Nahitaji kufahamu nini chanzo cha majipu na tiba zake sehemu za siri

Frank Lyova

Member
Feb 20, 2017
13
10
Habari zenu wana JF,

Kuna magonjwa mengine kama yanadharirisha hivi jinsi ya kuyatamka kwa watu.. lakin ndo hvyo waswahli walishatwambia mficha malazi kifo umuumbua.. Mimi ndugu zangu nina tatizo la jipu limenitokea kwenye makalio pemben kidogo mwa njia ya haja kubwa..

Ni kama uvimbe ulio mgumu endapo utaubinya..Hii jipu limeniletea homa kabisa na linauma kiasi nashndwa hata kukaa vizuri..

Hivyo naomba kufahamu wenye uzoefu na haya magonjwa au kama uliwah kuumwa nahtaji kufahamu ni dawa gani itanitibu au matatizo haya chanzo chake ni nini?

Nahtaji kushauriwa na wenye uzoefu wa haya matatizo tu..
 
Hilo silo jipu ni ugonjwa unaoitwa kwa jina Bawasiri nenda Hospitali ukatibiwe usipo pona nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.

Bawasiri (Hemorrhoids)​

MARADHI YA BAWASIRI.jpg

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri​

Nje​

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani​

Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili. Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?​

Bawasiri husababishwa na
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri​

  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri​

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi​

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu​

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy
  • kutibu chanzo cha bawasiri

Njia za kuzuia Bawasiri​

  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa. chanzo. Bawasiri (Hemorrhoids)
 
Hilo silo jipu ni ugonjwa unaoitwa kwa jina Bawasiri nenda Hospitali ukatibiwe usipo pona nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.

Bawasiri (Hemorrhoids)​

View attachment 1888909

sasa mkuu kama ni bawasiri mbona leo kinaanza kutoa usaha.. au bawasiri nayo hutoa usaha kama jipu
 
Back
Top Bottom