Nahitaji kubadilisha fani ya uwalimu

Acha kwanza huo Ualimu.
Njoo mtaani! Tukae kidogo halafu ujifunze Computer na ICT utapata connection ya Uhamiaji kirahisi sana mkuu.
Trust me!! Na akili itakukaa sawa.

Mtaani nimekaa miaka 5 bila ajira hivo najua harakati Za kitaa vizuri kaka usionge kuwakatisha watu tamaa kama unauwezo wa kumshauri mtu mshauri
 
mkuu pole sana na changamoto yako

Piaa pole na changamoto za sisi wakosoaji kwenye uzi wako. watu wamekosoa kwa sababu unainekana hujui unachotaka au kama unakijua umeshindwa kukielezea

Any way............

Elimu ambayo inakutambukisha kifani ni Degree. Hii ni muhimu sana.
Usijiangaishe na mambo ya post graduate hasa kama degree yako ya kwanza ni ya ualimu.

Fanya hivi, Soma Diploma potential ya kile unachokitaka, au kama una nguvu soma degree upya kabisa ndio uamze kutafuta ajira upya au kufanyiwa Recategorization

Pia kama hutojali, Jifunze fani ya udereva na uwe compitent uwe VIP driver halafu anza kuvizia nafasi za udereva kwenye Taasisi/ Mashirika ya umma. Huko kuna madereva wana hela hata maofisa wako hapo shuleni au wilayani hawatii mguu.

Kufanya icho nilicho kueleza haizidi mwaka mmoja kama utakuwa flexible.

Shukran sana kaka udereva naujua wa kitaa tu ila bado leseni maana kipindi nasubiri ajira miaka hiyo mitano nimejichanganya sana na mafuso, ufundi rangi na ujenzi
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unazopata kutoka kwa wadau.

Naomba nikutaarifu kuwa kwa ngazi uliyonayo sasa( degree) ndio ngazi kubwa ya elimu inayotambuliwa na serikali. Ni ngumu sana hata kupata ruhusa kwa mwajiri wako kwenda kuchukua degree nyingine. Yaani akupe ruhusa ya miaka mitatu au minne? Ni ngumu.! Ruhusa unayoweza kupata wew ni ruhusa ya miezi isiyozidi 18, yaan wakiamini unaenda kujiendeleza kwa ngazi ya masters! Ungekuwa umeajiriwa na diploma ungekuwa na nafasi hiyo ila kwa degree hapana!

USHAURI
Achana na mawazo ya kubadili hiyo fani kwani ni ngumu kupata ruhusa.
Jambo la msingi pambana ukasome Masters yoyote inayorelate na mambo ya uongozi na zaidi na zaid... Wakati huo kama utaweza jiingize kwenye siasa ya chama tawala uuze CV yako na
ili uweze pata connection mbalimbali ikiwemo kuteuliwa kuwa afisa elimu wilaya au mkoa!

Asante kaka ila changamoto ukisoma masters kwenye education inakuwa ni advantage tu kwako ila sio kimaslahi (mshahara)
 
Sikia huu USHUHUDA labda UTAWEZA kukusaidia..

Niliajiriwa Idara x katika halmashauri z, nilikua na diploma.

Ila kiukweli Mimi nilipenda sanaa fani y.

Baada ya miaka 2 nika apply chuo course y na kuomba ruhusa ya masomo.

Nikaenda kusoma masomo ya fani y.

Nikaunga na masters kabisaa ya fani y.

Nilivyorudi kutoka masomoni nikahamishiwa bomani kutoka kijijini nilipokuwa naitumikia fani x, nikawa mfanyakazi wa Idara y bomani.

Nikakuta mkuu wa Idara y amepata shavu la kwenda kusoma phD ulaya, hivyo nikawa na kaimu huku jamaa ananifundisha kazi.

Nasubiri mwezi wa 7 kufanyiwa RECATEGORIZATION ili niwe mkuu wa Idara kamili wa y.

Then na wewe.....

Nenda chuo kasome bachelor ya IT then maliza.
peleka Cheti kwa utumishi wako subiri RECATEGORIZATION.

Huku unasubiri kubadilishiwa muundo.

Ukimaliza unaweza kuwa unatafuta Kazi kwengine kupitia ajira.go.tz au wizara ya utumishi huwa wanapost nafasi kibao za kufanyia Kazi UN na AU na kwengine huko (int. Org) kwa watumishi wa umma..

Chukua hatua....

Mimi nilichukua hatua, sikutaka ndoto zangu zife.

Sikuipenda Kazi x, umasikini wa nyumbani ulinifanya nikaisomee na kuajiriwa serikalini ili tu nitoke kwenye mikono ya kulelewa na ndugu.

Sikuacha ndoto zangu za kuwa y KUFA.

#YNWA
 
Daah yan nimesoma nikajikuta mpka machozi yana nitoka mkuu mungu akubariki uwe na moyo huo huo usiwe kama wengine wanakatisha watu tamaa Asante sana kaka ngoja nifanyie Kazi ushauri wako niishi ndoto zangu
Mkuu wa majeshi mstaafu mzee wetu Gen (Ret). D. Musuguri aliwahi sema siku ambayo katimiza miaka 100 ya uhai wake mambo muhimu matatu.

Kama mwanaume

1. Hutakiwi kukata tamaa

2. Hutakiwi kuogopa chochote chenye lengo chanya.

3. Kupambana mpaka mwisho.
 
Uhamiaji niki maanisha wizara ya uhamiaji nimesema fani niki maanisha IT au computer science nafikiri uwandishi ila natumaini umenielewa
Mkuu tulia Basi da!Wizara ya uhamiaji Waziri wake nani? nikupe connection.
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unazopata kutoka kwa wadau.

Naomba nikutaarifu kuwa kwa ngazi uliyonayo sasa( degree) ndio ngazi kubwa ya elimu inayotambuliwa na serikali. Ni ngumu sana hata kupata ruhusa kwa mwajiri wako kwenda kuchukua degree nyingine. Yaani akupe ruhusa ya miaka mitatu au minne? Ni ngumu.! Ruhusa unayoweza kupata wew ni ruhusa ya miezi isiyozidi 18, yaan wakiamini unaenda kujiendeleza kwa ngazi ya masters! Ungekuwa umeajiriwa na diploma ungekuwa na nafasi hiyo ila kwa degree hapana!

USHAURI
Achana na mawazo ya kubadili hiyo fani kwani ni ngumu kupata ruhusa.
Jambo la msingi pambana ukasome Masters yoyote inayorelate na mambo ya uongozi na zaidi na zaid... Wakati huo kama utaweza jiingize kwenye siasa ya chama tawala uuze CV yako na
ili uweze pata connection mbalimbali ikiwemo kuteuliwa kuwa afisa elimu wilaya au mkoa!
Kusoma Masters tofauti na degree ni kupoteza muda.

Kuruhusiwa unaweza kabisa.

Ngoja Nikupe mifano miwili ya watu niwajuao.

1. Huyu Alisoma BAED with IT, kwahiyo aliajiriwa kama mwalimu Ila alipambana akahamishiwa bomani kuwa IT.
Akiwa bomani amesoma Dip ya IT na na mwaka huu ameomba ruhusa akasoma Bach. Ya IT.
Na taarifa chini ya kapeti ni kwamba barua yake imetoka, unasubiriwa muda muafaka wapewe barua zao waliomba. Na jina lake lipo..!!

2. Huyu Alisoma BAED, alipambana akaingia bomani, Ila yeye ndoto zake ni kuwa Muhasibu.
Hivi navyoandika hapa kamaliza semester ya kwanza open ya Accounts.

Kusoma masters tofauti na bachelor yako sio ushauri mzuri.

Hata waziri mkuu (Majaliwa) alishawahi kulisema hili.
Na alishauri watumishi wasome masters za bachelor zao.

Simshauri kabisaa asome masters isiyo ya bachelor yake Wala diploma.

Chakusoma ni hiyo Bach ya IT.
Na si lazima aende full time (huenda ana michongo yake, then akienda chuo itafeli), asome tu open.

Maana changamoto ya kwenda chuo mtumishi wa Umma, kama unategemea posho kutoka ofisini ina maana utazikosa zotee.

#YNWA
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...
Nadhani ameelewa, Ila lililokuu asisome masters nyengine ili ahame Idara.

Anachotakiwa ni kutafuta bachelor nyengine ili afanyiwe Recategorization au ataomba ajira mpya ofisi nyengine kama huko uhamiaji akutakako.

Na kama anaona kurudi chuo Tena ni changamoto basi asome OPEN.

Mimi nadhani asisome bachelor nyingine bali akasome tu masters ya bachelor yake ya kwanza. Huoni kama kusoma bachelor nyingine ni kujipotezea muda?
 
Mimi nadhani asisome bachelor nyingine bali akasome tu masters ya bachelor yake ya kwanza. Huoni kama kusoma bachelor nyingine ni kujipotezea muda?
Serikali haiajiri masters.
Masters ni added advantage.
Mfano niliajiriwa na diploma, nikaomba ruhusa ya kwenda masomoni.
Huko masomoni nikachukua bachelor na masters.

Nimesoma bachelor tofauti na diploma yangu hivyo nimefanyiwa recategorization.

Nimehamishwa idara (kwasababu ya bachelor) ila nimekuwa mkuu wa Idara kwasababu ya masters.

Then iliyonipeleka kwenye hiyo Idara ni bachelor na ndio iliyonifanya nifanyiwe recategorization.

Mind you, kwenye utumishi wa umma Kuna categorization na recategorization, ni vitu viwili tofauti.

Pia hapo juu nimetoa mfano wa walimu walioajiriwa na bachelor ila kwasasa wanasaka post nyengine kwenye Idara nyengine.
Zisome utaelewa.

#YNWA
 
Serikali haiajiri masters.
Masters ni added advantage.
Mfano niliajiriwa na diploma, nikaomba ruhusa ya kwenda masomoni.
Huko masomoni nikachukua bachelor na masters.

Nimesoma bachelor tofauti na diploma yangu hivyo nimefanyiwa recategorization.

Nimehamishwa idara (kwasababu ya bachelor) ila nimukuwa mkuu wa Idara kwasababu ya masters.

Then iliyonipeleka kwenye hiyo Idara ni bachelor na ndio iliyonifanya nifanyiwe recategorization.

Mind you, kwenye utumishi wa umma Kuna categorization na recategorization, ni vitu viwili tofauti.

Pia hapo juu nimetoa mfano wa walimu walioajiriwa na bachelor ila kwasasa wanasaka post nyengine kwenye Idara nyengine.
Zisome utaelewa.

#YNWA
... vipi ikitokea mfano umeajiriwa kwa, say, Bsc Ed. Kutokana na mazingira baadae ukasomea, say, diploma ya Computer Science, ukafanyiwa recategorisation.
Vipi kwenye ngazi ya masters ukisomea CS kwa kutumia cheti cha Bsc Ed japo kwa sasa umeajiriwa kwa diploma ya CS?
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unazopata kutoka kwa wadau.

Naomba nikutaarifu kuwa kwa ngazi uliyonayo sasa( degree) ndio ngazi kubwa ya elimu inayotambuliwa na serikali. Ni ngumu sana hata kupata ruhusa kwa mwajiri wako kwenda kuchukua degree nyingine. Yaani akupe ruhusa ya miaka mitatu au minne? Ni ngumu.! Ruhusa unayoweza kupata wew ni ruhusa ya miezi isiyozidi 18, yaan wakiamini unaenda kujiendeleza kwa ngazi ya masters! Ungekuwa umeajiriwa na diploma ungekuwa na nafasi hiyo ila kwa degree hapana!

USHAURI
Achana na mawazo ya kubadili hiyo fani kwani ni ngumu kupata ruhusa.
Jambo la msingi pambana ukasome Masters yoyote inayorelate na mambo ya uongozi na zaidi na zaid... Wakati huo kama utaweza jiingize kwenye siasa ya chama tawala uuze CV yako na
ili uweze pata connection mbalimbali ikiwemo kuteuliwa kuwa afisa elimu wilaya au mm
Ujuzi au fani ya mtu inapimwa na degree uliyosomea kwa mfano diploma ulisoma clinical officer alafu degree ukasoma Account basi wewe serikali itakujua wewe ni muhasibu na sio mtu wa afya. Ukiajiriwa na bachelor kiserikali hiyo wataitambua ndio fani yako huwezi kufanya recategorization kwa elimu ya postgraduate. Labda ufanye mchongo wa kutoka taasisi y kwenda x. Ila siyo kufanya recategorization hiyo postgraduate serikali hawaitambui kama ndio fani yako, fani yako ni bachelor
 
Nimechoka tu na taaluma ya ualimu Kazi nyingi maslahi madogo wakati kuna watu wana level ya Elimu hiyo hiyo lakin maslahi yao makubwa niliwaza nijiendeleze nikasome postgraduate diploma ya computer science au IT ni hame kabisa kutoka Ualimu niende sector nyingine ndani ya serikali niombe kubadilishiwa
Kwahiyo huko uhamiaji kuna mishahara minono eenh!!

how does it range!!
 
Ujuzi au fani ya mtu inapimwa na degree uliyosomea kwa mfano diploma ulisoma clinical officer alafu degree ukasoma Account basi wewe serikali itakujua wewe ni muhasibu na sio mtu wa afya. Ukiajiriwa na bachelor kiserikali hiyo wataitambua ndio fani yako huwezi kufanya recategorization kwa elimu ya postgraduate. Labda ufanye mchongo wa kutoka taasisi y kwenda x. Ila siyo kufanya recategorization hiyo postgraduate serikali hawaitambui kama ndio fani yako, fani yako ni bachelor
Anaweza kusoma degree nyengine then anafanyiwa recategorization.

#YNWA
 
... vipi ikitokea mfano umeajiriwa kwa, say, Bsc Ed. Kutokana na mazingira baadae ukasomea, say, diploma ya Computer Science, ukafanyiwa recategorisation.
Vipi kwenye ngazi ya masters ukisomea CS kwa kutumia cheti cha Bsc Ed japo kwa sasa umeajiriwa kwa diploma ya CS?
Serikali inaajili bachelor.
Before kuitambua hiyo masters watataka bachelor kwanza.

#YNWA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom