Nahitaji kufungua tuition centre kubwa na maabara katika mkoa wangu ili niajili na kusaidia jamii yangu

Wilinasi Petroleum

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
207
197
Habarini ndugu zangu nahitaji kufungua tuition centre yangu kubwa pamoja na maabara katika mkoa wangu, ili niajili na kusaidia jamii yangu.

Hebu nisaidieni mawazo, changamoto zake ni zipi? Na mahitaji ni Yepi?
 
Hawata kuwa na hela ya kukupa,maana hiyo hela ya malipo uliyoipanga ni nyingi sana kwao,maana huko maisha ni magumu sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hawata kuwa na hela ya kukupa,maana hiyo hela ya malipo uliyoipanga ni nyingi sana kwao,maana huko maisha ni magumu sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Sio kweli, sijaanza kufundisha Leo mkuu, tangia nikiwa Darasa la Tano mwaka 2003 mpaka 2015 mimi nilikua nafundisha twisheni na nilikua nalipwa, Mara baada ya kuhitimu chuo pia nimefundisha sanaa mpaka nilipo chukuliwa na shule moja ya private walio nidanganya kunilipa mshahara mnono wa milioni 1 moja net. Mara nilipo anza kufundisha nilipatwa kupendwa sana wanafunzi kwasababu nilipenda wanafunzi wangu waelewe ili wajichotee maarifa kutoka kwangu. Kitu moja kilicho niboa kwenye ile kazi sikua huru, kabisa muda mwingi niliutumia kuwaza wanafunzi na kufundisha pamoja kuandaa lesson plans. Lakini pia kufuatiliana kulikua kwingi sana, ndipo nilipo amua kuacha kazi na kuendelea na kazi zangu binafsi. Lakini kabla ya kuacha kazi mimi na mwalimu wenzangu tumekuwa tukisumbuliwa sana na mamia ya wanafunzi wanao Hitaji tuwafundishe changamoto ilikua ni muda na eneo la kuwafundishia ilitubidi wakati mwingine tuwafundishie practical nyumbani tunako ishi. Ndipo nilipo kuja na wazo la kutatua tatizo katika mkoa wangu. Nimesha nunua uwanja, sasa ndio nipo naplani jengo moja tu kubwa la kawaida kwaajili ya kuanzisha darasa langu.
 
mi nadhani kma capital sio ishu, changamoto inabaki kwenye location ya vyote hvyo viwili. na pia inahitaji uvumilivu ili utengeneze jina na wateja wa kudumu kwanza.

kwakua umesema usaidie jamii, kwakuweka gharama za chini na nafuu zaidi utakua umesaidia vikubwa jamii yako. (usitake faida za haraka).
 
Mm niliachana na mpango wa kufundisha tuition nilipomaliza chuo kikuu 2007 nikaamua kuwa tu nafundisha mathematics mtu mmoja mmoja nyumbani kwake kwa gharama ya 10,000 /= kwa lisaa limoja.Wateja wangu wengi ni watoto wa kishua ,wahindi , wazungu pamoja na wanavyuo vikuu.

Faida yake ni kwamba mda aunibani kufanya biashara au mambo mengine mfano kwa ss nina wanafunzi sita pale Masaki mmoja anaenda kuanza first year Cambridge University -UK,wengine O-level,wanafunzi wa biashara ,vipindi naanza saa 12 asubuhi mpk saa 6 mchana nishavuta 60k naingia mtaani kwenye mishe zangu.

Changamoto za tuition center ni hizi:
1.Muamko wa elimu katika mkoa au mtaa husika
2.Kipato cha wazazi mfano vijijini huko vipato vyao vidogo labda ufanye kwa topic moja mwanafunzi anakulipa fungu moja la nyanya .
3.Baadhi ya viongozi wanapiga marufuku dhana ya tuition.
4.Upatikanaji wa eneo kubwa (Darasa) na la kodi nafuu.

Nakutakia kila la kheri !
 
Historia inaonesha wanafunzi wanaosoma tuition sana ndo wanaongoza kwa ufaulu afifu. Ni muda muafaka sasa kwa serikali kupiga marufuku tuition.
 
Back
Top Bottom