku moja.
 
Kwani kuongea hilo na Raisi tu? Mbona hata wasaidizi wake au TRA wenyewe watakusiliza na kulifanyia kazi hili, Mkuu wapo watendaji wachini wazalendo kama wewe.
Kama wale waliokataa viroba vya hela pale bandarini ili wasipitishe mafuta ghafi.Wale pia Rais anapaswa kuwa -promote kama alivyofanya kwa Kaimu Kamishna.Maana bila wale kukataa ule mpunga,hata huyo Kamishna mkuu asingejua.Bila shaka mamlaka ya upandishwaji wao ipo chini ya Kamishna,atatenda jambo
 
Ila sema Mr.President mwenyewe huwa anatumia mikutano mingine kwa kutokujua,anatufundisha kukwepa kodi.Kule Kilombero kwenye ziara yake,alikuwa anasema kusafirisha bila ushuru mwisho tani moja....Kwa hiyo we kama una tani kumi au isihirini,basi beba moja moja toka home mpaka sokoni....Hata kama mara kumi kwa siku ili usilipe kodi
 
Mleta uzi unatafuta promosheni ? Wahusika wa Kodi Wapo why mpaka Rais. This is cheap popularity. Shut up.
 
Unataka sifa eeh...wacha wakwepe kodi tuu .hata namii nna mpango huo,.maana kod sasa zmekua za kukomoana

Acha sifa.na kujipendekeza..we ungekua unafanya biashara na mtaftaj wala usingethubutu leta hii kitu hapa sabab ungeujua uchungu tunaopata wafanyabiashara nw,
Inshort ,acha sifa na kujipendekeza
 
Back
Top Bottom