Nahitaji kujifunza driving sehemu ipi nitapata mafunzo ya uhakika?

Catha96

Member
Jun 29, 2021
54
70
Habari ndugu wana JF
Nipo Dar es salaam natafuta sehemu nzuri ya kujifunza driving ,gharama zake na muda wa mafunzo ni kwa muda gani naomba kufahamishwa.
Asante nawasilisha.
 
KAMA HUTAKI JANJA JANJA ANZA NA BASIC DRIVING YA (VETA) HALAFU KACHUKUE GAMBA LAKO ZURI KWA ADVANCED DRIVING PALE (NIT)

JAPO UNAWEZA KWENDA VYUO BINAFSI PIA, KWA MAFUNDI GEREJI UNAOWAJUA, KWA WASHIKAJI WENYE MAGARI YAO N.K

GHARAMA INATEGEMEA CHUO NA CHUO ILA ZINAANZIAGA 150,000 NA KUENDELEA... MUDA INATEGEMEA NA WEPESI WAKO WA KUJIFUNZA ILA INAKUWAGA WIKI 3 HADI MWEZI NA KUENDELEA
 
Njoo strategic school kijitonyama Karibu na ofisi ya serikari ya mtaa ya kijitonyama...au Karibu na Karibu na kabisa la krisko church..pia tunatoa na huduma nyingine ya reseaters na qt...
 
Nikifundishwaga hua siwez hata kama miaka miwili ila nikijifunzaga huwa nachukua siku siku moja

Mto mada umenikumbusha mbali
Miaka ya 2000 mzee alinilipia ada veta kujifunza udereva enzi hizo nina miaka 19 basi nikaanza mafunzo ila ulipita mwezi bila bila mzee akaongeza ada tena bila bila nikapelekwa private nako mwaka mzima hata steling siwez kuiongoza basi nikaamua kuachana ikapita miaka 5 mzee akanunua Volvo moja hiv matata bas imekuja tu siku mbili zimepita nikaanza kuifanyia zoez haikupita wiki nikakatiwa leseni huyoo njian mpaka leo hiyi inshallah kenya zambia na kwingineko nimevuruga sana nazan umepata kitu mtoa mada
 
Habari ndugu wana JF
Nipo Dar es salaam natafuta sehemu nzuri ya kujifunza driving ,gharama zake na muda wa mafunzo ni kwa muda gani naomba kufahamishwa.
Asante nawasilisha.
Ingia google play, download ‘Driving app’ yeyote nzuri, jifunze basics, halafu muombe ndugu yako yeyote mwenye gari akufundishe sehemu ya wazi, baada ya hapo aanze kukufundisha barabara za vichochoroni, ukishazoea contro lza gari, aanze kukuingiza lami za service road, baada ya hapo akupeleke main road , ila sehemu zisizo na traffic, baada ya mida utakuwa umejua. Leseni nenda kahonge tu unaletewa hadi mlangoni
 
Back
Top Bottom