Nahitaji kufahamu hii hali kukojoa mkojo wenye damu

Habari, wakubwa heshima yenu.

Mimi ni kijana umri ni 25 Me, kwanza nianze kwa msemo wa kiswahili usemao "mficha maradhi kifo humuumbua" nimeona leo nifunguke apa ili nipate ushauri kabla ya kwenda mbele zaidi. Miezi 2 sasa kuna tatizo la kiafya kwenye mwili wangu silielewi. Nimekuwa natoka damu sehemu za haja ndogo.

Yani ni hivi. Nikienda haja ndogo kawaida sipati tatizo ilo ila tu pale nikienda haja kubwa kuna wakati naona sinki limechafuka mstari wa damu ambayo inatokea katika haja ndogo na sipati maumivu yoyote, na hii hali hainitokei mara zote inatokea mara moja moja kitu ambacho kinanipa hofu mnoo na mawazo kutokana na jinsia yangu.

Nimeandika humu leo najua wapo wataalamu wa masuala ya kiafya wanaweza kunishauri nifanyaje niondokane na hili tatizo na kama nahitaji utatuzi zaidi niwapi sehemu sahii.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana kabisa damu kutoka kwenye njia ya haja ndogo wakati wa kujisaidia haja kubwa au hata unapokua na kikohozi muda mwengine. Ni tatizo linafahamika na linatibika. Wahi tu kwa daktari wala usiogope.
 
Back
Top Bottom