Nahitaji kujua misimu ya kilimo na ni mbolea ipi inayofaa kwa mazao ya aina zote?

Dec 22, 2020
26
21
Habari wana Jf,

Ninaomba kujua ni mbolea ipi hasa inayofaa kwa mikoa yote na kwa mazao ya aina yoyote ile. Pia ni misimu gani ya kilimo ambayo inafaa kwa anayetaka kuuza mbolea?

Ahsanteni
 
Hamna mbolea inayofaa kwa mazao ya aina yote na mikoa yote...

Ila kuna mbolea inayofaa kwa mazao flani flani na kwa sababu flani flani.Kuhusu mikoa yote kuna mbolea inafaa sehemu flani kwa sababu flani..

Umeuliza swali ambalo majibu yake yanaweza kujaza kitabu cha page 1000.

Sasa sema hivi Nipo mkoa A,Ni ukanda wa joto/baridi,Nataka kulima za B,msimu wa baridi/Joto,udongo wa shamba ni C,Msimu wa mvua/kiangazi,Ardhi ni bikra/imetumika,Nataka kumwagilia kwa kutegemea Mvua/mto/kisima.

Nahitaji ushauri,Je itafaa?

Misimu ya mvua ndo misimu ya kupiga hela kwa wauza mbolea.

Na kama lengo ni kuuza mbolea sema tujue straight tunakushauri vip
 
Typing error mkuu , Sorry

Sawa sijajua unataka kuuza wewe kama wewe au kupitia maduka ya pembejeo za kilimo..

Ila super gro kama inafahamika kwa wakulima na kuna maduka ya pembejeo mengi tu yanauza..

Kwahiyo ni rahisi kwako kama unaweza kwenda field moja kwa moja na kuanza kuwauzia wakulima hasa maeneo ambayo wanalima sana mbogamboga,mpunga.

Ukitaka kuuza hiyo bidhaa lazima ujue wapi kuna wakulima wengi...

Mfano msimu wa mpunga ukiongea vzr na M/kiti wa wakulima bonde la mpunga rukwa/kyera/usangu anaweza kukuunganisha na wakulima wa mpunga ukauza bidha nyingi kwa pamoja na hata kwa kupima pima...

Unahitaji strategy sababu kuna liquid fertilizers nyingi sokoni ambazo ni bei chini na Wakulima wetu wanapenda cheap.

Super gro ni bidhaa nzuri utauza km ukiwa na plan nzuri.Ningekuwa wewe iringa na Moro ingekuwa target yangu ya kwanza.
 
Mwaka 2017, wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi. Kitabu chenye jina...

MWONGOZO WA UZALISHAJI MAZAO
KULINGANA NA KANDA ZA KILIMO ZA
KIIKOLOJIA, hard copy na softy copy.

Kitabu kina kilakitu unachohitaji kujua kuhusu kilimo.
Kimeeleza ni mkoa gani, wilaya gani, ulime mazao gani, kwa wakati gani na jinsi ya kuhudumia (mbolea na n.k). Kitabu kitaisha matumizi yake mwaka 2026 then watatoa kingine.

Ninayo PDF ila nimeshindwa ku upload, network zinasumbua, nipo shamba.

Search kupitia Google au tembelea page ya wizara ya kilimo, utapata hiyo pdf.
 
Wataalamu wa kilimo mngechapisha vitabu vya kutoa elimu hii hakika mngepata faida na kusaidia wengi.
Ni kweli best nimeanzisha ukulima WA kwenye containers SASA nimeuliza humu habari za Peatmoss na Perlite hakuna anaenijibu. Mbona nchi za wenzetu wanavyo?. Ila ukianzisha umbea WA nyoka WA Ginimbi utaambiwa Hadi rangi yake.
 
Mwaka 2017, wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi. Kitabu chenye jina...

MWONGOZO WA UZALISHAJI MAZAO
KULINGANA NA KANDA ZA KILIMO ZA
KIIKOLOJIA, hard copy na softy copy.

Kitabu kina kilakitu unachohitaji kujua kuhusu kilimo.
Kimeeleza ni mkoa gani, wilaya gani, ulime mazao gani, kwa wakati gani na jinsi ya kuhudumia (mbolea na n.k). Kitabu kitaisha matumizi yake mwaka 2026 then watatoa kingine.

Ninayo PDF ila nimeshindwa ku upload, network zinasumbua, nipo shamba.

Search kupitia Google au tembelea page ya wizara ya kilimo, utapata hiyo pdf.
Mkuu nakihitaji hicho kitabu kama hautajali nije inbox nikupe namba yangu unitumie WhatsApp.

Natanguliza shukurani
 
Ni kweli best nimeanzisha ukulima WA kwenye containers SASA nimeuliza humu habari za Peatmoss na Perlite hakuna anaenijibu. Mbona nchi za wenzetu wanavyo?. Ila ukianzisha umbea WA nyoka WA Ginimbi utaambiwa Hadi rangi yake.
Sio kila wanacho anzizha wazungu nawe lazima uanzishe Afrika.Mzungu hana ardhi kubwa mwafrika ana ardhi ya kubwa tens
a sehemu zingine huweki hats
a mbolea.Kwa nini uingie gharama wakati nature ina kusapoti.Chunguza walioanzisha kilimo cha green house wengi wamefeli kuliko waliofaulu.Unalima nyanya kwa gharama ndani ya green house huku mwenzio analima kiasili huko njombe halafu anauza bei bwerere were unauza bei kubwa unashindwa sokon.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom