Nahitaji kujenga nina milioni 13, mwenye ramani nzuri anipe

Kina mama kwenye huu uzi mbona siwaoni

au mnasubiri wengine tujenge nyie mje mjiite "mother house"??

ebu wanawake mkuje m comment mnapita tuu mnasoma kimya kimya

mje mseme hapa bei za kokoto sh ngapi,maana nyie ndio mnasumbua sana tarehe za kodi kutudai

msg zenu za kutukumbusha kodi zimezidi,haya mje hapa mseme nondo sh ngapi na hy 13M inatoa nyumba ya aje.
Wamama tupo,..ila nimeogopa kumkatisha tamaa mleta uzi,kwa ml 13 mimi nimejenga master,jiko,sebule na vibaraza mbele na nyuma.
Na haijaisha vyema,baadhi ya vyumba hakuna plaster
 
Hapo kwenye dirisha nyambulisha tuone hiyo 85,000 inavyofikiwa with kioo one way utafungua wengi
unajenga vizuri mno , fanya hesabu za tofali bati na nondo kwanza , cement , kokoto na mchanga hivyo ni rahisi mno , simamia mwenyewe na usitume mtu dukani , nenda mwenyewe .

kwa mfano dirisha la alluminium la 5×6 ukituma mtu atakwambia ni laki 2 unusu au laki 3 , wakati ukweli ni kwamba gharama la dirisha kama hilo hilo ukienda mwenyewe kununua vifaa na kutafuta tu fundi wa kukuunganishia haliwezi kuzidi elfu 85 , usiwe mvivu wa kusimamia tu
 
Kina mama kwenye huu uzi mbona siwaoni

au mnasubiri wengine tujenge nyie mje mjiite "mother house"??

ebu wanawake mkuje m comment mnapita tuu mnasoma kimya kimya

mje mseme hapa bei za kokoto sh ngapi,maana nyie ndio mnasumbua sana tarehe za kodi kutudai

msg zenu za kutukumbusha kodi zimezidi,haya mje hapa mseme nondo sh ngapi na hy 13M inatoa nyumba ya aje.
tupo mkuu ngoja kwanza wenye ujuzi waje ila kufanya finishing ndo tutaenda wote kununua material mkuu
 
Binafsi niko kwenye mchakato wa kujenga but tathmini yangu ya kwenye makaratasi kwa actual rates za mtaani bila bargaining hapo kila item nime assume nimeajiri mtu inaonesha naweza jenga nyumba ya kisasa ya vyumba 4 vya kulala 2 ni self,sebule,choo na sebule vya ndani,dining,jiko na store/duka
Hapo najenga na kuezeka msauzi bila finishing.It means nikifanya bargaining na other initiatives kama nilivyosoma michango ya wadau hapo juu naweza hamia nikawa nafanya finishing nikiwa ndani
Hilo la madirisha ngoja nilifuatilie
 
Mm nimejenga nyumba yangu huku moshi tofali za kuchoma(new land) na nikapauwa(bati za kawaida)nikaweka dirisha sio aluminium ila ni chuma pamoja na vioo,umeme(rea)maji(kirua Kahe water) kwa wakazi wa moshi wanaelewa

Sikuweka tiles wala plaster vyumbani ni rough tu chini nkahamia nilitumia gharama ya 8ml
Fundi nilimtoa kigoma 750000 kupandisha boma na kupauwa

Mkoani gharama za ujenzi zipo chini ukilinganisha na dar
Pia hao wanaokuambia kuna nyumba ya kiume na kike,yy mwenywe amepanga kwa mtogole chuma moja
Asee
 
Tafuta nyumba inayoendana na hiyo bei ununue. Kujenga kwa hiyo hela labda nyumba ya chumba kimoja, sebule, public toilet na jiko.

Vitu vinavyogharimu ni msingi, na finishing + mbao na mabati.

Tafuta fundi mwelewa na mwaminifu akupatie gharama zote za ufundi mpaka inakamilika nyumba yako.
 
Atapigwa kuna nyumba zinauzwa hazina hata lenta. Anaweza akanunua mjanga.
Bora ajenge mwenyewe aone.
Tafuta nyumba inayoendana na hiyo bei ununue. Kujenga kwa hiyo hela labda nyumba ya chumba kimoja, sebule, public toilet na jiko.

Vitu vinavyogharimu ni msingi, na finishing + mbao na mabati.

Tafuta fundi mwelewa na mwaminifu akupatie gharama zote za ufundi mpaka inakamilika nyumba yako.
 
Mm nimejenga nyumba yangu huku moshi tofali za kuchoma(new land) na nikapauwa(bati za kawaida)nikaweka dirisha sio aluminium ila ni chuma pamoja na vioo,umeme(rea)maji(kirua Kahe water) kwa wakazi wa moshi wanaelewa

Sikuweka tiles wala plaster vyumbani ni rough tu chini nkahamia nilitumia gharama ya 8ml
Fundi nilimtoa kigoma 750000 kupandisha boma na kupauwa

Mkoani gharama za ujenzi zipo chini ukilinganisha na dar
Pia hao wanaokuambia kuna nyumba ya kiume na kike,yy mwenywe amepanga kwa mtogole chuma moja
Ha ha ha ha huyu fundi ni kiboko yao.
Ilkuwa ya vyumba vingapi mkuu?
Hongera sana
 
Habari mkuu, njoo nikupe hii,

3 bedrooms
Sitting room
Dining
Kitchen
90 sqm

Contact 0715477041

nile -8.PNG
Screenshot_20210329-154649_Adobe Acrobat.jpg
 
Binafsi niko kwenye mchakato wa kujenga but tathmini yangu ya kwenye makaratasi kwa actual rates za mtaani bila bargaining hapo kila item nime assume nimeajiri mtu inaonesha naweza jenga nyumba ya kisasa ya vyumba 4 vya kulala 2 ni self,sebule,choo na sebule vya ndani,dining,jiko na store/duka
Hapo najenga na kuezeka msauzi bila finishing.It means nikifanya bargaining na other initiatives kama nilivyosoma michango ya wadau hapo juu naweza hamia nikawa nafanya finishing nikiwa ndani
Hilo la madirisha ngoja nilifuatilie
usiwe na haraka.jua kwanza vinavyofanya nyumba kuwa nyumba ni nin? ni boma ,kupaua milango na madirisha.ukimaliza hapo setting choo na sshimo lake.sambamba na kufanya wiring ya bomba na umeme.hapo unaingia na kulala hata kama haina rang ila plaster.tu.sana cha muhim kumaliza kwa ukamilifu ni choo.kiweke tiles saf kabisa na kimalize choo.sehem nyingine utaimaliza taratibu
 
Hapo tofari karibia 2000 na bandari 4 za bati.

Saruji kuanzia msingi, kujengea na ripu ni mifuko 80.

Nondo pc14, mbao za kenchi na papi zaidi ya pc 200.

Milango si chini ya mitano, madirisha si chini ya matano (utakayopenda).

Trip 10 za mawe ya msingi, kokoto trip 1, mchanga wa kujengea na ripu trip 20, mollarm ya kushindilia vyumbani trip2.

Misumari ya bati kg10, misumari mchanganyiko kg10, biding wire kg 5.

Rangi lt20@ ndoo4.

kuvuta umeme, kuvuta maji na wiring ya nyumba.

Tiles box 60, saruji ya kupachikia tiles mifuko20, graut pact 6.

Mkuu kiwanja unacho?

Embu tusaidiane kupigia hesabu kwanza hayo kutokana na bei ya kwenu, kisha ujumlishe na gharama za fundi ujenzi na bill ya maji wakati wa ujenzi, kisha uje na mrejesho.
We ndg umesaidia weng na hii short budget ya vitu
 
kwa requirements yako milion 13 inatosha kujenga iyo nyumba..kama upo siliac nichake inbox ntakufanyia estimates, desgn ya michoro 3D rendering
 
Back
Top Bottom