mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 2,985
- 9,316
Salamu kwa wakubwa zangu na madogo zangu humu natumai nyote ni wazima wa afya.
Ni kweli kila mtu anajua Rais ndio kiongozi wa nchi na ana majukumu kadha wa kadha hususan katika kuleta maendeleo kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi husika.
Mimi ninachojua kwa mtu yeyote kuna tabia fulani fulani au tuseme kasumba lazima awe nazo hivyo kwa kuwa Rais naye ni mtu tu wa kawaida basi pasi na shaka kuna vijitabia lazima awe navyo haijalishi ni vijitabia vizuri au vibaya.
Ninachotaka kujua
1. Je, Rais yeyote anapokabidhiwa Ikulu (madaraka) kunakuwa na jopo la wataalamu wa masuala ya Saikolojia kwa ajili ya kumsaidia na kumshauri namna ya ku-behave mbele ya watu akiwa umma?
Nimeuliza hivi kwa sababu mtu anakuwa na vijitabia Mfano kuna tabia nyingine tuseme kuropoka , kujikuna sehemu za siri au kutema makohozi mbele za watu n.k.
2. Je, pia kuna mwalimu/mentor specifically anayemfundisha namna ya kuongea kwenye umma wa watu? Yaani aongee nini , wakati gani, mahali gani na kwa ajili ya nini?.
3. Unapokuwa Rais kuna tabia nyingine lazima uziache kutokana na hadhi ya cheo husika. Mfano umalaya,ulevi n.k je kuna kitengo maalumu cha kufuatilia tabia za Rais binafsi ambazo ni mbaya akiwa out of public eyes?
4. Na je kama hataki kuacha hivyo vijitabia, kuna mtu ambaye anaweza kumfokea huko Ikulu kwamba acha hizo tabia ili asijidhalilishe yeye mwenyewe na cheo kizima cha Urais?.
Natanguliza shukrani .