Nahitaji kufahamu hii hali kukojoa mkojo wenye damu

PierreLiquid

JF-Expert Member
Oct 16, 2019
873
1,000
Habari, wakubwa heshima yenu.

Mimi ni kijana umri ni 25 Me, kwanza nianze kwa msemo wa kiswahili usemao "mficha maradhi kifo humuumbua" nimeona leo nifunguke apa ili nipate ushauri kabla ya kwenda mbele zaidi. Miezi 2 sasa kuna tatizo la kiafya kwenye mwili wangu silielewi. Nimekuwa natoka damu sehemu za haja ndogo.

Yani ni hivi. Nikienda haja ndogo kawaida sipati tatizo ilo ila tu pale nikienda haja kubwa kuna wakati naona sinki limechafuka mstari wa damu ambayo inatokea katika haja ndogo na sipati maumivu yoyote, na hii hali hainitokei mara zote inatokea mara moja moja kitu ambacho kinanipa hofu mnoo na mawazo kutokana na jinsia yangu.

Nimeandika humu leo najua wapo wataalamu wa masuala ya kiafya wanaweza kunishauri nifanyaje niondokane na hili tatizo na kama nahitaji utatuzi zaidi niwapi sehemu sahii.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
2,876
2,000
Kwanza nikupe pole mkuu kwa tatizo hilo, lakini la pili nikushauri uende hospital kukaa na tatizo hilo miezi miwili ni hatari sana maana kama ni ugonjwa unakuwa unaendelea kukomaa na hatimaye kuleta athari kubwa kuliko kama ungeuwahi mapema.

Wakati mwingine ukiona dalili usizozielewa kwenye mwili ni vyema ukajisalimishe hospital mapema.
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
5,740
2,000
🤔 PierreLiquid hii kitu nahisi chimboko lake inawezakua mambo ya kiroho.
Kisayansi sidhani.

Pia una mwili wa mazoezi vizuri sindio?
 
PierreLiquid

JF-Expert Member
Oct 16, 2019
873
1,000
Sawa
Kwanza nikupe pole mkuu kwa tatizo hilo, lakini la pili nikushauri uende hospital kukaa na tatizo hilo miezi miwili ni hatari sana maana kama ni ugonjwa unakuwa unaendelea kukomaa na hatimaye kuleta athari kubwa kuliko kama ungeuwahi mapema

Wakati mwingine ukiona dalili usizozielewa kwenye mwili ni vyema ukajisalimishe hospital mapema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,180
2,000
Habari, wakubwa heshima yenu.

Mimi ni kijana umri ni 25 Me, kwanza nianze kwa msemo wa kiswahili usemao "mficha maradhi kifo humuumbua" nimeona leo nifunguke apa ili nipate ushauri kabla ya kwenda mbele zaidi. Miezi 2 sasa kuna tatizo la kiafya kwenye mwili wangu silielewi. Nimekuwa natoka damu sehemu za haja ndogo.

Yani ni hivi. Nikienda haja ndogo kawaida sipati tatizo ilo ila tu pale nikienda haja kubwa kuna wakati naona sinki limechafuka mstari wa damu ambayo inatokea katika haja ndogo na sipati maumivu yoyote, na hii hali hainitokei mara zote inatokea mara moja moja kitu ambacho kinanipa hofu mnoo na mawazo kutokana na jinsia yangu.

Nimeandika humu leo najua wapo wataalamu wa masuala ya kiafya wanaweza kunishauri nifanyaje niondokane na hili tatizo na kama nahitaji utatuzi zaidi niwapi sehemu sahii.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda hospitali
 
Mrs Van

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
5,026
2,000
Kama ukienda haja kubwa ndio unaona mchirizi inawezekana labda ni choo ndio kinatoa damu. Cha msingi nenda hosptal ukafanye checkup inawezekana shida ikawa upande wa mkojo au upande wa tumbo.
 
Nima Imma

JF-Expert Member
May 14, 2015
2,319
2,000
Pierr kata bima ya NHIF kama hauna nenda katibiwe ndugu yangu,, ila angalia tena vyema inatoka mbele ama nyuma kama ni nyuma ni bawasiri ,,na ukifika kwa dr. Wala usiogope kuongea mwelezee mwanzo mpaka mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom