nahitaji kujua fistula ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nahitaji kujua fistula ni nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by silent, Feb 25, 2012.

 1. s

  silent Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari wana wa forum, kwa upeo wangu fistula ni ugonjwa wa kutokwa na haja ndogo mara kwa mara na kwa kutokujijua kama unatokwa na haja ndogo na mara nyingi huwatokea mama zetu baada ya kujifungua..Sasa wana wa forum nahitaji kujua zaidi maana ya huo ugonjwa na dalili na cause zinazopelekea ugonjwa huo kuwapata mama zetu.Na pia kuna ukweli wa aina yeyote unaosema kwamba fistula kwa asilimia kubwa huwapata wanawake wafupi? Nipe majibu yenu ili nipate kujua zaidi kuhusu ugonjwa wa fistula
   
 2. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu, fistula by definition is an abnormal communication between two epithelial surfaces, maana Yale ni mawasiliano yasiyo ya kawaida Kati ya sehemu
  Mbili zisizotakiwa kuwa na muingiliano, ndani njia ya mkojo kibosh na uke, njia ya uke na njia ya haja kubwa, koo la hewa na koromeo la chakula. Mara nyingi mawasiliano haya kuwa bi kwa viungo vilivyo karibu karibu.
  Wanawake kupata fistula hii Gironde zaidi wakati Wa kujifungua, mwanamke anapokuwa na nyonga ndogp itakayoshindwa kupitisha mtoto na hapa anakuwa mbali na hospitali kupata huduma ya upasuaji kunyoa mtoto. Hapa wanapata uchungu pingamizi kwa muda mrefu, kichwa cha mtoto kukandamiza sehemu ya uke kwa juu kuna libido cha mkojo na chini kuna njia ya haja kubwa! Sehemu hizi kukandamizwa kwa muda mrefu hupelekea tissue za sehemu hiyo kukosa blood supply na hatimaye kufa na hivyo kuweka tundu
   
 3. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu, fistula by definition is an abnormal communication between two epithelial surfaces, maana Yale ni mawasiliano yasiyo ya kawaida Kati ya sehemu
  Mbili zisizotakiwa kuwa na muingiliano, ndani njia ya mkojo kibosh na uke, njia ya uke na njia ya haja kubwa, koo la hewa na koromeo la chakula. Mara nyingi mawasiliano haya kuwa bi kwa viungo vilivyo karibu karibu.
  Wanawake kupata fistula hii Gironde zaidi wakati Wa kujifungua, mwanamke anapokuwa na nyonga ndogp itakayoshindwa kupitisha mtoto na hapa anakuwa mbali na hospitali kupata huduma ya upasuaji kunyoa mtoto. Hapa wanapata uchungu pingamizi kwa muda mrefu, kichwa cha mtoto kukandamiza sehemu ya uke kwa juu kuna libido cha mkojo na chini kuna njia ya haja kubwa! Sehemu hizi kukandamizwa kwa muda mrefu hupelekea tissue za sehemu hiyo kukosa blood supply na hatimaye kufa na hivyo kuweka tundu Kati ya uke na kibofu
  Cha mkojo ndo unaona wanatoka mkojo muda wote au kinyesi kutokea
   
 4. s

  silent Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa kunisaidia kujua maana yake ila ni kweli hupata wanawake wafupi?
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mwanamke mwenye nyonga nyembamba itakayoshindwa kupitisha mtoto na akakosa huduma ya dharura ya upasuaji ataweza kupata fistula. Mwanamke anaweza kuwa mfupi akawa na mtoto ambaye ni mdogo na akazaliwa bila shida. Sio kila mwanamke mfupi anapata fistula. Muhimu kupeleka mama mjamzito hospitali mapema anapoanza uchungu madaktari watapima njia na kuangalia kama mtoto atapita.
   
Loading...