Nahitaji kufahamu kuhusu chama cha ADC!

Mkomawatu

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
267
118
Habari ndugu zangu wana JF! Upo msemo mmoja wa kiingereza usemao "no research no right to speak", hivi ndivyo ilivyo kwangu binafsi,naomba wadau wenye taarifa za kina kuhusu chama cha ADC wanijuze,nahitaji kufahamu makao makuu yake,utaratibu wa kujiunga na chama,Je vipi chama cha ADC kina Jumuiya ya vijana Taifa,vilevile nahitaji kufahamu falsafa ya chama.Ndugu zangu naomba nisaidiwe tafadhali kwa sababu hadi sasa nipo kwenye upembuzi wa chama cha kujiunga nacho.
 
Ngoja nikuitie Mzee Mwanakijiji akusaidie. Mara nyingi yeye ndiye mfuasi wa vyama vya staili hii kama ilivyokuwa kwa CCJ!
 
Last edited by a moderator:
Ungeuliza kuhusu ccj ninge muita Nnauye Jr ndio anakifahamu vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Habari ndugu zangu wana JF! Upo msemo mmoja wa kiingereza usemao "no research no right to speak", hivi ndivyo ilivyo kwangu binafsi,naomba wadau wenye taarifa za kina kuhusu chama cha ADC wanijuze,nahitaji kufahamu makao makuu yake,utaratibu wa kujiunga na chama,Je vipi chama cha ADC kina Jumuiya ya vijana Taifa,vilevile nahitaji kufahamu falsafa ya chama.Ndugu zangu naomba nisaidiwe tafadhali kwa sababu hadi sasa nipo kwenye upembuzi wa chama cha kujiunga nacho.

Mkuu unataka kuwa mwenyekiti wa vijana wa ADC? mpigie Mhe. Hamad Rashid mlezi wa chama cha ADC ili akusaidie
 
Nape yupo nyuma ya ADC kwani hajiamini gambani akikigwaya kivuli cha Lowassa..NAPE kadi ya CCJ umemkabidhi nani?
 
Back
Top Bottom